Nassari afunika nyumbani kwa sioi sumari 15/6/2012

ngurati

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
221
240
Katika Hali isiyokuwa ya kawaida, siku ya Jana mbunge aw arumeru mashariki Mhe. Nassari dogo janja, aliendesha harambee kwa ajili ya ku drill maji, kujenga vyoo na bweni kwenye shule ya mazoezi ya elimu Maalum Patandi iliyoko maeneo ya tengeru kwenye kata ya akheri.

Hii ndio kata anayotokea mbunge aliyetangulia na aliyekuwa mgombea Ubunge wa CCM sioi sumari.

Marehemu sumari aliahidi kuchimba maji kwa miaka na hakuwahi kutekeleza. Leo dogo janja katekeleza akishirikiana na wananchi (participatory development) . Heko kwako dogo janja, kutekeleza ahadi Mpaka nyumbani kwa mpinzani wako.
 
Huu ni muda wa utekelezaji wa ahadi sio kufunika na kufunua! utoto tu ndio unaomsumbua huyu kijana!
 
Kuahidi ni jambo moja na kutekeleza ni jambo jingine,watekelezaji ni wachache na anachofanya Nassari kwa sasa ni jambo ambalo wengi hushindwa kufanya.
Hongera Nassari.
 
Kafunika nini? Watu wanaitaji kuona yale yote aliyosema kwenye ahadi zake yanatimizwa kama kushusha bei ya sukari, na kujenga barabara.
 
Kuahidi ni jambo moja na kutekeleza ni jambo jingine,watekelezaji ni wachache na anachofanya Nassari kwa sasa ni jambo ambalo wengi hushindwa kufanya.
Hongera Nassari.

Kuitisha harambee ndio kutimiza ahadi? Kila siku JK na Lowassa wanaitisha harambee kwa hiyo wanatimiza ahadi.
 
Maendeleo huanza taaratibu, si mbaya dogo janja na anavyoendela maana hata miezi 3 hana anaonyesha kuwa ameanza kutambaa katika ahadi zake,tusubiri kuona atakapoanza kutembea na kukimbia, hongereni wana arumeru kwa kuchagua jembe lenu kuliko waliochagua wabwabwaji k.m lusinde,wasira, n.k
 
Kafunika nini? Watu wanaitaji kuona yale yote aliyosema kwenye ahadi zake yanatimizwa kama kushusha bei ya sukari, na kujenga barabara.

Ajenge barabara ni yeye anakusanya kodi? alichotuahidi huku Arumeru ni maji ambayo tayari sukari tunasubiri viwanda vitano vinavyojegwa huko Gombe
 
Huu ni muda wa utekelezaji wa ahadi sio kufunika na kufunua! utoto tu ndio unaomsumbua huyu kijana!

Kwani CCM walipokuwa Jagwani walikuja kufanya nini wasitimize ile miahadi ya baba mwanaasha ? halafu wameongeza nyingine kama tano wakati za mwanzo hata wajazishika
 
Kuitisha harambee ndio kutimiza ahadi? Kila siku JK na Lowassa wanaitisha harambee kwa hiyo wanatimiza ahadi.

maendeleo ni ya wananchi wenyewe, bali ishu ni kwamba nani anaweza kuwa mobilize the society to play that role!
 
hongera Josh Nassari na kuna kilaza mmoja jana alisema humu JF watu wa Arumeru Mashariki wanadai kwanini sukari haishuki bei... Chapa kazi kamanda
 
Unapanda jukwaani kuto ahadi ukimtegemea sabodo aje ajenge visima? huu si utoto jamani?

pole sana kwa kutegemea migongo ya watu wengine,umesikia akimwomba sabodo? Yeye kaitisha harambee ya wananchi wa jimbo lake, mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe, nyie mnasubiri kujengewa na ndio maana mnauza mali za wananchi, tutahakikisha wananchi wanapata haki zao
 
Asante kwa taarifa nilikua sijui kama SABODO ni mpiga kuwa wa arumeru.
 
Kuitisha harambee ndio kutimiza ahadi? Kila siku JK na Lowassa wanaitisha harambee kwa hiyo wanatimiza ahadi.
Kama harambee inafanyika kwa ajili ya kutimiza ahadi fulani kuna ubaya gani?Ulitaka Nassari atoe fedha zake mfukoni wakati wananchi nao wanatakiwa kuchangia kwa ajili ya maendeleo yao wenyewe na njia mojawapo ni hiyo harambee.
JK na Lowassa sijawahi kuwasikia wakiitisha harambee zaidi ya kuona wakialikwa katika kuzifanikisha,sijui unapata wapi habari kuwa wanaitisha harambee.
 
Unapanda jukwaani kuto ahadi ukimtegemea sabodo aje ajenge visima? huu si utoto jamani?
Sabodo hakuombwa kujenga visima bali ni dhamira yake binafsi ndio iliyomsukuma kusaidia kujenga visima baada ya kuona kijana ana nia ya dhati ya kuwaletea maendeleo wana Arumeru
 
Kafunika nini? Watu wanaitaji kuona yale yote aliyosema kwenye ahadi zake yanatimizwa kama kushusha bei ya sukari, na kujenga barabara.

mwenzako nape kitengo chake ni propaganda na uenezi wa magamba, tutajie wasifu wako ndani ya maukurutu-turned magamba!!!!
 
Nimegundua humu ndani watu wengi hawaelewi maana halisi ya mbunge na kazi zake zaidi ya kwenda bungeni na kutunga sheria.
 
Asante kwa taarifa nilikua sijui kama SABODO ni mpiga kuwa wa arumeru.

punguza ufinyu wa mawazo, sabodo si mwananchi wa arumeru,pili si mwanachama wa cdm, je kuna barua yoyote toka cdm aliyoandikiwa sabodo ya kuombwa msaada au ni yeye kwa roho ya kiibinadam aliamua kujitolea?
 
Back
Top Bottom