Nasikia Malalamiko Kanda ya ziwa

GreatThinkers,
Ni kama wiki moja tuuu huyo jamaa yao kafungua barabara mpya pale Usagara Mwanza. Lakini Sehemu ya Feri kupaki na kupakia Magari ina SLOPE Kali kiasi kwamba hapatumiki, Ikipita inagusa mbele na nyuma hivyo inabaki hewani.Boti bado zinatia nanga sehemu ya ovyo ovyo ile ya zamani, wachina washasepa. Yeye kafungua!!

Vibanda vya kukatia tiketi vimewekwa upande wa Kulia barabara ya kutokea, ni UTUMBO mwingine am,bao hata yeye hakugundua. Mistakes ni kibao lakini ndiyo hivyo jamaa alisimikwa kwa bahati mbaya.

Si Si Em ni Uozo Mtupu!
 
mhh Mwanza International airport!!!

An international airport is an airport typically equipped with customs and immigration facilities to handle international flights to and from other countries. Such airports are usually larger, and often feature longer runways and facilities to accommodate the large aircraft commonly used for international or intercontinental travel. International airports often host domestic flights (flights which occur within the country) in addition to international flights.

Nimeshapanda ndege hapo Mza kuelekea Nairobi, Entebe na DRC, madege yale makubwa yanayobeba samaki yanapaa direct kuanzia pale Mza kwenda ubelgiji, Uholanzi na pia Urusi.
 
Nyambala,

Uwanja una uzio? kwa nini mifugo inalisha pale?

Je unajua wananchi wa Igombe wanakatisha Uwanjani kwenda makwao, kiusalama ni sawa?

Unajua ni njia moja tuu ya ndege kupaa na kutua?

Unajua ule uwanja ni wa jeshi?

Unajua pale hata watu hamsini hawawezi kukaa katika viti kwa wakati mmoja, halafu AC haifanyi kazi?

Unazifahamu vizuri shule za kata, zimejengwa kuridhisha tu watunzania ila si kweli kwamba ni kwa dhati ya kukuza elimu tanzania.

Ndio uwanja wa mwanza ulivyo.
 
Uwanja wa ndege wa mwanza haujawahi kuwa wa kimataifa hata kidogo licha ya kwamba kuna wakati midege mikubwa ya ulaya ilikuwa inatua kuchukua minofu ya samaki. Uwanja ule hauna hadhi ya kuwa wa kimataifa vinajulikana viwanja 2 tu vya kimataifa i.e. KIA na Dar. Mfuko wa cement mwanza unauzwa sh. 18,000 wakati pale dodoma unauzwa sh. 13,500. Kuna wakati serikali iliahidi kujenga kiwanda hicho mkoani shinyanga lakini kimya. Ukiacha SAUT, kanda ya ziwa haina chuo cha maana cha umma wala cha binafsi.
 
Naona vijana wa Nape kwenye thread hii hawajatia pua maana ukiangalia ki uhalisia mpaka wao moyoni inawachoma!
 
Nyambala,

Uwanja una uzio? kwa nini mifugo inalisha pale? - Kwani ule wa Dar ukiingiza ng'ombe unafikiri hawatakula zile nyasi around?

Je unajua wananchi wa Igombe wanakatisha Uwanjani kwenda makwao, kiusalama ni sawa? - Mpaka miaka ya mwanzoni na ktkt mwa 90's watu walikuwa wanakatiza uwanja wa DIA.

Unajua ni njia moja tuu ya ndege kupaa na kutua? - Hata uwanja wa DIA ulikuwa hivyo zamani na bado ukaitwa international airport

Unajua ule uwanja ni wa jeshi? - Of course ulikuwa, kwa sasa siyo!

Unajua pale hata watu hamsini hawawezi kukaa katika viti kwa wakati mmoja, halafu AC haifanyi kazi? - Sawa kabisa, nadhani mkuu usiombe ufike Ndjamena

Unazifahamu vizuri shule za kata, zimejengwa kuridhisha tu watunzania ila si kweli kwamba ni kwa dhati ya kukuza elimu tanzania.

