Nasubiri Heshima ya Bunge Kwa General Kyaro

Pasco umekuwa kipofu!
Ina maana wewe hujui kanuni za bunge?
Bunge lina taratibu zake kupokea taarifa rasmi FULL STOP.
sijaona tatizo kwa naibu spika

hizo taarifa wanasubiri ni kutoka kwa madaktari waliomfanyia POSTMOTERM? Spika, naibu spika wote ni CCM na ndio serikali. Waziri wa mambo ya ndani yuko humo. Huu ni ukosefu mkubwa wa nidhamu katika bunge letu.
 
....Ninasubiri, na nitafurahi na kuona kwamba Bunge letu limefanya haki kama litasimama dakika moja tu, kutoa heshima kwa mpendwa wetu, kamanda, aliyekwenda vitani akakoswa risasi na majeshi ya idd Amini kwa niaba yetu, aliyekuwa mkuu wa majeshi ya Tanzania (1988-1994) marehemu General Mwita Kyaro... sitaki mlundikano wa watu, sitaki wabunge watoke bungeni... nataka wabunge wasimame dakika moja tu basi!
Kwani kamanda huyu aliyepigana vita yeye kacheza filamu ngapi mkuu?
 
Ccm wao ni watawala,ila kiukweli wanaongozwa ktk mambo mengi,mfn mdogo ni leo bungeni kupitia kamanda zitto.
 
Wonders will never end in this country, jana kwenye TBC1 kipindi cha Habari ya saa 2 jioni nilitamani kupasua TV ya nyumbani kwangu nilipoona item ya kwanza ya news ni mazishi ya Kanumba, then Mpiganaji aliyetetea taifa lake kwenye vita dhidi ya Nduli Iddi Amin Dada mwaka 1978-79 na hatimaye kuwa CDF kipindi cha awamu ya Rais Alj H Mwinyi, marehemu Ernest Mwitta Kiaro anakuwa item number 2
Afadhali hao, ITV ya fisadi Mengi haikuwa na taarifa hiyo ya mpiganaji huyu kabisa, waliniudhi sana
 
Acheni wabunge wafanye kazi tulizowatuma sio kuomboleza vifo vya kila mtu tafadhari!

Ila naamini ni sahihi pale anapotokea mtu maarufu na mwenye mchango mkubwa katika taifa apewe heshima yake.

Angalia umati uliomzika kanumba zaidi ya watu 600 wamepoteza fahamu, jamaa maarufu anadeserve heshima ya bunge.
Kuzikwa na watu wengi sio tiketi ya kwenda mbinguni
 
Acheni wabunge wafanye kazi tulizowatuma sio kuomboleza vifo vya kila mtu tafadhari!

Ila naamini ni sahihi pale anapotokea mtu maarufu na mwenye mchango mkubwa katika taifa apewe heshima yake.

Angalia umati uliomzika kanumba zaidi ya watu 600 wamepoteza fahamu, jamaa maarufu anadeserve heshima ya bunge.

Ugonjwa huu unaitwa mzoloto wa akili ktk kuchangia mada
 
Kwani kamanda huyu aliyepigana vita yeye kacheza filamu ngapi mkuu?

swala siyo amecheza filamu ngapi, ni heshima kwa mchango wa kila mmoja. Kwanini bunge libague heshima kati ya majemedari waliotoa mchango mkubwa kwa taifa. Kyaro alijitolea uhai wake kwa ajili yetu, ni bahati tu risasi haikumpata ni HERO! pima mwenyewe, mcheza sinema na yule anayesema mimi nife badala ya wewe! lakini ujumbe wangu ni kuwa tusiwabague, ona MAHUNDI amezikwa kama kapuku tu wakati ndo alikuwa anaongoza usalama wa raia miak nenda rudi.
 
Tatizo watu wameguza msiba wa Kanumba mtaji kila mtu anataka aonekane ameshiriki, hivi wewe hushangai kaenda Rais, kaja waziri mkuu makamu naye akaona asipitwe naye ashiriki je ulitegemea bibi kiroboto akae nyuma lazima naye aonekana ameshiriki
 
Kwa kweli hapa ni mtihani mkubwa kwa bunge letu maana kama ni hoja ya mchango wa marehemu hawa kwa taifa hili, mimi naamini mchango wa General Kiaro ni mkubwa sana kwa taifa hili kuliko marehemu Kanumba. Kwa kweli binafsi sitawaelewa kabisa wabunge wetu wasipolitambua hilo na kumpa heshima yake kamanda huyu.
 
Acheni wabunge wafanye kazi tulizowatuma sio kuomboleza vifo vya kila mtu tafadhari!

Ila naamini ni sahihi pale anapotokea mtu maarufu na mwenye mchango mkubwa katika taifa apewe heshima yake.

Angalia umati uliomzika kanumba zaidi ya watu 600 wamepoteza fahamu, jamaa maarufu anadeserve heshima ya bunge.

Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni! Yaani mkuu, kwako wewe na uwezo wote uliopewa na Mungu wa kupambanua mambo unabariki kilichofanywa na bunge kwa sababu hizo ulizozitaja zisizo na mashiko na ambazo nimezipaka rangi nyekundu?
Tukubali kwamba bunge linaendeshwa kisanii na kupindisha kanuni zake.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom