Nassari afyatuka: Kama maji hatuna flyover za nini?

ki ukweli maji ni muhim sana pengne kuliko hayo ma flyovers nyiee mnayajua.katika uchakarikaji wa kibiashara wanawake wako weng mno,sasa unakuta anapoteza more tha six hours anahaingakia maji..mpaka aje aende kwenye biashara zake ameshapoteza masaa 7,anauza uza kidogo watu wa ushuru wa soko hawa hapa wanataka chao,inakuwa unyanyasaji kwa mama huyu.hata mim naunga mkono hoja ya mh.nassari
 
mkuu watanzania walio wengi wanaishi vijijini..wanatumia mudamwingi kwenda kutafuta maji na hii ni kwarika zote vijana,wamama,watoto,na wazee..hawa walitakiwa muda mwingi watumie katika shughuli za kilimo,na watoto wanatakiwa kuwa shule badala ya kuwaste the whole day kutafuta maji..by the way maji ni afya pia..you should think twice mkuu..

Kweli Mkuu, kijana amesema kitu ambacho jamii inatakiwa ili kufikia maendeleo endelevu, sioni mantiki ya kujenga flyovers ambazo gharama zake ni sawa gharama inayohitajika ili mji wa Magu, Bunda, Kisesa, Nyangunge, na Kwimba uwe na sustainable water supply.

ni aibu sana kwa wakazi wa kanda ya ziwa hususani Magu ambapo ziwa victoria liko chini ya kilometre 7 kutokuwa na maji ya uhakika, leo katika mji wa Magu na Bunda ndoo ya maji inafikia sh. 500, then we talking about flyovers, kama tunahitaji maendeleo ni vyema tukawekeza kwenye maji ili ifikie mahala mwananchi atumie muda wake mwingi katika shughuli za uzalishaji mali badala ya kutafuta maji.

Hili suala wala halina itikadi, ni vyema tukaangalia namna wananchi wetu hususani walioko vijijini wanavyopata taabu na suala hili la maji na mwisho wa siku tunawtumia kama rubber stamp pindi tunapohitaji kurudi katika nyadhifa zetu, Magu Bunda, Kwimba (Ngudu) lazima zikombolewe bila kujali aidha kwa watu wengine kuchukua majimbo hayo ili kuleta hamasa na msukumo mpya katika kushughulikia matatizo ya wananchi. Narudia tena kwamba hili suala halihusiani na itikadi za kisiasa.
 
wakuu nimemsikiliza nasari muda mfupi uliopita alichosema kweli kina manufaa tunataka fly overs barabara nne nne na madaraja ya kifahali wakati huduma ya msingi hasa na maji kwa wananchi hawana tujadili

OH! God!!!! Nasari kakurupuka tena -

Barabara sio huduma ya msingi ...?! yaani yeye anataka tubaki kwenye barabara za one way na za mashimo ... mi namshauri huyu dogo akae kimya hadi pale atakapo pata akili kwamba sasa hivi anachoongea anasikilizwa na mamilioni ya wananchi...
 
Tutapata maji tutakapowaodoa Magamba katika uongozi wa tanganyika.Kwa sasa tunapigania uhuru wetu toka kwa hawa magamba na tunamuomba sana Mungu atuwezeshe katika mapambano haya
 
tanira1 Sio barabara za kifahari, dhumuni ni kupunguza msongamano ili tuwahi kazini tuweze kushughulikia maji, imagine mtu una drive 21 km for three hours (tegeta to masaki) kila siku X2 means 6 hours back and forth... think.

hakuna suala la kujadili hapa,

Unafuata nini tegeta kote huko kama unafanya kazi masaki. Poor Life Planning.
 
OH! God!!!! Nasari kakurupuka tena -

Barabara sio huduma ya msingi ...?! yaani yeye anataka tubaki kwenye barabara za one way na za mashimo ... mi namshauri huyu dogo akae kimya hadi pale atakapo pata akili kwamba sasa hivi anachoongea anasikilizwa na mamilioni ya wananchi...
Ni kweli kakurupuka sababu ukweli ni kwamba hizo barabara hazitajengwa na vijimaneno vya kupambia kauli mbiu tu.
 
CCM vipaumbele vyao ni aina ya Comedy isiyochekesha wala kuelimisha, CCM na SERIKALI yake inatupa UMASKINI WA KUTUPWA!
 
tanira1 Sio barabara za kifahari, dhumuni ni kupunguza msongamano ili tuwahi kazini tuweze kushughulikia maji, imagine mtu una drive 21 km for three hours (tegeta to masaki) kila siku X2 means 6 hours back and forth... think.

hakuna suala la kujadili hapa,
nyinyi siku hizi hamuaminiki mmeshindwa kutuletea maji kwa almasi na dhahabu mtatuletea kwa kuwahi kazini? kwanza uwajibikaji kwa watanzania wengi ni donda ndugu sema labda mnataka kuwahi dili uliloacha jana cha kujdili bado kipo
 
OH! God!!!! Nasari kakurupuka tena -

Barabara sio huduma ya msingi ...?! yaani yeye anataka tubaki kwenye barabara za one way na za mashimo ... mi namshauri huyu dogo akae kimya hadi pale atakapo pata akili kwamba sasa hivi anachoongea anasikilizwa na mamilioni ya wananchi...
brother njiwa kwanza nimegundua wewe ni mbinafsi kisha unakaa mjini kumbuka bibi yako kule sitimbi akikosa barabara bado ataishi akikosa maji safi na salama inakuaje bado mimi nabaki kwenye msimamo kwa tanzania maji muhimu kuliko flyover za dar kwanza dar nini wanazalishia nchi hii zaidi ya kufuja rasimali za nchi hii
 
Hii ina mantiki kubwa kabisa! Heko Nassari...hukutumia macho yako mawili, ila lile la tatu. Na ndivyo tunavyohitaji.
wakuu nimemsikiliza nasari muda mfupi uliopita alichosema kweli kina manufaa tunataka fly overs barabara nne nne na madaraja ya kifahali wakati huduma ya msingi hasa na maji kwa wananchi hawana tujadili

Watu wanawaza maslahi ya watu wachache, ili hali tuliowengi tunabaki makabwela. Wanawaza kuijenga kigamboni, wa Tandahimba hana hata maji, wamatombo mwanae aenda uchi shuleni, wakibondo ashindia uji kwa siku, jasho lao na rasilimali zao zinaelekezwa sehemu moja. Flyover za nini hali kuna sehemu hazifikiki? Shule-Hospitali hakuna...maji, barabara hakuna, umeme, nk. wengine wanawaziwa kujengewa barabara za juu na miji mnayoita ya kisasa, ni nini hii zaidi ya ulimbukeni na upunguani. Kwani kinachojenga Dar si ni rasilimali za watanzania! Kwanini wao wapate hisa kubwa hali UTANZANIA HAUNA MATAWI? Kwanini iwepo Moshi na Lindi, Dar na Kigoma, Mwanza na Singida, Osterbay na Tandale? Pumavu!
Mungu wetu anaita sasa!
 
OH! God!!!! Nasari kakurupuka tena -

Barabara sio huduma ya msingi ...?! yaani yeye anataka tubaki kwenye barabara za one way na za mashimo ... mi namshauri huyu dogo akae kimya hadi pale atakapo pata akili kwamba sasa hivi anachoongea anasikilizwa na mamilioni ya wananchi...

wewe gamba usiyekuwa na akili inamaana hujui kuwa huduma ya maji ni muhimu kwa jamii kuliko hata hiyo barabara?? Akili yenu nyie wa chama cha msitu wa mabwepande ni kama akili za inzi au konokono. Pia unaweza kuwa hujui kuwa maji yanatumika kunywa,kuonga,kufulia,kupikia pamoja na viwandani pia wanatumia maji. Acha ushabiki wa kimagamba usiokuwa na faida kwa wananchi.
 
huyu ni pung'o tu, hana lolote, unajua wakati mwingine wana chadema wanaongea ili wapate sifa tu. kwani yeye kama kule arumeru hahitaji fly over anafikiri hata sisi watu wa kimara na ubungo hatuhitaji hizo? hajui karaha gani tunaipata kutoka kimara hadi posta asubuhi, hajui utendaji wa kazi na mapato ya serikali yanavyopotea kutokana na watu kuchelewa kufanya kazi maofisini kwasababu ya foleni au kuchoka sana kwenye mafoleni kunakopunguza utendaji wa kazi wakifika ofisini. namshauri kwa hili anyamaze kabisa, alafu aache mapepe, ajifunze kwa wenzie kina zito wanaoongea kiutu uzima. TUNAITAJI FLY OVERS as many as we can, hii itatufanya utendaji kazi hapa dsm uende kwa kasi, mapato yataongezeka tutapata pesa za ziada hata kuleta hata hayo maji anayololoma nayo. YOU NEED TO UNDERSTAND THAT, sio CHADEMA wote wakiongea wanaongea point, wengine hapo ni pumba tupu...kwanza ni mgeni bungeni, aongee point au aombe msaada wazoefu pale kina zito, mbowe, dr. slaa hata kama hayuko bungeni atamsaidia kumwelekeza. asiongee pumba akatuaibisha chadema wote.
 
Back
Top Bottom