Nasubiria Salamu za Rais LEO!

chuwaalbert

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
3,598
2,115
Ndugu wana JF, leo mwaka wa 2011 unaisha. Kama kawaida Rais atatuhutubia na kutueleza vipaumbele vyake vya mwaka unaofwata. Ubaya ni kuwa mengine anakuja fanya ambayo hayakuwa kipaumbele chake, matokeo yake anayatekeleza VIBAYA! Kwa nfano, suala la Katiba mpya, aliibuka nalo hewani pale alipotuhubia mwishoni mwa mwaka jana, wakati kwenye kampeni za kuusaka ulaji hili halikuwa kipaumbele chake na chama chake! Mwaka huu ataibuka na lipi?
1. Tungependa kupata ufafanuzi wa VITAMBULISHO vya TAIFA. Zoezi linaendeleaje?
2. Tngependa kujua anayachukuliaje mapendelezo ya wadau kuhusu sheria ya Katiba mpya.
3. Tungependa kujua msimamo wake kuhusu kulipwa kwa DOWANS!
Nawasilisha!
 
Pole sana kama unasubiri la maana toka kwa huyo kiumbe!
Nunua dawa za BP mapema,kwa sababu hata leo atadanganya kama siku zingine!
 
Huna haja ya kusubiri kwani hata kabla hajasema wewe umeshampangia aseme nini
 
Hana la kusema aibu tupu hii nchi, hakuna ajira, mafuta disaster, mafuriko, mishahara mpaka sasa kwa baadhi ya sekta bado hawajapata. Ushauri wangu kwa JK we lala tu, kula mwaka mpya kwa raha zako. hatutaki kukuona kwe TV. Kichefuchefu. Khaaaaaa!!!!:yawn::yawn:
 
labda kama unataka kuangalia tabasamu lake maana ataanza kukenuakenua kama mwanamke anetekenywa tekenywa hamna jipya kwake, ni heri angewahutubia mke wake na watoto wake
 
Katika matukio ambayo hayapo kabisa kichwani mwangu ni hotuba ya kikwete ya kuaga mwaka. Sidhani kama ataongea la maana zaidi ya kusema NCHI IMEENDELEA KUWA YA AMANI NA USALAMA NA HALI YA UCHUMI IMEENDELEA KUBOREKA. Katika suala la uchumi anaweza kusema kwamba TANZANIA NI MIONGONI MWA NCHI TANO DUNIANI AMBAZO UCHUMI WAKE UNAKUA KWA KASI SANA. Anaweza kuwachanganya wananchi kwa kusema kwamba KUPANDA KWA GHARAMA YA MAISHA NI TATIZO LA KIDUNIA. Baada ya hapo atajisifu kwa hatua aliyofikia ya uundaji wa katiba mpya. Mwisho atawaahidi wananchi kwamba atajitahidi kuendelea na jitihada zake za kuzunguka dunia kuomba misaada ili awakomboe wananchi kiuchumi. Baada ya hapo wimbo wa MUNGU IBARIKI AFRIKA utaimbwa. Kisha, atawashukuru wananchi kwa kumsikiliza.

Sasa hotuba kama hiyo niisikilize ya nini! Nisije nikapata hasira na kushikwa na BP bure halafu niage dunia na kuwaachia mateso mke na watoto wangu.
 
Hapa nrb tayari Kibaki katoa salama za mwaka mpya saa kumi jioni. Amezungumia kuimarika kwa miundo mbinu hasa barabara, mpango wa devolution of power to county level(madaraka serekali za majimbo), kuimarika kwa ksh kupelekea kupungua kwa mfumuko wa bei, pia aligusia uchaguzi ujao na umuhimu wa vijana kuchangamkia fursa za soko la pamoja EA. Hapa kazi iliyobaki ni moja tu kujumuika na ma beauty wa jiji kukaribisha mwaka. Heri ya mwaka mpya wana JF.
 
pole sana! endelea kumsubiri mbumbumbu aongee ati mambo ya maana yanayo ikabili nchi. utasubiri mpaka kesho. happy new year
 
Hana la kusema aibu tupu hii nchi, hakuna ajira, mafuta disaster, mafuriko, mishahara mpaka sasa kwa baadhi ya sekta bado hawajapata. Ushauri wangu kwa JK we lala tu, kula mwaka mpya kwa raha zako. hatutaki kukuona kwe TV. Kichefuchefu. Khaaaaaa!!!!:yawn::yawn:

ole wangu nikijaribu kuangalia hotuba yake!! mwaka mzima unaweza ukawa nuksi.
 
Ndugu wana JF, leo mwaka wa 2011 unaisha. Kama kawaida Rais atatuhutubia na kutueleza vipaumbele vyake vya mwaka unaofwata. Ubaya ni kuwa mengine anakuja fanya ambayo hayakuwa kipaumbele chake, matokeo yake anayatekeleza VIBAYA! Kwa nfano, suala la Katiba mpya, aliibuka nalo hewani pale alipotuhubia mwishoni mwa mwaka jana, wakati kwenye kampeni za kuusaka ulaji hili halikuwa kipaumbele chake na chama chake! Mwaka huu ataibuka na lipi?
1. Tungependa kupata ufafanuzi wa VITAMBULISHO vya TAIFA. Zoezi linaendeleaje?
2. Tngependa kujua anayachukuliaje mapendelezo ya wadau kuhusu sheria ya Katiba mpya.
3. Tungependa kujua msimamo wake kuhusu kulipwa kwa DOWANS!
Nawasilisha!
Yaani wewe ndo hewa kabisa! Badala ya kufikiria masuala ya msingi kama ajira,umeme unaleta bla bla,umetumwa nini? Ndo nyie mnaoandaliwa maswali ya kumuuiza mtu
 
Back
Top Bottom