Nassari: Kanisa la KKKT - Dayosisi ya Meru lina miradi ya maendeleo kuliko serikali

Huyu dogo kina Mbowe wasipokuwa makini ndio atakayeizamisha Chadema sasa sijui kama anafahamu hiyo miradi ya Kanisa fedha nyingi zinatoka serikalini.

Serikali ipi hii iliyofulia au ?
 
hivi tusichomuelewa nassari ni kipi?
Mbona kila tangazo la afya utasikia ni kwa hisani ya watu wa USA.
Barabara utasikia kwa hisani ya watu wa japan
kilimo utasikia kwa hisani ya watu wa norway.
Bajeti yetu ni tegemezi kwa asilimia nyingi tu na wawekezaji ni zaidi ya asilimia tisini ni wageni,kwa trend hii utakuwa ni punguhani wa akili kubisha kuwa miradi ya serikali ni michache kulinganisha na KKKT.
 
Nassari anaendelea kuonyesha ni jinsi gani alivyo na uwezo mdogo.

Hata mbumbumbu ukimuuliza kwenye kila eneo analoishi ataje projects ambazo ni gvt sponsored na church/privately sponsored atakuambia kuwa miradi ya gvt ni mingi zaidi.
 
Joshua ameongea ukweli,NI KWELI KWAMBA KKKT WANA MIRADI MINGI KULIKO SERIKALI KWENYE JIMBO LAKE,serikali ina miradi michache mno na ninaitaja hapa yote
1.chuo cha nelson mandela
2.chuo cha CDTI
3.Arusha National Park
4.chuo cha mifugo Liti Tengeru
5.kituo cha uhamilishaji cha taifa (NAIC)


kanisa la KKKT linamiliki miradi ifuatayo
1.ranch 3
2.benki(hamna benki ya serikali arumeru,wala ATM,kuna crdb,nbc,na Meru Community bank)
3.chuo kikuu kishiriki cha makumira-(kina maktaba ya kwanza afrika mashariki na kati,kwa umri na ubora)
4.shule za sekondari zaidi ya 50,zinazojitegemea.
5.vyuo vya ufundi vikubwa 10 vikiwemo chuo cha walemavu usa river,chuo cha leguruki ufundi,chuo cha mshikamano-itambulike katika jimbo la Nassari hakuna chuo cha Veta hata kimoja
6.miradi ya bio-gas.
****kwa muda niliopitapita kwenye jimbo la dogo janja hayo maneno ninaweza nikaamini.

pia isisahaulike kwamba jengo ambalo air Tanzania wamekodi toka zamani lilopo mjini arusha karibu na clock tower linamilikiwa na KKKT.
 
pia isisahaulike kwamba jengo ambalo air Tanzania wamekodi toka zamani lilopo mjini arusha karibu na clock tower linamilikiwa na KKKT...................................[/QUOTE]

Nelson mandela sio ya serikali mkuu ni kazi ya mdhungu hiyo wala serikali isijisifu kuwa inamiliki Nelson mandela.
 
nimesahau kutaja hospitali....hospitali ya rufaa kwenye jimbo la dogo janja ni ndogo,ukilinganisha na za KKKT,hata ukizungumzia mkoa wa arusha kwa ujumla,hospitali kubwa na bora inamilikiwa na KKKT,kwenye sekta ya utalii pia KKKT inamiliki hoteli kadhaa katikati ya mji wa Arusha****walutheri na wakatoliki wanajituma sana mikoa hii....madhehebu mengine tuige yaliyo mema ili tuendelee....serikali yetu haiaminiki tena.
 
Dar wakiristo wengi sana hata mbunge wangu Halima Mdee ni Mkiristo John Mnyika Mkiristo lakini hata siku moja hujawasikia wanakwenda Kanisani kushukuru kwa Baba Askofu kwa kuchaguliwa kuwa wabunge...huyu kijana yeye kila siku anatoa pongezi Kanisani kwa Baba Askofu, ndio maana tunauliza Arumeru hakuna Waislam hata kidogo waliomchagua Nassari.
Mlipotangaza Zanzibar watu wote wasile mchana kwani hakuna wakristo kule?
 
Sikonge City Leo mbunge anaitukana serikali ambayo ndio inatoa mapesa yote hayo kulipa kanisa ili lijenge shule hospitali na makanisa leo anaitukana rudia MOU nasari uko nyuma sana ila kabla ya kuongea fikira hilo kanisa na MOU
 
Last edited by a moderator:
Kijijini kwetu, umeme ni wa kanisa katoliki, maji ya bomba ni mradi wa kanisa katoliki, Kituo cha afya ni cha kanisa katoliki (serikali ina zahanati ambayo kila siku haina dawa), mikopo ya miradi midogo midogo inatolewa na kanisa, mradi wa kuezeka bati nyumba 10 za wananchi wasioweza kununua mabati lakini wameweza kujenga nyumba za matofali ya kuchoma, ni wa kanisa katoliki. Kwa hiyo sioni cha ajabu katika meneno ya Nasari. Miradi ya serikali kijijini
2.jpg
kwetu ni shule za msingi na sekondari, soko na barabara ya vumbi yenye mashimo. Hakuna cha zaidi.

Ni kweli nyie Chadema mnaunga mkono Kanisa la Meru lina miradi mingi kuzidi Serikali ya Tanzania?
 
Siku zoate huwa nasisitiza kwamba chama chadema ni makini that why chadema wanachukua vijana kama dogo janja for that brave.
Vijana wanajua kuchallange sn as u can see dogo janja, wazee ubongo una virus.
 
Huyu dogo kina Mbowe wasipokuwa makini ndio atakayeizamisha Chadema sasa sijui kama anafahamu hiyo miradi ya Kanisa fedha nyingi zinatoka serikalini.

serikali ombaomba inahitaji kusaidiwa
 
Huyu dogo kina Mbowe wasipokuwa makini ndio atakayeizamisha Chadema sasa sijui kama anafahamu hiyo miradi ya Kanisa fedha nyingi zinatoka serikalini.
EA

TOA MAWAZO MGANDO, ALIONGEA KITU ALICHOKIONA, KUNA JENGO LIMEJENGWA KWA tSH 45M NA BIBI WA 90 , NA HOSTEL YA KANISA WAMEJITOLEA WATU, SASA KWA NINI ASIJUE?
 
Nimegundua kwa nini Nassari anataka lianzishwe taifa la Kaskazini majuzi kasema hii nchi ni laini kama maini...halafu huyu Askofu Akyoo nae anamdanganya huyu mtoto...hivi Arumeru hakuna Waislam?

Mkuu nenda Meru utaiona hiyo miradi, na Nassari hajasema Meru hakuna waislamu yeye amesema tu KKKT ina miradi mengi kuliko serikali. Ukienda Meru utaona miradi hiyo inahudumia wote wakristo na waislamu.
 
MoU inasaidia kanisa kufanya miradi yake. Funguka.

Hata taasisi ya kiislamu ya Aghakhan ina MOU na serikali, na hawalipi kodi kabisa. Hata wao MOU yao inawasaidia wajiendeleze hata kuwa na hospitali zenye gharama kuliko hospitali binafsi zisizo na ruzuku. Funguka na uangalie upande wa pili pia.
 
Hata taasisi ya kiislamu ya Aghakhan ina MOU na serikali, na hawalipi kodi kabisa. Hata wao MOU yao inawasaidia wajiendeleze hata kuwa na hospitali zenye gharama kuliko hospitali binafsi zisizo na ruzuku. Funguka na uangalie upande wa pili pia.

Kumbe kkkt ni taasii? mie nilifikiri kanisa!

Agakhan unawajuwa au unawasikia tu?

The Aga Khan Development Network (AKDN) is a group of development agencies with mandates that include the environment, health, education, architecture, culture, microfinance, rural development, disaster reduction, the promotion of private-sector enterprise and the revitalisation of historic cities. AKDN agencies conduct their programmes without regard to faith, origin or gender.

Soma zaidi: Aga Khan Development Network
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom