Usikute ni agano baya la kipepo walifanya wazazi mababu na mababu, kataa hilo agano huku ukiomba na kusema navunja agano na shetani likome kizazi na kizazi chako kijacho katika jina la YESU
Usikute ni agano baya la kipepo walifanya wazazi mababu na mababu, kataa hilo agano huku ukiomba na kusema navunja agano na shetani likome kizazi na kizazi chako kijacho katika jina la YESU
Uko BONGO au ULAYA ,.?mtafute SPEECH THERAPIST,.huyo ana elimu ya kuwasaidia watu kama hao,.hata mabubu,wenye vithemi,waliozaliwa na midomo ya sungura[cleft palate] na watu waliopatatwa na stroke pia,.kwa bahati mbaya kwa Tazania to the best of my knowladge hayupo,.aliyekuwepo aliondoka,..mdogo wangu aliyepo marekani alihudhuria mafunzo yake na sasa hivi anaongea vizuri
Ushauri ninaoweza kukupa ambao utapunguza taratibu kigugumizi cha mtoto wako ni huu:
1. Wakati anapozungumza na kukwama, asitokee mtu kutaka kumkwamua kwa kumalizia neno aliloanza. Mwacheni ajitahidi mwenyewe hata kama itapita dakika nzima. Kumsaidia/kumkwamua kunamfanya ajihisi vibaya na kisaikolojia hii inamuathiri kwa kuhisi kuwa "hana anachokijuwa)...
Kuna tafauti baina ya dawa na tiba.
Dawa kwa maana ya vidonge zipo: benzodiazepines, anti-convulsanta, anti-pressants, antipsychotic na antihypetensive (Nimeziona hizi kutoka Wikipedia, lakini mti akiamua kutumia dawa SIKU ZOTE IWE NI KWA USHAURI WA DAKTARI...
Mamamia thx for ur advice, na raia fulani don't just generalize kwa kusema hakina dawa,
Pia mwanangu alipoanza kuongea alikuwa nacho bahati nzuri watoto wadogo walikuwa wengi mtaani kwetu na walipenda sana kuimba, basi tulishahama ila kiliisha kabisa, sijui ni zile nyimbo ama ni nini?
Namshukuru Mungu
Pole sana, najua unavyojisikia ksb nami nilikuwa mhanga wa tatizo hili.
Mwanangu alikuwa na kigugumizi kikali kweli (anajipiga mikono au kichwa anainama na kuinuka mpaka ) mimi nilikuwa najihisi kulia, nilikosa amani hata nilipompeleka shule,nilimwambia mwalimu wake tatizo lake, bahati nzuri yule mwalimu wake alipokuwa mdogo naye alikuwa na tatizo kama la mwanangu akanambia wala nisijali atakwenda naye vizuri tu wala nisiwe na wasiwasi..
Kigugumizi hakirithiwi ila kinaigwa. Kinapanda zaidi akiwa na hasira,furaha au shauku ya kueleza kitu. Mpe muda wa kutosha akiongea,usimkatishe wala kumuonyesha kuwa ana tatizo. Kwa umri wake ana uwezo wa kuacha kama ata interact na watoto wenzie wanaoongea kawaida.