Nashindwa kumshauri rafiki

Kalumbesa

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,013
356
Kuna rafiki yangu mpenzi ameoa mwanzoni mwa mwaka jana...ni kipindi kirefu sasa amekuwa akiniomba ushauri juu ya mambo kadhaa kwani nami pia nimeoa...ameniambia amekuwa akivumilia sana katika ndoa yake ila kuna wakati huwa anakuwa karibu kufanya mambo ya ajabu kulingana na yale mwenza wake anayotaka...Anadai mke wake anapenda kuwa ana mcontrol ama kuwa na maamuzi juu ya mambo anayotaka kuyafanya...kwa mfano kama anataka kwenda mahali ama kuonana na marafiki zake au kwenda kufanya mazoezi mke wake huwa anakuwa against ama anakataa yeye kwenda kama hakumwambia muda mrefu kabla...yaani anapaswa kuwa alishamueleza mapema...huwa anajaribu kumweleza kuna ubaya gani nikienda kwenye mazoezi?lakini wapi mke huwa mbogo na kutoafiki yeye kwenda..wakati mwingine huwa anampuuza na kwenda ila ndiyo hivyo tena akirudi nyumbani kunawaka moto.ila hujifanya mjinga kuepusha shari...Na pia hata akipigiwa simu na rafiki waonane mke huwa mgumu kukubali hata kama rafiki yule naye anamfahamu..mke anaonekana kutokupenda mume aende mahali peke yake....Jamaa ananiuliza nifanye nini?mke wako anafanya hivi?napata tabu kumjibu maana nahofia kuwa m baya maana nachoweza kuongea kinaweza kumfanya akaharibu ndoa yake ama akanichukia mimi kama nitakuwa upande wa mkewe..nalazimika kumkwepa anapotaka kuniona kwa hili...Wadau nakaribisha mawazo yenu!hasa kwa wenye committed relationship au ndoa..kama bachelors chukulieni kama tatizo la mtu wa karibu siyo kujibu kirahisi kama vile, mwambie amuache...nk..Karibuni!!
 
Mwambie rafiki yako awe mwanaume.......

Ikibidi aongeze mke full stop......
 
Kawaida sana kwa newly married couples. Ajitahidi kwenda nae kokote aendako. Wakishapata mtoto majukumu yakazidi ndani mwenyewe atabwaga manyanga. Kama ni mazoezini basi amnunulie bukta waongozane. Kama ni baa the same; kwani kuna siri gani ambazo wife hatakiwi kusikia toka kwa friends wa bwana.

Mimi nakumbuka when I was dating my hubby tulikuwa tunatoka wote kila anapokwenda including kwenye bar na wakati nilikuwa sinywi. These days I have a lot to do siwezi kumpa company kila aendako.

But that is love. Mwambie achukulie positively unless he is not proud to be in her company. Na asijaribu ku compare ndoa yake na za watu wengine. Kama nilivyosema wengine wameshakaa na wake zao muda na wake zao wana watoto hivyo hawana muda wa kutoka. Na kila nyumba na formular yake; akitaka ndoa aione chungu basi aendelee kufanya comparison!
 
Mwambie rafiki yako awe mwanaume.......

Ikibidi aongeze mke full stop......

Huyo mke mmoja kizungumkuti, wawili si atapata heart attack:))

Awe mwanaume kwa kuongea na mke wake A,B and C..labda huyo mkewe anataka wawe wanatoka wote..Hebu amuelewe mkewe!!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Mwambie rafiki yako awe mwanaume.......

Ikibidi aongeze mke full stop......

Kaka una maanisha ampuuze ? akiongeza mke si inaweza kuwa soo maana huyo mke anaweza kuwa na matatizo yake pia....any way naogopa kumpa ushauri kama huu maana baadaye anaweza kunigeuka na mimi..nimejaribu kufikiiri sana naweza kumshauri vipi ili nisije haribu ndoa yake ila kwa anavyonieleza inaonekana mke anataka kumweka chini mshikaji...
 
Kuna rafiki yangu mpenzi ameoa mwanzoni mwa mwaka jana...ni kipindi kirefu sasa amekuwa akiniomba ushauri juu ya mambo kadhaa kwani nami pia nimeoa...ameniambia amekuwa akivumilia sana katika ndoa yake ila kuna wakati huwa anakuwa karibu kufanya mambo ya ajabu kulingana na yale mwenza wake anayotaka...Anadai mke wake anapenda kuwa ana mcontrol ama kuwa na maamuzi juu ya mambo anayotaka kuyafanya...kwa mfano kama anataka kwenda mahali ama kuonana na marafiki zake au kwenda kufanya mazoezi mke wake huwa anakuwa against ama anakataa yeye kwenda kama hakumwambia muda mrefu kabla...yaani anapaswa kuwa alishamueleza mapema...huwa anajaribu kumweleza kuna ubaya gani nikienda kwenye mazoezi?lakini wapi mke huwa mbogo na kutoafiki yeye kwenda..wakati mwingine huwa anampuuza na kwenda ila ndiyo hivyo tena akirudi nyumbani kunawaka moto.ila hujifanya mjinga kuepusha shari...Na pia hata akipigiwa simu na rafiki waonane mke huwa mgumu kukubali hata kama rafiki yule naye anamfahamu..mke anaonekana kutokupenda mume aende mahali peke yake....Jamaa ananiuliza nifanye nini?mke wako anafanya hivi?napata tabu kumjibu maana nahofia kuwa m baya maana nachoweza kuongea kinaweza kumfanya akaharibu ndoa yake ama akanichukia mimi kama nitakuwa upande wa mkewe..nalazimika kumkwepa anapotaka kuniona kwa hili...Wadau nakaribisha mawazo yenu!hasa kwa wenye committed relationship au ndoa..kama bachelors chukulieni kama tatizo la mtu wa karibu siyo kujibu kirahisi kama vile, mwambie amuache...nk..Karibuni!!

...aaahhh, mwambie huyo rafiki yako afuate matakwa ya mkewe bana, mbona sio magumu ki hivyo?

Kuna shida ganikumwelezea mwenzake well in advance mipangilio yake ya siku, wiki hata mwezi?
Mke nae anamipango yake kwake.
Ndio Ndoa hiyo, au yeye atajiskiaje mkewe akiwa anakurupuka kama yeye?

Hilo la kukuuliza mkeo anayafanya hayo, sio busara. "Kila mtu na Mtu'we!"
Anastahiki kuzifanyia kazi taratibu za nyumbani kwake iwapo anatamani maisha ya furaha, amani na utulivu.
 
nahisi huyo dada alishawahi kujeruhiwa ndio maana anakaa kimachale machale....mwambie aongee naye her past relationship au malezi yake aliyokulia labda alimuona baba anacheat katika hizo sehemu.......................anachotakiwa kufanya ni kumshirikisha mkewe kila sehemu anayokwenda waende wote,akishindwa kwenda wote awe anampigia simu mara kwa mara akiwa na rafiki zake,kumtumia message za anampenda ammemiss,na kurudi nyumbani on time bila kulewa chakari hii itampa huyo dada assurance.....
 
Kawaida sana kwa newly married couples. Ajitahidi kwenda nae kokote aendako. Wakishapata mtoto majukumu yakazidi ndani mwenyewe atabwaga manyanga. Kama ni mazoezini basi amnunulie bukta waongozane. Kama ni baa the same; kwani kuna siri gani ambazo wife hatakiwi kusikia toka kwa friends wa bwana.

Mimi nakumbuka when I was dating my hubby tulikuwa tunatoka wote kila anapokwenda including kwenye bar na wakati nilikuwa sinywi. These days I have a lot to do siwezi kumpa company kila aendako.

But that is love. Mwambie achukulie positively unless he is not proud to be in her company. Na asijaribu ku compare ndoa yake na za watu wengine. Kama nilivyosema wengine wameshakaa na wake zao muda na wake zao wana watoto hivyo hawana muda wa kutoka. Na kila nyumba na formular yake; akitaka ndoa aione chungu basi aendelee kufanya comparison!

Huu ushauri mzuri...na ndio maana akiniuliza wewe mke wako yuko hivi huwa namwambia naye ana mambo yake bila kutoa comparison na mkewe...asante kwa ushauri mzuri
 
Kuna wanawake wengine mkiwa kwenye ndoa hawaendi nje ya geti,but kwa mwanamke ambaye anapenda kukutana na rafiki zake bila shaka atamwelewa jamaa
 
...aaahhh, mwambie huyo rafiki yako afuate matakwa ya mkewe bana, mbona sio magumu ki hivyo?

kuna shida ganikumwelezea mwenzake well in advance mipangilio yake ya siku, wiki hata mwezi?
mke nae anamipango yake kwake.
ndio ndoa hiyo, au yeye atajiskiaje mkewe akiwa anakurupuka kama yeye?

hilo la kukuuliza mkeo anayafanya hayo, sio busara. "kila mtu na mtu'we!"
anastahiki kuzifanyia kazi taratibu za nyumbani kwake iwapo anatamani maisha ya furaha, amani na utulivu.

wanasema there is no wrong for a man to be fool in love with his wife......
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
kaka una maanisha ampuuze ? Akiongeza mke si inaweza kuwa soo maana huyo mke anaweza kuwa na matatizo yake pia....any way naogopa kumpa ushauri kama huu maana baadaye anaweza kunigeuka na mimi..nimejaribu kufikiiri sana naweza kumshauri vipi ili nisije haribu ndoa yake ila kwa anavyonieleza inaonekana mke anataka kumweka chini mshikaji...

dawa ya mwanamke anae kuhisi una mwingine pembeni ni kumtafutia
huyo mwingine na ikibidi uwatambulishe.........

I mean nachukia kuhisiwa mwizi wakati siibi,bora niibe na ijulikane naaiba.
Full stop...
In this case sio kuiba but kuchukua....
 
...aaahhh, mwambie huyo rafiki yako afuate matakwa ya mkewe bana, mbona sio magumu ki hivyo?

Kuna shida ganikumwelezea mwenzake well in advance mipangilio yake ya siku, wiki hata mwezi?
Mke nae anamipango yake kwake.
Ndio Ndoa hiyo, au yeye atajiskiaje mkewe akiwa anakurupuka kama yeye?

Hilo la kukuuliza mkeo anayafanya hayo, sio busara. "Kila mtu na Mtu'we!"
Anastahiki kuzifanyia kazi taratibu za nyumbani kwake iwapo anatamani maisha ya furaha, amani na utulivu.

Ni sahihi kabisa unavyosema...ila tatizo jamaa ananipa mifano kwamba sometimes mkewe hujisahau na kufanya mambo fulani bila hata kumjulisha yeye in advance...kwa mfano anaweza kutoka ofisini jumamosi(nusu siku) akapitia kusuka bila kumweleza yeye in advance akimpigia anamwambia nimepitia kusuka..sasa anashangaa kwa nini yeye akimuaga mbele yake anamwambia mbona haukunieleza toka awali?
 
Kuna wanawake wengine mkiwa kwenye ndoa hawaendi nje ya geti,but kwa mwanamke ambaye anapenda kukutana na rafiki zake bila shaka atamwelewa jamaa

na ni kweli ..mke wa jamaa si mtu wa kutoka toka ki hivyo ni kazini/home/kanisani na safari nyingine wanazokwenda pamoja kwa ndugu na jamaa..i mean si mtu wa
 
ni sahihi kabisa unavyosema...ila tatizo jamaa ananipa mifano kwamba sometimes mkewe hujisahau na kufanya mambo fulani bila hata kumjulisha yeye in advance...kwa mfano anaweza kutoka ofisini jumamosi(nusu siku) akapitia kusuka bila kumweleza yeye in advance akimpigia anamwambia nimepitia kusuka..sasa anashangaa kwa nini yeye akimuaga mbele yake anamwambia mbona haukunieleza toka awali?

huyo mke kamzidi jamaa ujanja
na jamaa kashakuwa mume *****....
 
chapa makofi tu tupa kule,kaoa kaolewa?cku hz wanawake wanataka kujipima mabav mpaka na waume zao,kama hyo yeye ndo anataka awe msemaj mkuu wa kila kitu wakat kaolewa tu ,kama nataka kwnda mahal namuaga mke wngu bt hawez kunizuia or question me further..smtimes u have to do it the hard way binadamu wngine mpk wapelekwe kwa force,atumie nafac yake kama mkuu wa familia kufanya mambo yke as long as sio mabaya.
 
nahisi huyo dada alishawahi kujeruhiwa ndio maana anakaa kimachale machale....mwambie aongee naye her past relationship au malezi yake aliyokulia labda alimuona baba anacheat katika hizo sehemu.......................anachotakiwa kufanya ni kumshirikisha mkewe kila sehemu anayokwenda waende wote,akishindwa kwenda wote awe anampigia simu mara kwa mara akiwa na rafiki zake,kumtumia message za anampenda ammemiss,na kurudi nyumbani on time bila kulewa chakari hii itampa huyo dada assurance.....

Ya kweli..ila inakuwa ngumu mke kwenda naye football ground yaani yeye aingie uwanjani mke awe anamcheki..mara nyingi kama mke amekataa kwa madai kwamba hakumwambia mapema hata akimwambia twende wote huwa hataki..na anamwambia kama mimi ni mkeo hautaenda...ila kama mimi ni mkeo unapaswa kunisikiliza
 
Si wote wenye hiyo tabia kuwa wanahisi jamaa cheater. Kuna sababu nyingi ambazo si mbaya. Mfano anaweza kuwa anania ya kumprotect mumewe maana kitaani si shwari na wote tunalikubali hilo. Na pili tunajua kuwa men are vulnurable when it comes to seduction!

Kwa hiyo mtu asijione kidume kama mkewe amuulizi anaenda wapi. Yawezekana na wife ana kidumu kwa hiyo hana sababu ya kukulinda wakati mwenyewe hajilindi!

Don't you guys feel loved when your wives care what you do?

dawa ya mwanamke anae kuhisi una mwingine pembeni ni kumtafutia
huyo mwingine na ikibidi uwatambulishe.........

I mean nachukia kuhisiwa mwizi wakati siibi,bora niibe na ijulikane naaiba.
Full stop...
In this case sio kuiba but kuchukua....
 
huyo mke kamzidi jamaa ujanja
na jamaa kashakuwa mume *****....

Ya kweli hata mimi naona dalili hizo...tatizo ukimshauri jamaa vibaya anaweza kwenda home aka force mambo na kumchapa ngumi wife ndoa ikaishia kuwa maafa...
 
Great Thinker you seem to know too much about this family. You have all answers as if you were there!

Ya kweli..ila inakuwa ngumu mke kwenda naye football ground yaani yeye aingie uwanjani mke awe anamcheki..mara nyingi kama mke amekataa kwa madai kwamba hakumwambia mapema hata akimwambia twende wote huwa hataki..na anamwambia kama mimi ni mkeo hautaenda...ila kama mimi ni mkeo unapaswa kunisikiliza
 
Ya kweli..ila inakuwa ngumu mke kwenda naye football ground yaani yeye aingie uwanjani mke awe anamcheki..mara nyingi kama mke amekataa kwa madai kwamba hakumwambia mapema hata akimwambia twende wote huwa hataki..na anamwambia kama mimi ni mkeo hautaenda...ila kama mimi ni mkeo unapaswa kunisikiliza

huyo basi ana gubu tu amuignore.....................................
 
Back
Top Bottom