natafuta house girl/msaidizi wa kazi za nyumbani

looohhh kuweni serious, niwatumie wa kuoka huku bukoba. Wana maji hao, yaani kwa mumeo uwe chonjo!!!!
 
Utingo we una wife?we unafanya kazi nae pia?je uko hapa town home unatoka na kurudi saa ngapi?

nina mke, watoto watatu wote wako shule boarding, nina duka la hardware, wife ndiye meneja & cashier, mimi ndiye supervisor wa vijana wa kupakia na kupakua mizigo, na mkurugenzi mkuu.

Kazi kwenu waoga wa kujasiria mali, mwapenda kuajiriwa tu na kukaa kwenye viyo yozi visivyo kuwa vyenu, mtapata ma-pressure mpaka mkome.:smile-big:
 
hayajakukuta.wala hayajakufika majukumu!!!!

halafu....... nyie mnaosema ni uvivu kwani nyie mnategemea wenzenu kukosa kazi na zilivyoadimika na elimu ni ndogo wataishije?

Tusaidiane/tugawane jamani si kila kitu unataka kung'ang'ana mwenyewe!
 
shosti majukumu hayakutinga ukaifahamu vizuri hii ishu!

hamna cha majukumu wala nini,kila mtu anatingwa na majukumu,kujiendekeza tu na kwa vile wanapatikana kwa vimishahara finyu,kinyume chake ungeelewa namaanisha nini.
 
Hivi ni uvivu au kitu gani,kwa nini kila mtu anatafuta msaidizi nashindwa kuelewa.
Sioni ubaya kutafuta msaidizi ikiwa mume na mke wote wanafanya kazi nje ya nyumba, vyenginevyo hata mimi nashindwa kuelewa.
 
Bado sijaona ambaye ametoa mchango wa kumsaidia huyu dada zaidi ya kulaumu na kurushana roho.
 
Sioni ubaya kutafuta msaidizi ikiwa mume na mke wote wanafanya kazi nje ya nyumba, vyenginevyo hata mimi nashindwa kuelewa.

hata kama mnafanya kazi nje ya nyumba,nafikiri mkijipangilia wewe na mumeo utaratibu mzuri kabisa hamuhitaji mtu wa kuwasaidia na vilevile inazidisha upendo kati yenu
 
hata kama mnafanya kazi nje ya nyumba,nafikiri mkijipangilia wewe na mumeo utaratibu mzuri kabisa hamuhitaji mtu wa kuwasaidia na vilevile inazidisha upendo kati yenu
Inawezekana ukawa uko "right", Shosti. Ulimwengu wa leo tunajaribu kurahisisha mambo ili kutaka kwenda na wakati, matokeo yake pale "unapojaribu" kutatua tatizo unashtukia unaanzisha tatizo jengine.
Anyway, Every one is a slave/master of his/her deeds.
 
Thanks Mammamia.I think we are on the same track!

Shost mipangilio ipo tu ila kuna mambo yanataka kidogo usaidizi.

Kuna shughuli kwa mfano kuchota maji ambayo yanatoka siku yoyote bila taarifa hii nayo unaipangilia vipi kama si kutafuta tatizo jingine la kukimbizana na kununua maji achia mbali maswala ya kua na mtoto mdogo.

moz-screenshot-1.png
Anyway Special thanks ziende kwa mammamia kwa kutambua what i want and why.
 
hawa wapo ila hawana guarantee
jana nikiwa mahali nikisubiri kuoshewa gari nilibahatika kuongea na wasichana wadogo wawili walioajiriwa kazi za kusaidia mama lishe,walinieleza kuwa wanalipwa sh 2,000 kwa kutwa lakini wakipata kazi ya mshahara wa kudumu,malazi na chakula watafurahi sana kwani katika hii ikitokea wanaumwa basi hawaingizi kitu kwa siku hiyo
kama bado unahitaji tuwasiliane uwajaribu hao
 
Siku hizi mayaya hawatoki Iringa/Mbeya na Lindi wanatoka Singida/Kondoa na Manyara kama una mume macho juu juu sikushauri hawa, kinadada wengi wamelia.
 
hawa wapo ila hawana guarantee
jana nikiwa mahali nikisubiri kuoshewa gari nilibahatika kuongea na wasichana wadogo wawili walioajiriwa kazi za kusaidia mama lishe,walinieleza kuwa wanalipwa sh 2,000 kwa kutwa lakini wakipata kazi ya mshahara wa kudumu,malazi na chakula watafurahi sana kwani katika hii ikitokea wanaumwa basi hawaingizi kitu kwa siku hiyo
kama bado unahitaji tuwasiliane uwajaribu hao

Asante sana Mkuu.
Ngoja nikupm.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom