Nashindwa kumwelewa huyu dada

smati

Senior Member
Dec 24, 2010
149
5
Jamani ni miezi michache iliyopita nilimwomba dada mmoja uhusiano na nilimpenda kweli. Akaanza malingo mara hapokei simu , mara majibu mkato etc. nilileta hapa jamvini watu wakasema hiyo ni dalili za kupigwa kibuti. siku moja nikamweleza ukweli kuwa kwanini anaifanyia hivyo. akaniambia yeye amesha pendwa . mikamwuliza kweli inatoka moyoni akasema kabisakabisa sinampango na wewe.
nikampigia siku ya pili kumjulia hali akaniambia analala kwa sababau tuu anahoma. nikampigia siku nyingine tena akaniambi hajeenda hata kanisani eti hajisikii vizuri. nikamwuliza isije ikawa umefanya maaumuzi yasiyo sahihi akanihakikishia homa yake haihusiani kabisa na uhusiano wetu.

Nikampigia tena siku nyingine hakupokea, nikajua kweli hapa sina changu.

Nikakaa kama siku ishirini akapiga simu eti kunisalimia. nikamwuliza hujambo , akaniambia ati bado anahoma na amekuwa na homa kwa muda mrefu toka anipige kibuti. baadaye akanieleza ukweli kuwa ni kwa sababu nilikuwa simpigii simu.

Nikamwuliza shemeji yangu aliye kupenda hajambo, ananiambia eti tumeachana na hayupo kabisa. na haraka akaniuliza kama nimesha pata mchumba??.

Nimeendelea naye lakini nakuta kama huu ni utoto. Nimfanyaje maana anaonyesha kunipenda lakini hataki nijue kuwa ananipenda.
msaada wenu wakuu maana simwelewi ,wanaojua kusoma mambo nielezeni.
asanteni.
 
Usimweke akilini,atakupasua kichwa,mchukulie poa tu,akipugia poa akiacha poa yani usimfikirie kabisa,jali mambo yako!Mabinti bwana yani hawajijui kabisa!
 
Samahani kusema
Lakini anakuchezea tu...
Anang'ata huko nyama ikiwa
Ngumu anarudi kwako...
 
Mkuu, huyo msichana usiruhusu achezee akili yako kiasi hiko.
Wengine tumepitia majaribu kama hayo.

Cha kufanya ni uumpe muda afanye maamuzi magumu. Kama anapenda kuwa na wewe atamke wazi, vinginevyo apotee kabisa.. Mpe condition tu, kama anafikiri anakuhitaji basi aseme kwa uwazi kabisa.

Usipoangalia utapoteza muda. amka kijana.. wasichana wako wengi tu.. unajua hata kama unampenda mtu, huwezi kumlazimisha yeye akupende. Kuwa mkali na mwenye msimamo kabisa ili yeye asuke au anyoe, muendelee na maisha mengine.
 
mkuu, huyo msichana usiruhusu achezee akili yako kiasi hiko.
Wengine tumepitia majaribu kama hayo.

Cha kufanya ni uumpe muda afanye maamuzi magumu. Kama anapenda kuwa na wewe atamke wazi, vinginevyo apotee kabisa.. Mpe condition tu, kama anafikiri anakuhitaji basi aseme kwa uwazi kabisa.

Usipoangalia utapoteza muda. Amka kijana.. Wasichana wako wengi tu.. Unajua hata kama unampenda mtu, huwezi kumlazimisha yeye akupende. Kuwa mkali na mwenye msimamo kabisa ili yeye asuke au anyoe, muendelee na maisha mengine.

i like this, maana sijajua inawezekana aliyesema amempenda kampiga kibuti na kwa kumwonyesha kuwa na yeye ni mkali basi karudi kutafuta koloni lake. Mimi sinaye tena akilini, siwezi tena kumwambia nampenda na sijafanya hivyo toka anitamkie kuwa amesha pendwa. Halafu kama yupo serious kweli angeniomba hata msamaha , na kutambua kosa lake, lakini amenyamaza tuu just taking me for granted. Nonononononono, it cant work like this ladies.
 
mkuu huyo unampenda zaidi ya yeye anavyokupenda.
Tafuta akupendae...

na yeye anajua, kuna siku alisha niambia, ninamvyo mpenda, na jinsi ninavyo mtreat vizuri haijawahi tokea. Ila tuu hataki kutoa jibu . Lakini pamoja na hayo kwanini hana msimamo. Labda kina dada nisaidieni hapa.
 
mkuu..nisaidie umri wako na wake binti?.. maana kama ni utoto wa binti nahisi na wewe ni mtoto mwenzie...am sorry to say so... Pia nijuze mustakabalii wa mahusiano yenu "ulishawahi kumvua chu@#&pi? maana inawezekana uli-"under-perform" plus binti ana-kibwana chake cha pembeni kina performance ya kutosha anakuwa anakosa jibu sahihi la awe na nani kati yenu nyie vidume viwili...pia mkuu mbona haya mambo ni madogo sana...kama anakuzingua kamata binti nyingine kali piga gemu na endelea na maisha afterall ratio ya sasa kwa dunia nai 1man to 4 women..kazi ni kwako..pata uwezo na ubunifu zaidi toka VODACOM
 
sijawahi mkuu ???
 
Jamani ni miezi michache iliyopita nilimwomba dada mmoja uhusiano na nilimpenda kweli. Akaanza malingo mara hapokei simu , mara majibu mkato etc. nilileta hapa jamvini watu wakasema hiyo ni dalili za kupigwa kibuti. siku moja nikamweleza ukweli kuwa kwanini anaifanyia hivyo. akaniambia yeye amesha pendwa . mikamwuliza kweli inatoka moyoni akasema kabisakabisa sinampango na wewe.
nikampigia siku ya pili kumjulia hali akaniambia analala kwa sababau tuu anahoma. nikampigia siku nyingine tena akaniambi hajeenda hata kanisani eti hajisikii vizuri. nikamwuliza isije ikawa umefanya maaumuzi yasiyo sahihi akanihakikishia homa yake haihusiani kabisa na uhusiano wetu.

Nikampigia tena siku nyingine hakupokea, nikajua kweli hapa sina changu.

Nikakaa kama siku ishirini akapiga simu eti kunisalimia. nikamwuliza hujambo , akaniambia ati bado anahoma na amekuwa na homa kwa muda mrefu toka anipige kibuti. baadaye akanieleza ukweli kuwa ni kwa sababu nilikuwa simpigii simu.

Nikamwuliza shemeji yangu aliye kupenda hajambo, ananiambia eti tumeachana na hayupo kabisa. na haraka akaniuliza kama nimesha pata mchumba??.

Nimeendelea naye lakini nakuta kama huu ni utoto. Nimfanyaje maana anaonyesha kunipenda lakini hataki nijue kuwa ananipenda.
msaada wenu wakuu maana simwelewi ,wanaojua kusoma mambo nielezeni.
asanteni.

Anakufaa sana huyo. Hawa wasichana wa maharage ya Mbeya siyo ishu. Mwanamke lazima awe na msimamo bwana. Mambo ya kutongozwa leo kesho ameshavua chupi siyo ishu!

As long as hajawahi kukuomba omba hela, yaani taking advantage of you basi anakufaa huyo. Take my words!
 
dawa yake tafuta kifaa cha kufa mtu
hakikisha anakiona,
akikuuliza we sema just friends
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom