Nassari afyatuka: Kama maji hatuna flyover za nini?

Kweli hii serikali ni kama haina kipau mbele wao ni bora liende tu, kulikuwa na uharaka gani wa kutenga hela za kujenga flyover, huku watu wengi hawana huduma bora za afya na kupata maji safi ni anasa. Kwa nini wasingeanza kuboresha afya na maji, ndo zije hizo flyover. Ingawa nazo zina umuhimu wake lakini wasingezipa uzito kiasi hiki kipindi hiki ambapo huduma za afya zimedorola zaidi na huduma ya maji safi sehemu nyingi nchini bado ni ndoto. Hivi hakuna washauri huko serikalini au nini?
 
kwa kumalizia; maji ni uhai flyover sio hitaji la msingi kwa sasa kwani serkal ikihamia Dodoma nazan itasaidia zadi ya flyover
 
ana point ila asisahau kwamba kila jambo na priorities zake

costing na economic efficiencies ni muhimu.... maji yana sera zake, barabara zina sera na nafasi zake

barabara hurahisisha maendeleo, na kwenye barabara huduma za jamii hufika mapema bila kusahau nafasi za kuuza mazao na rasilimali nyingine kirahisi hivyo kuweza kupa pesa za kuweka maji, umeme, zahanati, shule nk.

its an egg and chicken.... ila mafly over ni chanzo cha poor planning, tusingeyahitaji kama miji tungeiweka kama ardhi yetu ilivyo
 
tembea uone ndugu yangu. Umesema ya TRA nikakumbuka. Pale TRA ya ARUSHA kuna mabinti wawili mapacha wa kichaga waliajiriwa mwaka jana. Walinifanya niwaze sana kwa kweli. Nji hii haiko salama tena.

hii nchi inaelekea kubaya,sasa ukabila ni waziwazi kabisa,acha tuuane heshima irudi kama rwanda
 
Huyo Nassari hajuwi uchumi ni nini.

Ikiwa Dar ina wakazi million 5 na kati yao million 1 wanapoteza masaa 4 kila siku barabarani ina maana kwa siku wanapoteza miaka zaidi ya 365 na ukiwapunguzia nusu ya huo muda wanaopoteza njiani ina maana una faida ya miaka 182. Na kila unapowacha hilo tatizo huo muda haupunguwi unazidi.
 
Huyu jamaa wakati akigombea ubunge kwenye kampeni zake alihaidi kutatua kero mbalimbali za wananchi kama wakimchagua yeye kero zao zitatatuliwa sasa atatue asilalamike kama ameshindwa ajiuzulu ubunge,CCM mwaka 2010 ilikuwa na ilani yake ya uchaguzi iliinadi nchi nzima na wananchi wakaikubali ndiyo maana waliichagua sasa hasiipangie CCM cha kufanya haiache itekeleze ahadi zilizomo kwenye ilani yake ikiwemo ahadi ya ujenzi wa Flyovers,kama kero za Arumeru mashariki zimemshinda kutatua kama alivyohaidi aachie ngazi wapo wanaoweza kutatua kero hizo watachukua nafasi yake,siyo yeye tu wabunge wote wa chadema hakuna walichotekeleza kwa yale waliyohahidi majimboni mwao wakati wa kampeni mwaka 2010,kama kuna mtu anabisha ataje jina la mbunge wa chadema ,jimbo atakalo na kero alizohaidi kuzitatua na ambao tayari zimetatuliwa mpaka sasa, wananchi wanahoji sana huku mtaani ikibidi nawashauri wabunge wa chadema mfanye mikutano majimboni mwenu muwaambie wananchi ni ahadi ngapi mmeshazitekeleza kati ya zile mlizoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2010, watu wamechoka makelele yenu mnaropoka sana vitendo zero!
 
Tatizo la maji litatatuliwa na CDM kupitia Saboda si anachimba visima kila jimbo la CDM.Barabara watagenga CCM
 
wakuu nimemsikiliza nasari muda mfupi uliopita alichosema kweli kina manufaa tunataka fly overs barabara nne nne na madaraja ya kifahali wakati huduma ya msingi hasa na maji kwa wananchi hawana tujadili

Kupanga ni kuchagua, wakati unapitishwa ule mpango wa miaka mi5 yeye hakuwa amechaguliwa ubunge, kwa hiyo anatakiwa awalaumu na wabunge wa chama chake waliopitisha huo mpango.
 
