kanyagio
JF-Expert Member
- Dec 10, 2009
- 1,021
- 365
Ndugu wajumbe, nimekuwa nikifikiria sana kuhusu kilimo na kuona kinaweza kulipa hasa ukizingatia kuwa kwa sasa kuna kilimo kwanza (naamini kuna upande mzuri wa huo mkakati). kwa sasa nimeanza kidogooooo kulima miti ya mbao wilaya ya Bagamoyo. nimepata ka-adhi kadogo kama ekari tano kwa ajili ya kupanda miti na nimeshapanda mitiki.
kwa sasa nataka kupanuka na kununua ardhi kubwa kwa ajili ya kilimo kikubwa. kwa msingi huu ninaomba msaada wenu kuhusu masuala haya:
nawasilisha
kwa sasa nataka kupanuka na kununua ardhi kubwa kwa ajili ya kilimo kikubwa. kwa msingi huu ninaomba msaada wenu kuhusu masuala haya:
- Wapi ninaweza kupata ardhi ya bei nafuu sijalishi mkoa, ila angalau eneo liwe linafikika kwa usafiri wa gari na kuna rutuba na source ya maji (specificity is needed)
- Je bei ya mashamba ni kiasi gani? on average?
- Je kwa sasa kilimo gani kinalipa kwa kuzingatia huitaji inputs kubwa.
nawasilisha