Nasubiria fidia ya gongo la mboto, ole wao iwe chini ya milioni 100

komredi ngosha

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
382
71
Wan Jf, nilisikia hivi majuzi wabunge wamepewa milioni 90 kila mmoja kununua magari. Hongera zao. Sasa twende Gongo la Mboto. Matokeo ya uzembe wa wa serikali yameleta maafa na kuua wenzetu. Napendekeza fidia iwe milioni 100 kwa familia iliopoteza ndugu yao. Ndio, thamani ya uhai wa Mtanzania ni kubwa zaidi ya gari ya mbunge. Pia watu hawa wameuliwa ktk maisha yao ya kawaida, wengine wakiwa wanategemewa na jamaa zao hivyo kuacha pengo kubwa ktk maisha yao. Nawasilisha.
 
hiyo ni ndoto kwa serikali hii.Mbagala kuna watu hadi leo hawajalipwa fidia... watavalue vizuri lakini siku cheki ikitoka unakuta wameslash 90% bila maelezo
wao hili si muhimu kama VX za wabunge na ndio maana kile kiajuza chao mjengoni kimedai sio suala la dharura
 
Haya si maneno ya busara kwa kipindi hiki kuzungumzia fidia wakati miili iko mochwari hadi hivi sasa. Fidia kwani ndio kitu gani kwa uhai wa mtu?? Usilete mzaha wa aina hiyo ndugu.
 
2891552.jpg
 
Back
Top Bottom