Huyo Nassari hajuwi uchumi ni nini.

Ikiwa Dar ina wakazi million 5 na kati yao million 1 wanapoteza masaa 4 kila siku barabarani ina maana kwa siku wanapoteza miaka zaidi ya 365 na ukiwapunguzia nusu ya huo muda wanaopoteza njiani ina maana una faida ya miaka 182. Na kila unapowacha hilo tatizo huo muda haupunguwi unazidi.

Ndio uwezo wake wa kufikiri umeishia hapo..Af Sabodo alidai atawachimba visima kwenye majimbo yao, nadhani pesa watakuwa wamempa padri atumie na mama Junior, manake khali yake sio nzuri toka alivyoshindwa Urais
 
tanira1 Sio barabara za kifahari, dhumuni ni kupunguza msongamano ili tuwahi kazini tuweze kushughulikia maji, imagine mtu una drive 21 km for three hours (tegeta to masaki) kila siku X2 means 6 hours back and forth... think.

hakuna suala la kujadili hapa,

Mkuu, kama ukiamka asubuhi unafungua bomba la maji na kuoga huwezi jua machungu ya kukosa maji. Lakini kwa mtazamo wangu, kuna hoja ya msingi. Inawezekana nyie wa mijini kwa sasa maji siyo priority, kwani mko kwenye level tofauti kabisa ambapo kupunguza msongamano barabarani ndio priority yenu.

Rudi kwenye maisha ya Mtanzania wa kijijini anayefuata maji umbali siyo chini ya kilometa 5!
 
Hii ndi faida ya kuchagua vijana wa mission town. Huyu bora amtafute sugu wafanye show nyingine.
 
wakuu nimemsikiliza nasari muda mfupi uliopita alichosema kweli kina manufaa tunataka fly overs barabara nne nne na madaraja ya kifahali wakati huduma ya msingi hasa na maji kwa wananchi hawana tujadili

Huyu dogo aache uchemshaji, hoja za namna hii hazitupeleki popote. Kwa maana hiyo anataka tukose maji tukose na fly overs pia? Kipi bora kukosa vyote au kimoja? Bora angesema anashauri priority iwe kwenye maji kwanza kabla ya flyovers, hapo ningeelewa. Lakini unaposema kuwa "kama maji hatuna flyovers za nini" unaonyesha kutoa a self destructing statement. Magufuli tayari anazo hela za kujenga flyovers, je kutokana na mawazo ya Nassari, tumshauri Magufuli azifuje ili tusijenge flyovers sababu maji hatuna? Ajaribu kwenda kumwambia Mh. Waziri labda atamsikiliza hoja yake, ila aangalie wasije wakapigana ngumi hata kabla hajamaliza kuongea. Maana ukishagusia kwenye flyovers na barabara, ni kama umegusa mboni ya jicho lake, inabidi uende taratibu. Juzi nimemsikia kwenye taarifa ya BAHARI akisema kuwa kwa kilometre za barabara anazojenga ukizichukua uzihamishie Rwanda, NCHI YOTE YA RWANDA ITAGEUKA KUWA LAMI HADI WATAKOSA MAHALI PA KULIMA. Yaani nilicheka mpaka nikataka kuzimia, sijui huyu Mh huwa anafikiriaje. Anaweza akaongea kitu ambacho wengi hamuwezi kuwa mmekiangalia katika alternative ambayo yeye anakiwazia halafu kinachekesha sana, huwa ananifurahisha sana......., mfano mwingine alisema "tuweke sheria tukubaliane sasa barabara zetu zitakuwa na upana wa kupita bajaj tu"......, "hata kama tusipobomoa jengo la TANESCO sasa hivi sababu liko ndani ya hifadhi ya bararabara, lazima ipo siku litakuja libomolewe tu unless tuibadilishe hiyo sheria, .... anaifurahishaga sana maneno yake na vitendo/kazi zake,... I LIKE HIM!
 
Huyu jamaa wakati akigombea ubunge kwenye kampeni zake alihaidi kutatua kero mbalimbali za wananchi kama wakimchagua yeye kero zao zitatatuliwa sasa atatue asilalamike kama ameshindwa ajiuzulu ubunge,CCM mwaka 2010 ilikuwa na ilani yake ya uchaguzi iliinadi nchi nzima na wananchi wakaikubali ndiyo maana waliichagua sasa hasiipangie CCM cha kufanya haiache itekeleze ahadi zilizomo kwenye ilani yake ikiwemo ahadi ya ujenzi wa Flyovers,kama kero za Arumeru mashariki zimemshinda kutatua kama alivyohaidi aachie ngazi wapo wanaoweza kutatua kero hizo watachukua nafasi yake,siyo yeye tu wabunge wote wa chadema hakuna walichotekeleza kwa yale waliyohahidi majimboni mwao wakati wa kampeni mwaka 2010,kama kuna mtu anabisha ataje jina la mbunge wa chadema ,jimbo atakalo na kero alizohaidi kuzitatua na ambao tayari zimetatuliwa mpaka sasa, wananchi wanahoji sana huku mtaani ikibidi nawashauri wabunge wa chadema mfanye mikutano majimboni mwenu muwaambie wananchi ni ahadi ngapi mmeshazitekeleza kati ya zile mlizoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2010, watu wamechoka makelele yenu mnaropoka sana vitendo zero!

Huyu dogo mimi naona kama ni mchemshaji tu, CHADEMA wasije rogwa wakampitisha ugombea tena nafasi hiyo kipindi kijacho, kuna uwezekano mkubwa wakapoteza jimbo. Yeye anadhani kuogea kwa sauti ya juu kama Freeman Mbowe, pindi anapokuwa jukwaani ndiyo u-CHADEMA huo. Apige majukumu ki-Taifa kama wenzake akina Zitto, Mnyika, Mdee, nk na ndiyo tutaelewa. Hawa vijana niliowataja wanafanya kazi zao kama si wabunge wa majimbo yao tu, bali kama wabunge wa Taifa la Tanzania.Nassari naye aige mtindo huo, watu watampenda. Maneno maneno kwenye majukwaa without delivery hayatusaidii sisi watanzania maskini ambao kila kukicha wengine wetu hatuna hata uhakika wa mlo wa siku. Kuna hoja za Katiba sasa hivi aingie hata huko atoe hoja zenye tija za kumkomboa mtanzania maskini, na watu wote watamsikia. Vinginevyo hapo CHADEMA bado inapwaya, mtakuja kuniambia!
 
tanira1 Sio barabara za kifahari, dhumuni ni kupunguza msongamano ili tuwahi kazini tuweze kushughulikia maji, imagine mtu una drive 21 km for three hours (tegeta to masaki) kila siku X2 means 6 hours back and forth... think.

hakuna suala la kujadili hapa,

Mkuu hebu tufikiri kidogo maana ni kawaida ya viongozi kubuni miradi ya aina hii kabla ya kufanya utafiti na matokeo yake inakuwa white elephant. Kwanza hebu tuelezwe ni jinsi gani flyover itakavyoweza kupunguza msongamano toka Tegeta hadi Masaki in your case . Pili hebu tupewe scope za hizo flyovers au mnadhani flyover ni additional road in the sky?
Tatu , tupewe basi mfano wa nchi ilisolve problem kama hii kwa kutumia flyovers. Mimi japo sio engineer wala nini ningeshauri zijengwe fast trains badala ya flyovers. Mjanja amngeangalia hili kwanza maana ni long term solution japo cost inaweza ikakaribia flyovers!!!!!. Mabasi ya speed ni upuuzi mwingine japo ni bora kuliko flyovers.
 
tanira1 Sio barabara za kifahari, dhumuni ni kupunguza msongamano ili tuwahi kazini tuweze kushughulikia maji, imagine mtu una drive 21 km for three hours (tegeta to masaki) kila siku X2 means 6 hours back and forth... think.

hakuna suala la kujadili hapa,

Madaktari wamegoma hawana vifaa vya kufanyia kazi. Ninyi mnawahi kazini mkashughulikie maji....kwa vifaa gani? Ninyi mnavyo? Au muwahi mkapige soga na kuandika yasiyotekelezeka?
 
Huyo Nassari hajuwi uchumi ni nini.

Ikiwa Dar ina wakazi million 5 na kati yao million 1 wanapoteza masaa 4 kila siku barabarani ina maana kwa siku wanapoteza miaka zaidi ya 365 na ukiwapunguzia nusu ya huo muda wanaopoteza njiani ina maana una faida ya miaka 182. Na kila unapowacha hilo tatizo huo muda haupunguwi unazidi.

kati ya barabara na maji kipi kiwe kipaumbele?
 
Back
Top Bottom