Nasikia kuna degree za "chupi"

tanzania kwetu

New Member
Apr 17, 2012
3
0
Jamani wana jf naomba mnisaidie katika hili,juzi katika pita pita zangu nilikuta watu wakizungumzia kuhusu degree ambazo wanachuo huzipata huko wanakoita chuo kikuu.
Sikuelewa pale nilipomsikia mmoja wa wachangiaji wa ile mada akisema "kwani siku hizi ni degree basi!,ni degree za chupi tu"kwa sababu nilikuwa nasubiri gari sikuweza kumuelewa anamaanisha nini,hebu wewe nisaidie kama unaelewa
Asante!
 
Mkuu, unachoshangaa ni degree zachupi? Je huna taarifa kwamba kuna hata Uwaziri wa chupi, Ukuu wa mkoa wa chupi, Ukuu wa wilaya wa chupi, Ubunge wa kuteuliwa wa chupi nk? Rushwa ya ngono nchi hii haitamalizika kwani mizizi yake iko hata kwa viongozi wakubwa wa kitaifa letu.
 
degree za chupi zinamaanisha mabinti wameenda kusoma chuo lakini uwezo wao ni mdogo ila wamebebwa na waalimu wao kwa kutembea nao wakawa wanapewa mitihani,test na kupewa maksi nzuri mtindo huu nasikia upo sana IFM,CBE,UDSM
 
Digrii ya chupi ni my daili bred is injinia! Am soli am glad i remove my name!
 
This reminds me! Miaka ya 90, kuna waanafunzi watano toka kitivo fulani UDSM walitakiwa kurudia mitihani (supplementary), waliporudia wakashikwa tena. Mmoja wao (binti) akamuendea lecturer wakaongea akachomoa. Kijana mmoja alipogundua hilo nae akamfuata lecturer lakini akatolewa nje.

Siku mbili baadae akamkuta lecturer yupo UDASA anapata kilaji na wenzake, dogo akamfuata lecturer na akamwambia: "Fulani (akimtaja yule binti) tulikuwa na matatizo sawa na ukamsaidia, na mimi naomba unisaidie. Kama ni kuvua tu chupi nami nitakuvulia hata sasa hivi".

Btw: Usiniulize kilichotokea baada ya hapo....
 
hizo ndo posho wanazojilipa walimu kwa kazi 'ngumu ya kufundisha' baada ya serikali kuwatupa..< kwa mujibu wao wenyewe >
 
Umenifurahisha sana, kama mie nilivyokoment kwenye moja ya thread za huyu jamaa.
 
degree za chupii? inamaana wanasemwa dada zetu kuwa vilaza wanategemea kutoa...ndo wafaulu. je hakuna wanaume wanaopata digriii hewa na hawa tutaita wanapata degree za aina gani? au nao hivohivo?
 
Nadhani hii ni mfululizo wa threads za kumdhalilisha mwanamke kama kawaida ya hapa JF.
Yaani miaka mitatu/minne/mitano.Assigments,tests,mitihani ya term,finals,disertation vyote alale na malecturer ni Uongo...na masomo yenye malecturer wanawake ??
 
hakuna kudharirisha mwanamke ni kweli zipo tena nyingi tu, na darasani inakuwa inajulikana nani kafaulu kwa kutembea na lecturer flan
 
Mkuu, unachoshangaa ni degree zachupi? Je huna taarifa kwamba kuna hata Uwaziri wa chupi, Ukuu wa mkoa wa chupi, Ukuu wa wilaya wa chupi, Ubunge wa kuteuliwa wa chupi nk? Rushwa ya ngono nchi hii haitamalizika kwani mizizi yake iko hata kwa viongozi wakubwa wa kitaifa letu.

ENG Stella Manyanya
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom