Nassari Azidi kuchangiwa Arumeru

mgeni wenu

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
3,664
1,730
Mgombea wa kiti Cha ubunge katika Jimbo La Arumeru Mashariki(CHADEMA)Joshua Nassari,jana katika Viwanja vya Patandi(Tengeru)
ameendeleea kuchangiwa shillingi hamsini na mia mia katika Mkutano wa Hadhara ambapo alikusanya zaidi ya Shillingi Laki5ni kama kurudishiwa Gharama Za mafuta na chakula ili aendelee na kampeni zake.

Mkutano uliohudhuriwa zaidi na akina mama wa Soko La Tengeru.

Wakati huohuo Polisi walipata wakati Mgumu sana kuelekeza Misafara ya CCM na Chadema pale ambapo Msafara wa CHADEMA ulipokuwa ukiondoka Tengeru kuelekea USA River ilipo kambi ya CHADEMA na ule wa CCM uliokuwa na Mabasi yakirudisha watu ARUSHA mjini walipokutana uso kwa Uso..

Leo CHADEMA wana mikutano32 ambayo itahutubiwa na wabunge wake mbali mbali huku Mgombea akihutubia Mikutano mitatu hadi Mitano kwa Siku
 
Mgombea wa kiti Cha ubunge katika Jimbo La Arumeru Mashariki(CHADEMA)Joshua Nassari,jana katika Viwanja vya Patandi(Tengeru)ameendeleea kuchangiwa shillingi hamsini na mia mia katika Mkutano wa Hadhara ambapo alikusanya zaidi ya Shillingi Laki5ni kama kurudishiwa Gharama Za mafuta na chakula ili aendelee na kampeni zake,Mkutano uliohudhuriwa zaidi na akina mama wa Soko La Tengeru.
Wakati huohuo Polisi walipata wakati Mgumu sana kuelekeza Misafara ya CCM na Chadema pale ambapo Msafara wa CHADEMA ulipokuwa ukiondoka Tengeru kuelekea USA River ilipo kambi ya CHADEMA na ule wa CCM uliokuwa na Mabasi yakirudisha watu ARUSHA mjini walipokutana uso kwa Uso..
Leo CHADEMA wana mikutano32 ambayo itahutubiwa na wabunge wake mbali mbali huku Mgombea akihutubia Mikutano mitatu hadi Mitano kwa Siku
Pesa za ruzuku wale MBOWE na SLAA halafu wakati wa uchaguzi utembeze bakuli! hii imekaaje siyo kuwaibia wananchi?
 
Hata tanu ya nyerere ilichangiwa hivi! Saa ya ukombozi imefika! Peeeooopleeee!
Tunakihujumu Chama. Tupunguze mshahara wa SLAA toka mil. 12 hadi saba kwa mwezi ili chama kisiwaongezee mzigo wa wananchi kwa kutembeza bakuli kikiomba pesa za kampeni
 
Nitaendelea kuripoti kila kinachojiri katika kampeni

Mkuu tujulishe na kiasi cha fedha za bakuli zilizopatikana ni ngapi ili tujue siku ya kugawana MBOWE, SLAA na NASSARI kila mmoja atapata shilingi ngapi ili wasije wakaambiwa na tume ya maadili kuwa wameiba au vipi?
 
si angenitafuta mimi nimpe hizo laki tano kuliko kusumbua watu.
 
Pesa za ruzuku wale MBOWE na SLAA halafu wakati wa uchaguzi utembeze bakuli! hii imekaaje siyo kuwaibia wananchi?
Nani mwizi kati ya yule anayechangisha kipindi cha kampeni na kuzikataa ruzuku au wanaopora aridhi za wananchi huko arumeru na gairo na kibaigwa.
 
Pesa za ruzuku wale MBOWE na SLAA halafu wakati wa uchaguzi utembeze bakuli! hii imekaaje siyo kuwaibia wananchi?

hakuna aliezaliwa akatembea mojaj kwa moja,kuna stage za kupitia mpaka afike hapo..so usihofu kwani muda ukifika utaelewa kinachoendelea...
 
si angenitafuta mimi nimpe hizo laki tano kuliko kusumbua watu.
Mkuu hapa hautafutwi ubunge unatafutwa mtaji. Hivi wewe ukichangiwa shilingi milioni 100 bado unahitaji kwenda mjengoni kufanya nini?
 
That's good of him.....CHADEMA imejengwa katika misingi hiyo siyo watu wachache wanamiliki uchumi...wanawatia watu umasikini ili wawatawale,,,,CCM wanafanya hivyo....wanajua wananchi wakielewa watawachukia.....Pambana Nassari
 
Nani mwizi kati ya yule anayechangisha kipindi cha kampeni na kuzikataa ruzuku au wanaopora aridhi za wananchi huko arumeru na gairo na kibaigwa.
Huyu anayekwenda kuwapaka wananchi mafuta kwa mgongo wa chupa ni hatari zaidi. Wao wanajua ardhi inaporwa wakati wa kkampeni tu? si wana viongozi huku majimboni kwa nini wasiripoti? au CHADEMA si chama bali ni Wanaharakati mbona hamueleweki? Hivi unajua ruzuku wanazozikataa zinatoka wapi? si kwa wananchi hao unaowatembezea bakuli na kuwanyang'anya kile walichobakiza baada ya kukupa zako huku kwenye ruzuku?NGOJA nikuache manake kama hujelewa kuwa wewe ni white paper basi.
 
Achani mtazamo hasi hii inaonyesha wazi watu wanavyo ikubali CHADEMA kuwa wapo tayari kukisapoti kwa hali na mali ili kisonge mbele kueneza huduma hii ya ukombozi wa fikira kwa watu wengine

Chadema wasilale bali wafanye kazi hizi pesa zitadaiwa kama hawazunguki nchi nzima
 
That's good of him.....CHADEMA imejengwa katika misingi hiyo siyo watu wachache wanamiliki uchumi...wanawatia watu umasikini ili wawatawale,,,,CCM wanafanya hivyo....wanajua wananchi wakielewa watawachukia.....Pambana Nassari
Na ole wake akose ubunge halafu tukamuona anatakata kwa pesa zetu za bakuli tutamfuata huko huko FOUNDATION FOR TOMMORROW manake tunajua huko ili ale mpaka awapigie magoti wazungu.
 
Huyu anayekwenda kuwapaka wananchi mafuta kwa mgongo wa chupa ni hatari zaidi. Wao wanajua ardhi inaporwa wakati wa kkampeni tu? si wana viongozi huku majimboni kwa nini wasiripoti? au CHADEMA si chama bali ni Wanaharakati mbona hamueleweki? Hivi unajua ruzuku wanazozikataa zinatoka wapi? si kwa wananchi hao unaowatembezea bakuli na kuwanyang'anya kile walichobakiza baada ya kukupa zako huku kwenye ruzuku?NGOJA nikuache manake kama hujelewa kuwa wewe ni white paper basi.
hapo red: pambanua una maana gani ?
 
Its no wonder cdm inaongozwa na Peoples Power, hivo raia wana kila sababu ya kukichangia, pasipo shuruti!
Mleta mada kama una namba za michango ya mtandao waweza ziweka hapa ili watu waendelee kuchangia!
Embu ccm jaribuni kuchangisha mtu muone kitakachowapata!...naamini watakaochanga ni watu kama Komba, Chiligati, Makamba, Mramba, Manji, Mwigulu, Kinana na watu wa jinsi hiyo walioneemeka sana na uwepo wa ccm!
 
Back
Top Bottom