Ndio uwanja wa mwanza ulivyo. - Sio kwamba mahitaji ndiyo yaliufanya uboreshwe?

Anywayz mkuu kifupi ni kwamba usafiri wa anga Tz bado sana hata ile airport ya Dar haina hadhi ya kuwepo ndani ya jiji lenye watu 5 million. Nakubaliana na wewe uwanja ule unahitaji kuboreshwa na hasa lile jengo. Lakini masuala ya ndege mfano BA au KLM, Emirates kutua pale hata kwa sasa wanaweza lakini je kuna mahitaji? Kumbuka hizo ndege sio kwamba hazitui Mza kwa sababu ya uwanja. Wale ni wafanya biashara kukiwa na mahitaji watakuja tu. Hawasubiri serikali iwaambie au kuwapangia. In that respect utakuta ndege kama Lufthansa, Air France haziji tena Dar, si sababu ya uwanja.
 
Yote uliyoongea ni kweli kabisa, licha ya rasilimali zote hizo za kanda ya ziwa hakuna maendeleo yoyote ya maana...
 
Me ningeshauri tujitenge tukaanzshe nchi ye2 ya lake zone ambayo itajali maslahi ya wananch wa kanda ya ziwa,inauma sana kuona mapato yanayotokana na mauzo ya dhahabu yakienda kujenga magorofa na barabara za bagamoyo na darslam wkt sis huku ndugu ze2 wanauliwa kwa risas kila kukcha.ila nadhan mwisho wa haya yote umewadia,kitaeleweka tu.
 
Naona vijana wa Nape kwenye thread hii hawajatia pua maana ukiangalia ki uhalisia mpaka wao moyoni inawachoma!
Blaza!! kanda ya kusini wana mkondo wa Gas na mafuta,chuma na makaa ya mawe,siyo bling bling..Hebu angalia wanavyoonewa,
Lakini ni watu wenye amani na hubeba tabasamu na kukubali madharau yenu,kama hawajui vile,bali wanajua.Hata rais kutoka kwao kajenga bungalow lushoto na si masasi.
Hawa binadamu wanasota sana,ni wakimbizi wa kiuchumi hapa Dar,wanastruggle sana,na ni wafanyabiashara wazuri tu!...bila ya wao Dar ingekuwa ngumu sana.Wamachinga wengi wamesaidia sana kuukuza uchumi wa Dar,kwa biashara ndogondogo na vitu chee kwa haraka,God bless them.
Blaza!!...hawa watu mnaowadharau ndio wanawaangalia sana nyie muwakomboe kutokana na elimu zenu,wanachangia sana nguvu ya CDM,ila wanaanza kuona mnavyowatenga and thats wrong bro!
Ni sawa na watu kuwadharau wazaramo kama hawajui kuwa wakamba walivamia moshi mpaka milimani,wakamba wakaja mpaka Dar na pwani,lakini chifu Pazi na jeshi lake wakawatimua wakarudi makwao na wengi waliuawa,hapo ndio chifu Pazi wakamwita "Pazi Mwingakamba" maana yake,PAZI mfukuza wakamba.-Souce"Zamani Mpaka Siku Hizi"
Kla kanda na kabila linas mchango wake,kama mnaona mnaonewa,poa ila wafikirieni watanzania wengine.Hii haihusu uchama bali utaifa!
 
Anywayz mkuu kifupi ni kwamba usafiri wa anga Tz bado sana hata ile airport ya Dar haina hadhi ya kuwepo ndani ya jiji lenye watu 5 million. Nakubaliana na wewe uwanja ule unahitaji kuboreshwa na hasa lile jengo. Lakini masuala ya ndege mfano BA au KLM, Emirates kutua pale hata kwa sasa wanaweza lakini je kuna mahitaji? Kumbuka hizo ndege sio kwamba hazitui Mza kwa sababu ya uwanja. Wale ni wafanya biashara kukiwa na mahitaji watakuja tu. Hawasubiri serikali iwaambie au kuwapangia. In that respect utakuta ndege kama Lufthansa, Air France haziji tena Dar, si sababu ya uwanja.

Kiusalama ili ndege itue inahitaji runway ya kutosha, kwa mfano kama ndege inahitaji 1km kutua yaani kukimbia mpaka kufunga brake, inatakiwa iwepo 1km ya ziada kama ndege hiyo itahitaji kuruka kwa dharura baada ya kutua, Mwanza airport hauna kiwango hicho na hata hizo ndege kubwa zinazotua zinatua kwa kulazimisha tu, ikitokea ndege kubwa imeshindwa kupaa mza airport hiyo ni ajali maana itaingia ama kwenye ziwa au itaparamia milima, runway ni fupi sana, ukiwaunapaa mza airport na ndege kubwa huwa unamaliza runway kabisa ndio ndege inapaa, hiyo ni hatari sana, ila huwa hatujiulizi tu! Uwanja ule unahitaji matengenezo makubwa na upanuzi mkubwa ili kufikia international standard.
Sijaongelea mambo mengine mengi, ukitaka kuendelea usijilinganishe na wengine walionyuma, hebu tuangalie hata ndugu zetu wa Kenya jomokenyata international airport, kama umewahi kuwa pale utaona utofauti, wala tusiende mbali kama Thabo airport ya j'berg navingine vingi, Watz tunahitaji uongozi makini wa kusimamia raslimali ili ziwanufaishe wazawa, kanda ya ziwa ilitakiwa ifanane na almasi, dhahabu, pamba , samaki na mifugo waliyonayo achilia mbali mbuga walizonazo!
 
Nyambala,

Uwanja una uzio? kwa nini mifugo inalisha pale?

Je unajua wananchi wa Igombe wanakatisha Uwanjani kwenda makwao, kiusalama ni sawa?

Unajua ni njia moja tuu ya ndege kupaa na kutua?

Unajua ule uwanja ni wa jeshi?

Unajua pale hata watu hamsini hawawezi kukaa katika viti kwa wakati mmoja, halafu AC haifanyi kazi?

Unazifahamu vizuri shule za kata, zimejengwa kuridhisha tu watunzania ila si kweli kwamba ni kwa dhati ya kukuza elimu tanzania.

Ndio uwanja wa mwanza ulivyo.

Mkuu ebu tusaidie hapa Tanzania kuna Airport gani nzuri sisi wengine atujui
 
Tatizo la watu wa kanda ya ziwa ni kukosa upendo kwa ndugu zao. Huwezi kuamini kijiji anachotokea msemaji mkuu wa ikulu ndugu Salva Rweyemamu hakufikiki kwa barabara,ni njia za baiskeli wala hawana mpango wa kujenga barabara si leo wala kesho. Anapotokea ndugu Dr mwl.Azavel Rweitama hamna huduma yoyote ya kijamii tofauti na kanisa la kikatoliki na msikiti mdogo na maduka kama 7 pamoja na gulio la kila jumapili tu. Ukienda kwa prof Mukandara,makamu mkuu wa chuo cha UDSM hamna hata hospitali,kuna sekondari za kata kama mbili au tatu ambapo mtoto utembea kilometre12 kwenda na kurudi nyumbani kwa mguu au mwenye uwezo ana mountbike,kule kwa magufuli watu wanajivunia aidha kuwa wawindaji au wafugaji, Anapotokea ndugu Kagasheki kuna uafadhali mana kuna maji,umeme,lami na kiwanda kichakavu cha CocaCola na uwanja wa ndege mithili ya kipande cha barabara pale bukoba mjini. Kwa prof.Ana Tibaijuka ndo kumefulia na hata hamna cha kujivunia,kule kwa dr.Kamara hata hakutamaniki,nakuhakikishia chakula kikuu ni viazi vitamu na maharage,ndizi hamna kwa kuwa kule hali ya udongo ni mbaya na migomba ukua kwa kimo cha mwanadamu. Kule hamna barabara,hamna centre,hamna hospitali,hawategemei kuwa na umeme kwa miaka ya uhakika10 ijayo huko kunaitwa Rushwa. Hiyo si utani ni jina la tarafa tangu miaka ya60. Kagera hamna chuo kikuu wala Technical school,watu wakimaliza form6 inawabidi waje mwanza au dsm! Shule pekee imayoweza na kwa miaka yote imewatoa wasomi wa kiume kanda ya ziwa ni Rubya Seminari,shule iyo haina mshindani hata mmoja,nakuhakikishia kuwa 95% haliye juu ktk utawala wa taifa ili,wahadhiri,mapdre,madiwani,wanasheria na wahasibu ni wa shule iyo. Sijagusia mwanza,shinyanga ,mara na Musoma,n.k. Sasa kwa hali kama iyo nani ataweza kusimama na kuijenga Kagera ikiwa ktk kanda ya ziwa? Kagera kuwa na wasomi wengi haina maana,ni sawa na Tanzania ilivo na raslimali nyingi na ni maskini. Wanakagera,mnaudhalilisha mkoa wenu!
 
Ndugu nakuunga mkono mawazo yako, na sio Kagera tu, angalia Tabora, kila mwaka kunamawaziri wanatokea tabora, tabora wametoa mpaka speaker, wazili wa elimu nk, lakini nenda kashuhudie mkoa ulivyo yaani wanashindwa hata kuwapa wenzao ufahamu wa kujitambua kwamba maisha ya kimaskini wanayoishi ni kwa sababu ya mawazo yao mgando, wamekuwa wabinafsi na watu wa kutaka kunyenyekewa na watu wa kwao, jamani mlio na upeo saidieni kuwafumbua wananchi macho na akili ili wajitambue na kubadili hali zao za maisha na hapa namaanisha watumie sanduku la kura vizuri sio kuchakua six kwa sababu ni six angalia six amefanya nini kwa miaka yote hiyo kama huoni alichofanya chagua chama mbadala.
 
Tatizo la watu wa kanda ya ziwa ni kukosa upendo kwa ndugu zao. Huwezi kuamini kijiji anachotokea msemaji mkuu wa ikulu ndugu Salva Rweyemamu hakufikiki kwa barabara,ni njia za baiskeli wala hawana mpango wa kujenga barabara si leo wala kesho. Anapotokea ndugu Dr mwl.Azavel Rweitama hamna huduma yoyote ya kijamii tofauti na kanisa la kikatoliki na msikiti mdogo na maduka kama 7 pamoja na gulio la kila jumapili tu. Ukienda kwa prof Mukandara,makamu mkuu wa chuo cha UDSM hamna hata hospitali,kuna sekondari za kata kama mbili au tatu ambapo mtoto utembea kilometre12 kwenda na kurudi nyumbani kwa mguu au mwenye uwezo ana mountbike,kule kwa magufuli watu wanajivunia aidha kuwa wawindaji au wafugaji, Anapotokea ndugu Kagasheki kuna uafadhali mana kuna maji,umeme,lami na kiwanda kichakavu cha CocaCola na uwanja wa ndege mithili ya kipande cha barabara pale bukoba mjini. Kwa prof.Ana Tibaijuka ndo kumefulia na hata hamna cha kujivunia,kule kwa dr.Kamara hata hakutamaniki,nakuhakikishia chakula kikuu ni viazi vitamu na maharage,ndizi hamna kwa kuwa kule hali ya udongo ni mbaya na migomba ukua kwa kimo cha mwanadamu. Kule hamna barabara,hamna centre,hamna hospitali,hawategemei kuwa na umeme kwa miaka ya uhakika10 ijayo huko kunaitwa Rushwa. Hiyo si utani ni jina la tarafa tangu miaka ya60. Kagera hamna chuo kikuu wala Technical school,watu wakimaliza form6 inawabidi waje mwanza au dsm! Shule pekee imayoweza na kwa miaka yote imewatoa wasomi wa kiume kanda ya ziwa ni Rubya Seminari,shule iyo haina mshindani hata mmoja,nakuhakikishia kuwa 95% haliye juu ktk utawala wa taifa ili,wahadhiri,mapdre,madiwani,wanasheria na wahasibu ni wa shule iyo. Sijagusia mwanza,shinyanga ,mara na Musoma,n.k. Sasa kwa hali kama iyo nani ataweza kusimama na kuijenga Kagera ikiwa ktk kanda ya ziwa? Kagera kuwa na wasomi wengi haina maana,ni sawa na Tanzania ilivo na raslimali nyingi na ni maskini. Wanakagera,mnaudhalilisha mkoa wenu!

