Nashindwa kuzipenda filam za bongo....

mimi natofautiana na wewe kidogo. Mimi napenda zile za kuchekesha kama pasu kwa pasu, arosto, inyee, vyumba vimejaa na kadhalika.
lakini sijui wakina kanumba,ray sijawahi kuangalia hata nusu movie. kwanza mimi sijawahi kununua hizo bongo movie wala siziangalii na sizitaki kabisa. mimi ndo nina beef kabisa coz sitaki kuona mtu anaziangalia. labda sina uzalendo. mi napenda wakina mtanga, majuto, masele, sharobalo,rutale, matumain nk.
napenda movie za viwango kama za jason bourne na wrong return 4. Mia
 
Mimi sikuwahi kuangalia bongo movie nikaimaliza.sipendi hata kuziona....waigizaji ni mambumbumbu na washamba sanaaaa...hawataki kujifunza kabissaaaaaaaaaa
 
Naona mzuka kwa watu unaongezeka

kuhusu hizi filam za bongo.....kwenye media na watu..

Sasa mimi najiuliza.kwa nini nashindwa kuzipenda hizi
filam za bongo????

Yaani nashindwa hata kutazama dakika ishirini tu ya filam hizi...

sababu kubwa ma actor wa kibongo hawauvai uusika kikamilifu na hakuna originality kwenye scrpt zao pia tunaitaji shule for filiming sasa ivi kuiga ni kwingi film moja tu ya kibongo worth watchin ni fimbo ya mnyonge na komedy za king ma
 
kwenye sanaa kumekuwa sehemu za kujitangazia biashara zo za mwili na nafasi ya kubomoa ndoa na mapenzi ya wapendanao. sizipendi coz hazina ujumbe na siwapendi wahusika coz wana nyodo. over
 
miaka 50 ya uhuru wameweza wamethubutu na wanasonga mbele.............with their both feet up in their asses! cant take even a sec to watch such craps! na mapoda yao
 
kuna mdau yoyote wa film za kibongo antuambie katika hizi movie kama kuna moja kali ambayotuna weza kuangalia tuone kiwango chao?
 
Wakuu,

Hawa akina Kanumba na wenzao wanachokifanya ndiyo mwisho wa uwezo wao (angalau kwa harakaharaka). Wako wapi wenye ujuzi wasaidie katika mawazo walau kwa kuandaa visa vinavyoeleweka? Wako wapi wajanja wa computer wasaidie kutengeneza sinema zenye effects zinazovutia?

Watu wenye uwezo wa mawazo hushia kulaumu hawataki kuandika filamu. Mabingwa wa computer wanataka waajiriwe Infotech, basi. Kukerwa na sinema za Bongo ni hatua moja na kufanyia kazi kero hiyo ni hatua nyingine. Tusitegemee kuendelea "kumfunda" Kanumba ili afanyie kazi ushauri wetu.... huenda hawezi kuu-interpret. Mfano, pamoja na Kanumba na Ray kuwa na mionekano ya kuvutia huenda wakashindwa kuact na kubehave kama Kiongozi wa nchi ila wanaweza wakang'ang'ania ku-act kwa kuwa wao ndiyo "wasanii" maarufu. Tunahitaji watu wengine waje na mawazo mengine. Hawa akina Wema wamefanya kile wanachoweza. Akina Bambo, Mtanga, Sharo milionea wamefanya kile wanachoweza. Mzee Majuto, Small wa Ngamba, Fundi Saidi (Mzee Kipara), Rajab Hatia (Pwagu), Ibrahim Raha (Mzee Jongo), Abdallah Mkumbila (Mhogo Mchungu), Onyango n.k. wamefanya walichoweza. Wamefanya walichoweza.

Tunahitaji akina James Cameron, Peter Jackson, George Lucas, Gore Verbinski, Tim Burton, Mel Gibson, J. R. R. Tolkien, Lewis Carol, Bishop Hiluka, Hermie Rajab (alale peponi) etc wengi zaidi Tanzania kuliko tunavyowahitaji akina Nicholas Cage, Denzel Washington (The Boss wa JF!), Johnny Depp.

Tunahitaji wababe wa kompyuta watusaidie katika kuboresha sinema zetu. Tuchukizwe na viwango vidogo vya sinema zetu halafu tuchukue hatua za vitendo za kuleta mapinduzi.
 
Tatizo lao kubwa wanaigiza maigizo?! Ila afadhali kidogo movies za JB, na zenye title ( majina ) za Kiswahili nimegundua nying huwa zina unafuu kwny uafadhali , ila Ukiona movie imetungwa Ray ikaushie usije ukapoteza pesa zako arifu?! Cheki kuna moja inaitwa SWAHIBA na nyingn MASAA 24 utazipenda..
 
wanajua kuwa hawawezi kuuza filamu zao bila kuweka maeneo mengi ya mapenzi,wanajua wabongo wengi wanavutiwa na michezo ya ngono au ifananayo.Ukifanya utafiti utaona % kubwa ya hizi picha ni wadada wanakaa nusu uchi ili kuvuta hisia za watu wanaopenda ngono na kuangalia hii pia angali makava yao.Bora nyie mnaziangalia mimi kwa zile nilizoziona basi nimeziona kwenye basi ninaposafiri,vinginevyo ni heri nimsikilize jangala na mzee mundu ila sio kucheki uchafu
Nimekusoma unapenda za Malawi
 
Upo ugonjwa wa watanzania kutokupenda 'made in tanzania'.Ugonjwa huu mbaya unaitwa "ukuvyata"- Ukosefu wa Kupenda vya Tanzania" Ugonjwa huu umedumaza sana uchumi wetu.
 
Naona mzuka kwa watu unaongezeka

kuhusu hizi filam za bongo.....kwenye media na watu..

Sasa mimi najiuliza.kwa nini nashindwa kuzipenda hizi
filam za bongo????

Yaani nashindwa hata kutazama dakika ishirini tu ya filam hizi...

Inawezekana umeathirika na ile kasumba, vizuri vya ulaya tu. Nyingine ni nzuri sana hasa za kina Ray na Kanumba ni za high quality at least
 
Inawezekana umeathirika na ile kasumba, vizuri vya ulaya tu. Nyingine ni nzuri sana hasa za kina Ray na Kanumba ni za high quality at least

filam za ki nigeria zina hitilafu nyingi saana lakini naweza kutazama
zipo ambazo story inakushika mpaka filam inakwisha hujaboreka wala kuyaona mapungufu ingawa yapo meengi

natazama za ki Nigeria nyingi tu
za ki Ghana nyingi tu
hata za ki Kenya nzuri zipo
za kiTZ sio kwamba zote mbovu
nimetazama KOLELO ya Irene Sanga niliipenda na za Mzee Majuto nazipenda
but hizi za kina Kanumba na wenzao nashindwa hata dakika kumi...hata nikijilazimisha...
 
Wakuu,

Hawa akina Kanumba na wenzao wanachokifanya ndiyo mwisho wa uwezo wao (angalau kwa harakaharaka). Wako wapi wenye ujuzi wasaidie katika mawazo walau kwa kuandaa visa vinavyoeleweka? Wako wapi wajanja wa computer wasaidie kutengeneza sinema zenye effects zinazovutia?

Watu wenye uwezo wa mawazo hushia kulaumu hawataki kuandika filamu. Mabingwa wa computer wanataka waajiriwe Infotech, basi. Kukerwa na sinema za Bongo ni hatua moja na kufanyia kazi kero hiyo ni hatua nyingine. Tusitegemee kuendelea "kumfunda" Kanumba ili afanyie kazi ushauri wetu.... huenda hawezi kuu-interpret. Mfano, pamoja na Kanumba na Ray kuwa na mionekano ya kuvutia huenda wakashindwa kuact na kubehave kama Kiongozi wa nchi ila wanaweza wakang'ang'ania ku-act kwa kuwa wao ndiyo "wasanii" maarufu. Tunahitaji watu wengine waje na mawazo mengine. Hawa akina Wema wamefanya kile wanachoweza. Akina Bambo, Mtanga, Sharo milionea wamefanya kile wanachoweza. Mzee Majuto, Small wa Ngamba, Fundi Saidi (Mzee Kipara), Rajab Hatia (Pwagu), Ibrahim Raha (Mzee Jongo), Abdallah Mkumbila (Mhogo Mchungu), Onyango n.k. wamefanya walichoweza. Wamefanya walichoweza.

Tunahitaji akina James Cameron, Peter Jackson, George Lucas, Gore Verbinski, Tim Burton, Mel Gibson, J. R. R. Tolkien, Lewis Carol, Bishop Hiluka, Hermie Rajab (alale peponi) etc wengi zaidi Tanzania kuliko tunavyowahitaji akina Nicholas Cage, Denzel Washington (The Boss wa JF!), Johnny Depp.

Tunahitaji wababe wa kompyuta watusaidie katika kuboresha sinema zetu. Tuchukizwe na viwango vidogo vya sinema zetu halafu tuchukue hatua za vitendo za kuleta mapinduzi.

mkuu nimekupata
actually nina mipango ya kuinvest pande hizo in the future
 
Napenda kibwagizo cha etv africa '',,,,,,,,Nigeria movies are made out of shoe string budget of $5000!!!cjui siku wakirate zetu watasema $1500!!!!sasa unategemea utaipenda vipi muvi ya $1200 wakati umezoea kuona muvi za $ 26,000,000!!!!!!
 
Naona mzuka kwa watu unaongezeka

kuhusu hizi filam za bongo.....kwenye media na watu..

Sasa mimi najiuliza.kwa nini nashindwa kuzipenda hizi
filam za bongo????

Yaani nashindwa hata kutazama dakika ishirini tu ya filam hizi...

Pongezi. Ni lazima kabisa kuwa wewe una akili timamu. mtu mwenye akili timamu hawezi kabisa kuangalia huo uchafu!
 
Upo ugonjwa wa watanzania kutokupenda 'made in tanzania'.Ugonjwa huu mbaya unaitwa "ukuvyata"- Ukosefu wa Kupenda vya Tanzania" Ugonjwa huu umedumaza sana uchumi wetu.

si kweli. hapa kila kukicha tunawasifu wasanii wa nyumbani wa uhakika.
tunawapenda kina Gurumo, Bitchuka, Dede, Marijani, mzee jongo na akina Julius. Nyaisanga.
Hizi muvi za akina Kanumba ni uchafu. insults to our intelligence
 
Miye nawacwac na uwezo wa akir wa watu weng..maana hata kwenye ukwel wao wanabisha tu..kusoma hawajui hata picha..standrd za filamu kwel hatuzijui?au jst tulumbane tu bila hata kutoka na tunachotakiwa kufanya..shame on...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom