Nassari alikana Mwananchi kuhusu Zitto na Urais

Nikiwa kama mwandishi wa habari, nimewahi kuandika humu ndani tabia chafu za mbunge Zitto Kabwe. Zitto anajiandikia habari, analazimisha ichapishwe bila kufanyiwa uhariri.

Katika watu watakaoliingiza hili taifa katika hatari, ZITTO ni mmoja wao. Anafika kuwahonga waandishi ili waandike habari zake na ziwekwe ukurasa wa mbele. Uongozi haulazimishwi, uongozi ni kazo watu wanapewa na wapiga kura. Jipangeni kuhusu Zitto.

Kazi nzuri Nassari, CCM- Inamsadia zitto kwenye hizi propaganda za kuvuruga CHADEMA
Kama hiyo ndiyo tabia ya zitto basi nchi hii bado tuna safari ndefu sana ya kupata wazalendo wa kweli wenye lengo genuine la kuikomboka kutoka kwenye makucha ya ccm. Najiuliza sasa tumwamini nani!! Kila kiongozi awe mzee au kijana anasukumwa na maslahi binafsi. Kazi kwelikweli.
 
Lile dokezo alilotoa Wasira juu ya Chadema kusambaratika kabla ya 2015 ndiyo kazi imeshaanza ila wameanza kwa mguu mbaya.Ninachoamini ni kuwa CCM (Mafisadi) wana fedha na dola nyuma yao lakini Chadema wana Mungu kwani sauti ya wengi ni sauti ya Mungu.
 
Ikitokea hii ikawa ni njama ya CCM kuivuruga CHADEMA kupitia Zitto ntaamini magamba noma aiseee
Zito Kabwe ni CCM PIWA na hata damu yake ni ya kijani kama ilivyo ya Mrema , Cheo na yule kibaraka mbunge anayeisumbua sana CDM.
 
Hili gazeti linatia Shaka!Waliandika habari ya Membe mwaka jana kwa mbwembwe,naona wamelazimishwa kumeza matapishi yao!
 
Zito kabwe ni rafiki mkubwa wa jack zoka endelea mwenyewe kuunganisha dots hapo.
 
Majigambo, ulafi wa madaraka na ubinafsi ndio unao tawala akili za baadhi ya viongozi na wawakilishi wawananchi katika sehemu mbalimbali hususani katika siasa.

Inasikitisha sana kuona vijana wenzetu wakionyesha tamaa na uchu wa kukimbilia ikulu.Jamani ikulu kuna nini?Mzee wetu,mwl.J.K.Nyerere alisema"Ikulu nipakuogopa kama ukoma"Why kila kukicha huwa vijana Nassar
i,Zito na mzee wao Siraha wanawaza kwenda ikulu na wengine wanadiriki kutaka kujitangazia Jamhuri yao?Hili Taifa tunalipeleka wapi?
 
Sielewi ni kwanini ZITTO anaitamani IKULU hivyo. Je kuna nini IKULU? Mbana nionavyo mimi ZITTO hana uwezo wa kuwa RAISI? Ni afadhari M.MEMBE kuwa Raisi, kwani anafaa!
 
Mtu yeyote anayekimbilia Ikulu tena anashawishishawishi watu kumpigia debe na kununua vijigazeti vimtangaze ni wa kuogopa kama UKOMA
 
Godbless Lema alishamwona zitto mapema..NI KAMA PAKA NA PANYA HAWA WATU WAWILI..HAWAELEWANI KABISA..tafakari
 
Mimi binafsi ni shabiki wa ZITTO kwa vitendo 100% hata mkimchukia kwa Kabila lake au Dini na hukatazwi kumshabikia yoyote kwenye nchi hii bila kujali chama

hapo umeharibu. Mimi natokea anakotoka Zitto. ingwa tumetengwa kwa wilya zetu, lakini KIGOMA ni moja. Zitto kabwe alianza kuwa maarufu, pale alipofukuzwa bungeni, nadhani ilikuwa 2008 kama sijakosea. nilikuwa mwaka wa pili UDSM. Ambaye hakumuunga mkono kipindi kile alitakiwa apimwe.

Mara baada ya kupata umaarufu, Zitto akaona yeye ndo Chadema (lina ukweli kidogo kwa kipindi kile) na Chadema ndo yeye. Akaanza maringo, shughuli za kujenga chama akaanza kuhudhuria kwa nadra sana, na matamko ya utata akaanza kuyatoa.

Kwa mfano, wakati CHADEMA wana harakati za kujenga chama kuanzia vijijini, yeye akaanza kutangaza nia ya kugombea URAIS, japokuwa hajataja chama kama kumbu zangu hazijalala. Sasa mtu anaye toa matamko kama hayo, huyo si wa kutusaidia, bali atatuangusha.

Kazi ya URAIS, nadhani CDM wanapaswa kuungwa mkono, pale walipomtaka na kumuuomba Slaa awabebee bendera badala ya yeye kuomba kubeba bendera. Mtu aombaye kubeba bendera, ni mbaya kuliko yule anayeombwa kubeba bendera kwa niaba ya chama. kuanzia hapo Iman yangu kwa Zitto imekuwa ikishuka siku hadi siku
 
Kama mtakumbuka vizuri, kwenye kampeni zake za ubunge 2010 huko Kigoma, Zitto aliwaambia wapiga kura wake kwamba 2015 haji kuomba kura za ubunge tena bali za urais.

Nashangaa mnavyoona hizo harakati mnashtuka...alidhamiria tangu mwanzo yeye atakuwa mgombea wa urais kupitia CDM. ila sijui asipoteliwa ndio atafanyaje awe mgombea kama alivyooahidi wapiga kuera wake.

Dogo yuko over ambitious, mtu wa namna hii ni hatari..soma historia ya Hittler, mtu anatamanim madaraka kwa njia yeyote ile na akiyapata hatataka kidudu mtu kimpinge kwa vyovyote vile.
 
sisi welevu tunajua ni mbinu za ccm km ilivyo km kawaida yao kupandikiza mamluki km akina zitto kwani sasa imeelemewa.....zitto ni kijana mnafiki sana....alipowageuka watz kuhusu mitambo ya dowans ndipo nilipoona nguvu ya rostam na mafisadi wengine
 
Mtu yeyote anayekimbilia Ikulu tena anashawishishawishi watu kumpigia debe na kununua vijigazeti vimtangaze ni wa kuogopa kama UKOMA

Wengi wamesema Zitto ni rafiki wa JK na anachofanya kuhusu kampeni zake za ikulu ni same na alivyopitia JKkwa kutmia magazeti na kutangaza mapema.JK miaka yote 10 akiwa foreign aliitumikia kwa kuusaka urais na hatimaye alifanikiwa lakini nkwa kuwajeruhi kina SAalim, sumaye na wengine.MBINU ANAYOTUMIA ZITTO NI ileile ya best wake JK asipodhibitiwa huko CHADEMA wahanga watakuja kuwa wengi.
Lakini alichokosea ni aina ya gari analotumia kuelekea ikulu, ni gari isyo 4WD kiasi kwamba atakapokita katika tope hataweza kutoka, kwani njia aliyopita ina madimbwi hatafika salama tope la barabara ile ni la mnato.Subirini mtamuona muda si mrefu
 
LEKA DUTIGITE mpaka ikulu.
Natoa hypothesis kuhusu huyu jamaa wa dutigite.
1.Ana nia ya dhati ya kuliongoza taifa hili
2.Anatumiwa na ccm kuvuruga cdm
3.Anataka umaarufu
Kama 2 sio sahihi anaweza kuuawa na ccm kwa sababu watasingiziwa cdm kuwa ndo wamehuska.Angalie sana
 
Zitto asifikirie kulazimisha umaarufu kutamsaidia. CCM inamtumia tu kukivuruga Chadema kabla ya 2015 wala zitto asiwe na ndoto za kuukwaa urais.

Kuna watu mahiri sana ndani na nje ya Chadema. Kuna vijana mahiri vibaya sana ambao wapo nje ya nchi na punde tu watarudi kujiunga na Chadema. Zitto analifahamu hilo ndio maana anaendelea kuropoka na kutumikia CCM. Najua vijana wawili ambao ni presidential materials ambao wapo USA na mmoja yuko UK.

Out of inquisitiveness...........

1. So ndo maana humtaki Zitto?????
2. Hata kama ni credible kumbe tayari una/ mna machaguo yako/ yenu????
3. Kama hata JK anawajua so ni halali kumkataza ZZK kama kweli anautaka na anafaa????
4. US na UK ndo chuo cha urais wa Tanzania???? Eurocentric mindset.....................?????
5. Kwa nini asiwe hata na ndoto ilhali ni Mtanzania na anavigezo may be...mi mwenyewe nina ndoto huku uwezo tu sina...?????
6. Unasema kuna watu mahiri nje na ndani ya chadema........can you give a comparative framework atleast with five indicators other than the constitutional givens????


I real wonder the way type of yours think that you can have the power of all the Tanzanians to say and judge for the presidential candidate....either ways if this is a mission cant it be covert one?????.............so many blah blahs make even the plan prone to abortion...........this is when my mind rejects the idea of multipartism......in unmatured countries with politicians with the shape and colour like some othe the ones you own today.....like "tukupe uwaziri wa fedha" very low thinking and planning version......you guys are soon gonna lead that block into blood sheds unnecessarily.......soo greedy and shameless to an extent of having a cabinet prior to the process that is supposed to bring effects...!!!!!!!

Where are the concerned authorities????? Why do you let such minds shake the Nation and its tranquility for no good reason..........????
 
Back
Top Bottom