Mkuu, umesema watu wa kanda ya ziwa wanakosa upendo kwa ndugu zao lakini naona hoja yako imejikita sana kwa mkoa wa Kagera peke yake, ebu tuambie watu wa Mwanza, Shinyanga, Tabora, then itakuwa vizuri ukatueleza watu wa wapi wana upendo na ndugu zao na uweke vielelezo kama ulivyoweka
 
Nadhani CDM wanatakiwa kulitumia hili kuwaelezea watu hasa wa vijijini wajuwe walivyo nyuma. Tatizo la watu wa kanda ya ziwa wengi hawajui kama wanaonewa kiasi hicho maana wengi hawajawahi kutoka katika vijiji walivyo zaliwa na hii ndo advantage ya chama cha magamba.

Watu wanaotoka kanda ya ziwa na wameshalijua hili ni wajibu wao kushirikiana na CDM kuweka mikakati ya kuwaelewesha watu wa kanda ya ziwa namna wanavyo nyonywa na magamba.

Likifanyika hili CDM watajiimalisha sana kanda ya ziwa. Nadhani kunakitu cha ajabu sana maana nimekutana na watu wengi sana amabao wanaunga mkono CDM wengi wanatoka kanda ya ziwa. Sijawahi kukutana na mtu wa kanda ya ziwa Dar anayeunga mkono CCM(magamba).

Upinzani wa kanda ya ziwa kwa CCM unatoka ndani ya moyo wa kila mmoja wala si mobilasation ya CDM. Huu ni upinzani wa kweli sana ambao CDM wanapashwa kujivunia na kuulea kwa umakini mkubwa ili kufanikisha malengo yao ya kisiasa.

Kanda ya ziwa lazima waongeze bidii ya kuwaelimisha na wenzao walioko vijijini walijuwe hili ili waunge mkono harakati hizi za kujikomboa.
CCM wanaweza kulichukulia hili ni kujibagua kwa kanda ya ziwa lakini ubaguzi huwa hautokani na maumivu ya ndani kama ilivyo sasa kwamba watu wa kanda ya ziwa wanaichukia CCM kwa mioyo yao na wale si kwa kushawishiwa na mtu.

Mungu ibariki Tanzania na watu wake wema!
Amen
 
Uwanja wa ndege wa mwanza haujawahi kuwa wa kimataifa hata kidogo licha ya kwamba kuna wakati midege mikubwa ya ulaya ilikuwa inatua kuchukua minofu ya samaki. Uwanja ule hauna hadhi ya kuwa wa kimataifa vinajulikana viwanja 2 tu vya kimataifa i.e. KIA na Dar. Mfuko wa cement mwanza unauzwa sh. 18,000 wakati pale dodoma unauzwa sh. 13,500. Kuna wakati serikali iliahidi kujenga kiwanda hicho mkoani shinyanga lakini kimya. Ukiacha SAUT, kanda ya ziwa haina chuo cha maana cha umma wala cha binafsi.

Mkuu, naona umeamua kujifariji na kujiliwaza, na maneno yako kuwa Tanzania kuna viwanja vya ndege vya kimataifa viwili tu, KIA, DAR, sijui umetumia vigezo gani mkuu, naongelea DAR sababu nimeishakitumia sana uwanja kuna choo kimoja kwa ajili ya wasindikizaji, uwanja kuna viti kama 20 kwa ajili ya wasindikizaji, uwanja hauna hotel, uwanja, hakuna feni joto kila kona, uwanja hauna huduma za jamii kama hospital, benki, sehemu za kupumzika. bado ndani ndio balaa tupu
 
Similar Discussions

19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom