NASISITIZA:IKULU IMEHUSIKA KATIKA KUMTEKA NA KUMTESA Dr.STEVEN Ulimboka

Determine

JF-Expert Member
Apr 27, 2012
257
79
Ndiyo maana kila wakati Rais kikwete anapojaribu kukana tuhuma za ikulu kuhusika anashindwa kujenga hoja,matokeo yake anaishia kutuuliza wananchi ;kwa nini tunadhani serikali imtese Dr ulimboka? na anamaliza kwa kusema serikali haikuwa na sababu za kumteka Ulimboka,(anafunga mjadala)

ukisoma between lines maelezo haya ya RAIS yanaacha maswali mengi sana.ikwemo hili la kwamba kumbe serikali huwa inatabia ya kuteka/kutesa/kuua raia wake kama kuna sababu,sema kwa ULIMBOKA serikali haikuwa na sababu na huu ndo utetezi wa jk
 
Kwa kulifungia gazeti la Mwanahalisi, serikali imekiri kuhusika kwake katika kuteka, kutesa na ikibidi kuua wale inaowaita wakosoaji kama ilivyofanya kwa Dr. Stephen Ulimboka. Ili kuwanyamazisha madaktari Ikulu ilitoa maelekezo kiongozi wao akamatwe na ahojiwe na ikibidi ateswe hadi akiri kuwa kuna msukumo wa kisiasa nyuma ya mgomo wao. Kwa bahati mbaya Dr. Stephen Ulimboka, pamoja na mateso ya kunyofolewa kucha na kung'olewa meno, hakuwa tayari kusaliti msingi wa madai yao kwa serikali. Hilo liliposhindikana, nachelea kusema, agizo lilitolewa apotezwe katika misitu ya Mabwepande lakini kwa nguvu za Mwenyezi Mungu, hilo halikuwezekana kama ilivyopangwa.

Kwa bahati nzuri sana Dr. Stephen Ulomboka yuko hai na mbinu zote za Ikulu kujaribu kujisetieri kwa kipande cha kaniki zimegonga mwamba na kama mazuzu wamekimbilia kulifungia gazeti la Mwanahalisi. Wengine tulitegemea Mhariri Mkuu wa Mwanahalisi, Said Kubenea, kuburuzwa mahakamani lakini kila mwenye akili anajua kuwa huko serikali lazima iumbuke tu hivyo wameamua kuuchuna. Raisi Kikwete, Mkuu wa TISS Othman Rashidi na IGP Saidi Mwema wanajitahidi sana kufunika mambo lakini majina ya wahusika wote waliomteka na kumtesa Dr. Stephen Ulimboka tayari yanajulikana na sasa ni swala la muda tu...kwa kulifungia Mwanahalisi ndio wanazidi kuchochea moto.
 
Samahani wakuu naomba kuuliza. Hivi Ulimboka alisharejea Tanzania?.
 
Nimetoka kula ban mwezi uliopita.
Nilivyo na uchungu na mateso ya dr Uli,naona ntatoa nafasi ya kupewa 2nd ban!
 
tumeichoka hii habari sasa! watu tulishajua vichwani mwetu kuwa nani kahusika! tumetulia, tatizo jf sasa imenunuliwa sasa watu wakishapewa vi pesa kidogo wanakumbushia kumbushia! embu muacheni jembe atibike afu akija atatuambia vizuri! hizi stori za kwenye foleni za mabus mjini huku mmesimama tumezichoka bana!
 
ila haka ka technic kamesaidia,najaribu kuunganisha dot kwa yaliyomkuta lema na la docta kama napata jibu
 
Kwa masilahi ya nchi na wananchi wake, serikali huwa inafanya mambo kama hayo. Sitaki kuamini kwamba hili pia lilikuwa na maslahi ya nchi na wananchi wake!!
 
tumechoshwa na hizi thread za ulimboka jaman.sasa basi tutakuteka mpaka ww.iacheni hii serikali imalize awamu yake mpka hapo 2015 mtakapoamua kumchagua mchungaji WEAPON aongoze nchi yetu.
 
mbona hiyo inafahamika,iliyobaki ni kuchukua hatua zaidi ya haya tunayosisitiza.Japo kwa sasa sijui nihatua gani
 
Back
Top Bottom