Nasikia Malalamiko Kanda ya ziwa

GreatThinkers,
Ni kama wiki moja tuuu huyo jamaa yao kafungua barabara mpya pale Usagara Mwanza. Lakini Sehemu ya Feri kupaki na kupakia Magari ina SLOPE Kali kiasi kwamba hapatumiki, Ikipita inagusa mbele na nyuma hivyo inabaki hewani.Boti bado zinatia nanga sehemu ya ovyo ovyo ile ya zamani, wachina washasepa. Yeye kafungua!!

Vibanda vya kukatia tiketi vimewekwa upande wa Kulia barabara ya kutokea, ni UTUMBO mwingine am,bao hata yeye hakugundua. Mistakes ni kibao lakini ndiyo hivyo jamaa alisimikwa kwa bahati mbaya.

Si Si Em ni Uozo Mtupu!
duh hii kali babu
 
Spencer,Umenigusa sana mkuu, tutapigana kuhakikisha kwamba barabara hiyo inapita Bariadi na si Serengeti. I swear italeta maendeleo sana kwa jamii yote ya Mbulu, Bariadi na MaguTunahitaji hii Barabara mkoa wa Shimiyu. Hata serikali ya Marekani wameliona hilo na ziara ya mh Clinton itajaribu kuaddress hilo.Duh tupe barabara yetu
GreatThinkers, Naskia kuna malalamiko kuwa Kanda ya ziwa licha ya kuwa Migodi yote ya Dhahabu iko kule hakuna hata international airport, Mwanza airport ni kama shule ya kata ni kweli? Naskia Kuna malalamiko kuwa kanda ya ziwa licha ya kuwa asilimia hamsini ya wasomi wote tanzania wanatoka kule hakuna hata chuo kikuu hata kimoja cha serikali ni kweli? Naskia kuna malalamiko kuwa kanda ya ziwa licha ya kuwa na madini yanayoweza zalisha Cement yako pale Shinyanga hakuna hata mpango wa kujenga kiwanda licha ya kuwa 2005 mliahidiwa ni kweli? Naskia kuna malalamiko kuwa kanda ya ziwa mkoa mpya wa Simiyu umeomba ile barabara inayopita serengeti mmeomba ipitie Lamadi, bariadi kuja Hydom na kuunga Babati naskia wamekataa ni kweli? Naskia kuna malalamiko kuwa kanda ya ziwa viwanda pia hakuna licha kuwa muna bidhaa nyingi lakini vunajengwa siku hizi eti msafiri mkaombe vibarua Kibaha na bagamoyo ni kweli? Naskia kuna malalamiko kuwa wilaya nyingi za zamani kama Musoma vijijini,Shinyanga Vijijini hazina hata makao makuu lakini baadhi ya zilizoteuliwa juzi juzi tuu zimejengwa vizuri ile mbaya ni kweli? Sasa kama ni kweli mnangoja nini- Hameni wote Si Si EM inaonekana wanachumia kwenu halafu wanawekeza kule Chalinze
 
Spencer,

..yaani ungejua jinsi watu wa kanda ya Ziwa walivyoibeba Tanu kwa michango yao wakati wa harakati za uhuru za uhuru wa Tanganyika ndiyo ungesononeka zaidi.

..eneo la "Sukuma Land" wakati wa harakati za uhuru lilikuwa linachangia zaidi ya asilimia 34% ya mapato ya Tanu, wakati wao wana make only 14% ya total population ya Tanganyika wakati huo.

..hakuna sababu za msingi kwamba eneo la kanda ya Ziwa liwe nyuma kimaendeleo kiasi hicho.

..mapato ambayo serikali inayapata kutoka kwenye migodi dhahabu ya kanda ya Ziwa yalipaswa kuwekezwa ktk sekta nyingine kama kilimo,ufugaji, na uvuvi ambazo zina ushirikishi mkubwa zaidi kwa wananchi.
 
Spencer,

..yaani ungejua jinsi watu wa kanda ya Ziwa walivyoibeba Tanu kwa michango yao wakati wa harakati za uhuru za uhuru wa Tanganyika ndiyo ungesononeka zaidi.

..eneo la "Sukuma Land" wakati wa harakati za uhuru lilikuwa linachangia zaidi ya asilimia 34% ya mapato ya Tanu, wakati wao wana make only 14% ya total population ya Tanganyika wakati huo.

..hakuna sababu za msingi kwamba eneo la kanda ya Ziwa liwe nyuma kimaendeleo kiasi hicho.

..mapato ambayo serikali inayapata kutoka kwenye migodi dhahabu ya kanda ya Ziwa yalipaswa kuwekezwa ktk sekta nyingine kama kilimo,ufugaji, na uvuvi ambazo zina ushirikishi mkubwa zaidi kwa wananchi.

Unajua mkuu wanasiasa kutoka kanda ya ziwa bila kujali vyama wakakaa pamoja na kutoka na one stand kwamba tunataka haya yafanyike katika say budget hii lazima yatafanyika tu. Siasa za namna hii zipo dunia nzima, lakni kwa utaratibu wa kila mtu napokuwa eleveted kisiasa anahamia Dar kifikra na phyisically bado safarik ni ndefu maana tutaendelea kutegemea neema na busara za CCM.
 
Mkuu, umesema watu wa kanda ya ziwa wanakosa upendo kwa ndugu zao lakini naona hoja yako imejikita sana kwa mkoa wa Kagera peke yake, ebu tuambie watu wa Mwanza, Shinyanga, Tabora, then itakuwa vizuri ukatueleza watu wa wapi wana upendo na ndugu zao na uweke vielelezo kama ulivyoweka
Tuwe wakweli watu wa huko ni wala rushwa wazuri hebu tuangalie utitiri wa makatibu wakuu kutoka Kagera pekee na madudu yanayofanyika ukilinganisha na elimu waliyonao! Tuangalie pia nafasi zao kama mawaziri halafu matokeo ya utendaji wao! Tuna mifano hai kama Ndg yetu Chenge na kusaini mikataba mibovu akiwa Mwanasheria Mkuu, pili kuuza TRL kwa Rites! Pia tuna karamagi na TICTS na Meremeta scandals! Tukiacha hayo tuangalie kwenye sakata la EPA kuna hata wanasheria na watu wakuheshimika wengi kama wakina Amb. Rwezaura walichota mahela mengii na wengi wenye majina yanayofanania kama wakina Malegesi! Tuje Bw. Mkono na nae pia kama mwanasheria wa BOT, alisomba mapesa chungu nzima ukiacha influence yake katika Bunge yaani ana kofia tatu huyu Mbunge, Mwanasheria (practising) na NEC member sasa angalia anavyojitengenezea nafasi za kuiba! Tusimsahau Bwn Cheyo Mapesa huyu ni kada wa CCM anahongwa kila siku kudhoofisha upinzani!

Pili kwa wale wanaosema ati watu wa huko wamesoma sana mie ninapingana nao watu hawa wanaonekana hivyo kwa vile wamejikita zaidi kwenye serikali na taasisi za serikali kama vyuo na hospitali kama mtu anasema shule iliyopo huko Kagera ni Rubya pekee yenye kufaulisha isiyo na upinzani huo uwiano wa kuwa wamesoma zaidi ukilinganisha na idadi yao inatoka wapi? kama hata chuo kikuu huko ni kimoja tu yaani SAUT katika mikoa hiyo mitano yaani Shinyanga, Mwanza, Kagera, Mara na Tabora! na hata sasa katika shule zinazofaulisha bado za huko hazileti ushindani kama za kaskazini! Tujaribu kuwaangalia pia kwenye sekta binafsi au biashara ndipo tunaweza ku-judge kama wamesoma kweli au la?

Tuwe realistic kama watu wa kanda ya ziwa wanaamua kujisaidia wanauwezo huo hata leo kwa position zao serikalini hawahitaji Mchawi wa matatizo yao kabisa! ukichukulia wingi wao na pia hata katika mageuzi yaani 2015 nina uhakika wale wa Mara, Shinyanga na Mwanza watakuwa tayari ku-support upinzani lakini si wale wasomi wetu walio madarakani! sahau hao! Wakati huo huo Kagera ni mkoa wa CCM haswa kwa jinsi wana CCM walivyoweza kuwarubuni kwa hiyo si leo wala kesho watajikwamu toka lundo la matatizo!
 
ahaaa kaka ni international kwa sababu zinatua ndege za kenya hebu acha uzushi wewe mwanza kuna air strip hakuna hata kiyu kinachoitwa aitport kabisa.
 
Nyambala,Geza Ulole,

..u can have as many Ministers,PS,...frm one area.

..bila kuwa na shughuli ya uchumi ya maana ambayo inashirikisha watu wengi zaidi watu wa eneo husika hawawezi kuinuka hata siku moja.

..kinachotakiwa kufanyika kanda ya Ziwa, Kusini, etc etc ni kuinua sekta ambazo zinashirikisha wananchi wengi zaidi. hawa wananchi wakiwa na uwezo wa kujitegemea then wataweza kutamani vingine kama elimu bora kwa watoto wao etc etc.

..serikali haiwezi kumgawia kila mwananchi wa kanda ya ziwa mabonge/mapande ya dhahabu, lakini inaweza kusaidia kuinua/kuiboresha sekta ya kilimo, mfano cha pamba, ili hali za kiuchumi za wananchi ziwe bora zaidi.

..kuhusu elimu nadhani ni kukosa commitment tu, lakini jitihada zikifanyika inawezekana kabisa kuanza kufufua na kuboresha shule chache ambazo zitaweza kuzi-challenge shule zinazosifika sasa hivi. kitu cha msingi ni kwamba shule hizo ziwe zinachukua watoto wa walalahoi.

NB:

..naona Dr.Slaa yupo hapa. I hope he can chime in kuhusu matatizo/challenges/potentials za kanda ya Ziwa.
 
Mimi kwa kuangali jinsi kanda yetu ilivyo siyo siri machozi yananilengalenga

Nafikiri bado CDM tuna kazi kubwa kufanya Consciatization hata kwa miezi 3 non-stop mpaka kuhakikisha watu wa kanda ya ziwa wanatambua umaskini na utajiri wao walionao,kiasi kwamba hata mtoto wa chekechea aweze kuyataja haya hata kama anaamshwa usingizini ...hawaujuhi utajiri wao na hawaelewi kawa wao ni matajiri sana.
 
Nyambala,Geza Ulole,

..u can have as many Ministers,PS,...frm one area.

..bila kuwa na shughuli ya uchumi ya maana ambayo inashirikisha watu wengi zaidi watu wa eneo husika hawawezi kuinuka hata siku moja.

..kinachotakiwa kufanyika kanda ya Ziwa, Kusini, etc etc ni kuinua sekta ambazo zinashirikisha wananchi wengi zaidi. hawa wananchi wakiwa na uwezo wa kujitegemea then wataweza kutamani vingine kama elimu bora kwa watoto wao etc etc.

..serikali haiwezi kumgawia kila mwananchi wa kanda ya ziwa mabonge/mapande ya dhahabu, lakini inaweza kusaidia kuinua/kuiboresha sekta ya kilimo, mfano cha pamba, ili hali za kiuchumi za wananchi ziwe bora zaidi.

..kuhusu elimu nadhani ni kukosa commitment tu, lakini jitihada zikifanyika inawezekana kabisa kuanza kufufua na kuboresha shule chache ambazo zitaweza kuzi-challenge shule zinazosifika sasa hivi. kitu cha msingi ni kwamba shule hizo ziwe zinachukua watoto wa walalahoi.

NB:

..naona Dr.Slaa yupo hapa. I hope he can chime in kuhusu matatizo/challenges/potentials za kanda ya Ziwa.

We unaelekea huijui vizuri kanda ya ziwa, kwani Nyanza Cooperative Union ilikufa vp? si ufisadi tu halafu kulindana cha kushangaza waliyoiua walisomeshwa na NCU hiyo hiyo mpk kufikia kupewa kuiendesha! maswala kama barabara, railway na miundombinu kwa ujumla ni mipango na wapangaji wenyewe ndio wao (makatibu Wakuu N.K.) ila wako busy kushibisha matumbo yao! hamna wa kumlaumu hapa! a change of their mentality kwa hao wakubwa waliosahau kwao is needed
 
Jamani ebu tuaangalie na hawa viongozi, Basil Mramba, Daniel Yona, Grey Mgonja, Edward Lowassa, Frederick Sumaye, Anna Mkapa, hawa ni Mafisadi Papa mtu yoyote atujuze sehemu wanazotoka
 
Huwezi kuwa na maendeleo kama huna nia ya maendeleo hayo na kukubali gharama na misumbuko mengine bila kujali kuunganisha nguvu na kusaidiana katika mambo kadhaa
 
Jamani ebu tuaangalie na hawa viongozi, Basil Mramba, Daniel Yona, Grey Mgonja, Edward Lowassa, Frederick Sumaye, Anna Mkapa, hawa ni Mafisadi Papa mtu yoyote atujuze sehemu wanazotoka
labda tofauti ni kuwa hawajaibia miradi ya kwao kama Chenge na Rites au mikataba ya madini
 
Masele siyo mbunge wa shinyanga mjini ni mbunge wa viti maalaum kama walivyo akina Vicky Kamata na wengineo, samahani kaka usinikumbushe kuhusu huyo mtu
Kanda ya ziwa hakuna CCM tena ilishakufa baada ya uchaguzi.kwa mkoa wa shinyanga mbunge wa CCM ni Masele tu. wengine wanatumikia upinzani.

Tunasubiri 2014 tusimike serikali za mitaa zote CDM na UDP kwa Bariadi.Siku hizi hata sare za CCM wanavalia ukumbini hawana ubavu wa kutembea kifua mbele wanajua ni ngome ya CDM.

Siku hizi Shinyanga hakuna ugomvi wa kisiasa kwani CCM kilishageuka kuwa chama cha upinzani, chama tawala ni CDM, hilo liko wazi hata kwa wana-ccm wenyewe ndiyo maana hakuna vurugu
 
Kwa mtazamo wangu mabadiliko yoyote yanaletwa na wale wanaohitaji hayo maendeleo. Itakuwa ngumu kumpelekea maendeleo mtu ambaye hayo kwake si kitu. Mahitaji yanatoka kwa wananchi. Ni kweli kwamba kila mtz anateseka na ugumu wa maisha. Lakini cha ajabu tunakaa kimya na kubaki kulalamika tuuuuu!
Mie siamini kama kuna chama au mtu atatuletea maendeleo mezani. Wajibu wa chama au mtu ni kutoa awareness tuu ya kile kinachotakiwa ili hayo maendeleo yaje.kuna mchangiaji mmoja amegusia maendeleo ya mikoa kama kilimanjaro. Utakuta kule kumeendelea kwa sababu msukumo unatoka kwa wananchi. Kinachosaidia huo msukumo ni upeo, uelewa na msukumo wa kuyahitaji hayo maendeleo. Kazi ya chama au kikundi inakuwa ni kuunganisha hayo mahitaji na kutafuta namna ya kuyatekeleza. Mtekelezaji anaweza kuwa serikali au mdau yeyote katika eneo husika.
Mytake: sidhani kama kuna mtz asiyejua ya kuwa hali ngumu ya maisha inasababishwa na uongozi tulionao. Hivyo tujitokeze kuupinga na kudai maslahi yetu bila kuongopa. Katika dunia hii hata mbinguni hakuna jambo lolote zuri unaweza kulipata kirahisi. Hata mungu ili kutuletea ukombozi ilibidi amtume mwanae mpendwa yesu aje aumie ili ukombozi upatikane. Ili mbegu iote nyingine mpya ni lazima kwanza ioze, ili mshumaa uwake lazima uungue ili ulete mwanga, ili kiberiti kitua moto lazima kuwa na msuguano mkubwa ili iwake. Jaribu kufikiria na mambo mengine kama hayo utaona kwamba hakuna jambo lolote zuri linakuja kirahisi. Hii inatokana na kwamba unapokuwa unaumia kuna baadhi wanafaidika na kuumia kwako. Unapoanza kudai haki yako inamaana una disturb their confort zones.
Hivyo tusirudi nyuma, tuwaunge mkono wanaosimama kutusaidia walau kujua haki zetu. Tusiwe wanafiki bali tuwe "firm" kwa kuwatia moyo. Sisi pia tutumie nafasi zetu kuwaelimisha wenzetu kuhusu elimu ya uraia tukianzia kwenye famila zetu, makazini, vijiweni, makanisani, misikitini, tunapokua kwenye vyombo vya usafiri, mahospitalini na kila mahali tunapokuwa na nafasi ya kuzungumza kuhusu mustakabali wa nchi yetu basi tufanye hivyo. Wengi wenu mtaitwa nyie ni wafuasi wa chadema lakini msifadhaike mioyoni mwenu. Nchi yetu haitaweza kuondokana na hali hii ngumu kwa chama chochote, bali na wananchi wenyewe na kisha chama kikaja kuyasimamia yale ambayo tumeyaainisha.
 
GreatThinkers,

Suluhisho pekee ni utawala wa majimbo kama ambavyo CDM imekuwa ikituamsha. Haiingii kichwani kwa mtu mzima kuona wadogo zangu wanakamatwa kama wazuraraji DAR wakati wameenda kutafuta kazi sehemu ambayo malighafi kutoka kwao imepelekwa.

Kwa nini watu wafanywe namna hii ndani ya taifa lao?
 
GreatThinkers,Suluhisho pekee ni utawala wa majimbo kama ambavyo CDM imekuwa ikituamsha. Haiingii kichwani kwa mtu mzima kuona wadogo zangu wanakamatwa kama wazuraraji DAR wakati wameenda kutafuta kazi sehemu ambayo malighafi kutoka kwao imepelekwa.Kwa nini watu wafanywe namna hii ndani ya taifa lao?
Wazururaji mbona ata mwanza polisi wanawakamata? Au wazururaji wanaokamatwa wote ni wasukuma,wakerewe, wazinza? tusaidie mkuu
 
Kusema zaidi ya asilimia 50 ya wasomi Tz wanatoka kanda ya ziwa, imenifanya nisiiamini hoja yako. Labda kwa kuwa UMESIKIA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom