Makanyaga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2007
- 10,326
- 6,849
Panadol;...CHADEMA hakuna walichotekeleza kwa yale waliyohahidi majimboni mwao wakati wa kampeni mwaka 2010,kama kuna mtu anabisha ataje jina la mbunge wa chadema ,jimbo atakalo na kero alizohaidi kuzitatua na ambao tayari zimetatuliwa mpaka sasa, wananchi wanahoji sana huku mtaani ikibidi nawashauri wabunge wa chadema mfanye mikutano majimboni mwenu muwaambie wananchi ni ahadi ngapi mmeshazitekeleza kati ya zile mlizoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2010, watu wamechoka makelele yenu mnaropoka sana vitendo zero!
Umesahau kitu kimoja;
Wabunge wengi walio mahiri ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wanafanya kazi kama wabunge wa Taifa kwa ujumla na si kama wa majimbo yao ya uchaguzi kule ambako walipigiwa kura.
Tusipokuwa waangalifu tutakuja kupoteza wabunge wa maana sana kwenye chaguzi zionazofuata simply tuna-assess delivery yao kijimbo zaidi kuliko kitaifa. Naomba hili kosa tusije tukalifanya.
Na ukiangalia vizuri, baadhi ya wabunge ambao concentration yao kubwa sana ni kwenye majimbo yao ya uchaguzi tu, wengi wao hawana tija kitaifa na wako pale kwa ajili ya kujiimarisha majimboni ili wawe na uhakika wa kurudi kwenye chaguzi zinazofuata.
Hata, hivyo, kuna baadhi ambao wana uwezo mkubwa wa kumudu vyote viwili vizuri sana, yaani majimboni kwao na kitaifa kwa ujumla, nawapa hongera zao!