Natafuta daktari wa mifupa!

Sebali

Member
Apr 24, 2011
38
1
Naombeni ushauri wenu wana Jf. Mimi nilipata ajali barabari hivyo kuna mfupa umevunjika sehemu ya nyongo ktk mguu. Hivyo naomba mnishauri sehemu ambapo kuna mtaalamu/watalaamu freshi wa mifupa.Mimi napatikana Dar na Mbeya. Naombeni ushauri wenu!
 
Sijakuelewa hiyo ni sehemu gani...umepata huduma yeyote tayari? Mfupa unapovunjika huwa unajiunga wenyewe, labda kama huo mfupa umetokeza nje basi utahitaji operation ili kufunga chuma na kuruhusu uchafu utoke. Kama haujitokeza kwa nje, basi unahitaji kunyooshwa ili uunge bila kupinda. Hayo yanatakiwa yafanyike mara moja baada ya kuvunjika.

Kama hayo yalifanyika na mfupa haukuunga, au umeinga vibaya, then hapo unaweza panga kutafuta daktari bingwa wa mifupa kwa ushauri na/au huduma zaidi.

Madaktari wa mifupa wapo wengi Dar es salaam. Muhimbili kuna kitengo cha mifupa kinaitwa MOI, kuna madaktari bingwa wanapatikana pale kwa emergency (casualty), clinic za kawaida na clinic za kulipia (fast track). Nakushauri uende hapo. Lakini pia kana una hela kuna hospital private nyingi tu kama Aga Khan, Hindu Mandal, Tumaini, TMJ, Regency...zina madaktari bingwa wa mifupa uatapatiwa huduma husika.

Pole sana kwa ajali.
 
nenda kitengo cha moi, pale muhimbili wanawataalam na vifaa vya hali ya juu
 
Naombeni ushauri wenu wana Jf. Mimi nilipata ajali barabari hivyo kuna mfupa umevunjika sehemu ya nyongo ktk mguu. Hivyo naomba mnishauri sehemu ambapo kuna mtaalamu/watalaamu freshi wa mifupa.Mimi napatikana Dar na Mbeya. Naombeni ushauri wenu!

Nenda Barere Hospital-Kibaha kwa Dr. Bake!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom