Nassari akisindikizwa na Kangi Lugola kutoa Shukrani Kanisani!!

Nassari yupo Kanisani...safi sana..sasa waislam waliokuchagua shukrani zao utazitolea wapi?

acha upofu wa udini kanisa ni sehemu ya kusali na kukutana na waumini wenzie ila kwa suala la wapiga kura amekuwa akiitisha mikutano mbalimbali kushukuru wapiga kura na kueleza mikakati ya maendeleo ya jimbo letu! au unataka aanze tena kuzunguka misikitini, kanisa katoliki, anagelikana, baptist, shia, sunni, mjahidina , jehova,budhist n.k kutoa shukrani? Na ufahamu hapo alipokuwa ni kanisa la lutheran ambapo yeye ni muumini hapo kuna makanisa mengi sana ya kikikristu arumeru hakwenda,na mbona umekimbilia kuulizia waislamu kwa nini hujaulizia wapagani wasiomuamini mungu ambao wapo huku, au wanaoamini dini ya kienyeji ambao hutambikia chini ya miti? milimani? kwenye mapango? mito mikubwa au misituni? unataka na kote huko aende akatoe shukrani? huo upofu utakutoka lini???
 
Nasari alikwenda kanisani kumshukuru Mungu siyo kuwashukuru wakristo! Nchi yetu haina dini, ila wananchi wake, Nassari akiwepo, wana dini zao. Wewe ritz una tatizo la udini, usijaribu kutugawa. Waislamu hao waliompigia Nassari, walikua wanapiga kura wakijua ni muumini wa imani ya Kikristo. Au unataka kusema tumefika mahali pa kuchaguana kwa itikadi zetu za dini?
 
Mkuu ritz,
Mungu ni mmoja! Hata angeenda kutoa hiyo shukrani kwenye sinagogi la aina gani bado alikuwa anamshukuru Mungu yule yule ambae ni wa wote! Kwa hiyo hapo amewakilisha watu wote wanaoamini uwepo na uwezo wa Mungu.
 
Last edited by a moderator:
kumshukuru mungu ni imani na siyo majivuno; sadaka yaweza kuwa 500/ na ukabarikiwa. Je kama alitoa 500 angegawanya? Tuwe tu wastaarabu katika mambo ya imani. Angekuwa mwabudu mizimu akatoa sadaka katika pango/chini ya mti au makaburini kwa imani yake mngedai na mgao
 
Aende na Msikitini as watu wa waliompigia walitoka dini zote

wengine atakutana nao majukwaani kwani kanisani hajaenda kumshukuru mtu bali Mungu wake sasa msikitini kuna Mungu wake? Siku anataka kuwashukuru watu atakutana nao majukwaani wakiwemo waislam.
 
Ritz ckushangai kwani wa2 wa ccm mnazalisha udini baada ya kushindwa siasa.MBONA JK HUWA ANAHUTUBIA TAIFA KUPITIA WAZEE WA KIISLAMU WA DAR? kama kuna wakristo mbona wote mmo huwa wanavaa barakhashia?
 
nassari yupo kanisani...safi sana..sasa waislam waliokuchagua shukrani zao utazitolea wapi?

awa kweli kazi ya magamba kwishaaaa yaani kwa uelewa wako alienda kushukuru wakristo au mungu

je waislamu pia c walialikwa na walikuwepo wengi mno kumsindikiza nassari
 
Sijawahi kumuona Kanisani hapa kwetu Kibara. Ni zaidi ya ukristu wake. Sasa hivi kila magamba anajitahidi aonekane anawajali wananchi na njia pekee ni kujifanya wako sambamba na wapiganaji. Umesikia maajabu ya Lowasa kuomba kuhamia CDM?

umesema vema, hujawahi kumuona, lakini huenda akawa mkristu na anaabudu katika kanisa jingine na siku hiyo kaja katika kanisa la Kibara.
 
Nasari alikwenda kanisani kumshukuru Mungu siyo kuwashukuru wakristo! Nchi yetu haina dini, ila wananchi wake, Nassari akiwepo, wana dini zao. Wewe ritz una tatizo la udini, usijaribu kutugawa. Waislamu hao waliompigia Nassari, walikua wanapiga kura wakijua ni muumini wa imani ya Kikristo. Au unataka kusema tumefika mahali pa kuchaguana kwa itikadi zetu za dini?

Mkuu ebu angalia vizuri Heading ya hii thread inasemaje ngoja nikukumbushe..

"Nassari akisindikizwa na Kangi Lugola kutoa shukrani Kanisani"

Sasa sijui hayo maneno yako umeyatoa wapi.
 
Hapo ni kanisani unless ukituthibishia kuwa Kange Lugora ni mwislamu na sio mkristu ndipo tutaanza kuhoji. kama ni mkristu mwenzake hakuna sababu ya kuhoji uwepo wake kanisani hapo na hata kumsindikiza mbunge mwenzie kumshukuru Mungu

Nani alikuambia mwislamu kuingia kanisani ni kosa? ile ni nyumba ya mungu kama ulivyo msikiti mtu yeyote anaingia ila tatizo woga wa muhusika kuhofia kukiuka taratibu za msikiti au kanisa halafu katika kujichanganya wakati mwingine husaidia kupata taarifa za upande wa pili kwa hiyo tusihofu waungwana pia kuna mahusiano binafsi tofauti na itikadi.
 
acha upofu wa udini kanisa ni sehemu ya kusali na kukutana na waumini wenzie ila kwa suala la wapiga kura amekuwa akiitisha mikutano mbalimbali kushukuru wapiga kura na kueleza mikakati ya maendeleo ya jimbo letu! au unataka aanze tena kuzunguka misikitini, kanisa katoliki, anagelikana, baptist, shia, sunni, mjahidina , jehova,budhist n.k kutoa shukrani? Na ufahamu hapo alipokuwa ni kanisa la lutheran ambapo yeye ni muumini hapo kuna makanisa mengi sana ya kikikristu arumeru hakwenda,na mbona umekimbilia kuulizia waislamu kwa nini hujaulizia wapagani wasiomuamini mungu ambao wapo huku, au wanaoamini dini ya kienyeji ambao hutambikia chini ya miti? milimani? kwenye mapango? mito mikubwa au misituni? unataka na kote huko aende akatoe shukrani? huo upofu utakutoka lini???

"Nassari akisindikizwa na Kangi Lugola kutoa Shukrani Kanisani"

Hiyo ndio Heading ya hii thread.
 
Mkuu ebu angalia vizuri Heading ya hii thread inasemaje ngoja nikukumbushe..

"Nassari akisindikizwa na Kangi Lugola kutoa shukrani Kanisani"

Sasa sijui hayo maneno yako umeyatoa wapi.

Nassari yupo Kanisani...safi sana..sasa waislam waliokuchagua shukrani zao utazitolea wapi?

ritz,
Kumbuka Faiza Foxy alifungiwa kutokana na tabia yake ya kuendekeza udini humu jamvini. Sasa wewe endelea uone kama hujashughulikwa. Bahati nzuri Invisible, Buchanan na Fang wanakufuatilia.
 
Mkuu ebu angalia vizuri Heading ya hii thread inasemaje ngoja nikukumbushe..

"Nassari akisindikizwa na Kangi Lugola kutoa shukrani Kanisani"

Sasa sijui hayo maneno yako umeyatoa wapi.

Ritz una kichwa nzito sana. Kwani kama yeye ni mkristo ulitaka akatolee wapi shukrani yake? Unajuaje kama pia atatembelea msikitini kutoa shukrani?
 
Ritz ckushangai kwani wa2 wa ccm mnazalisha udini baada ya kushindwa siasa.MBONA JK HUWA ANAHUTUBIA TAIFA KUPITIA WAZEE WA KIISLAMU WA DAR? kama kuna wakristo mbona wote mmo huwa wanavaa barakhashia?

Mkuu kofia sio uislam hata Mrema anavaa barakhashia...mie nimeuliza baada ya kuona Nassari akisindikizwa na Kangi Lugola kutoa Shukrani Kanisani.
 
Back
Top Bottom