Nashindwa kumsahau mchumba wa mtu!!

Pindima

JF-Expert Member
Aug 16, 2011
347
81
Tulikua wapenzi kwa muda mrefu ila kulitokea kutokuelewana kwenye mwezi wa 2, kwa kushindikizwa na familia yake wakaamua kukubali posa ya mtu mwengine! Ila sasa mapenz yamerudi tena kwa kasi kubwa mimi kumuoa siwezi kwasasa kwasababu maisha hayaruhusu!! Sasa tatizo tunajiona ni wakosaji kwa mungu na kwa huyo mchumba wake,kiukweli tumeamua tuwe marafiki tu lkn mioyo haikubali!! Tafadhalini tupeni ushauri wa kusahauliana kwan tuyatendayo si haki!!
 
mhh iyo kali
ninkinakwamisha wewe usimuoe sasa?
pesa?ndoa si pesa una za MATEMBELE NA DAGAA fanyakweli....KUMCHUNGULIAMCHUMBA WAMTU SI VYEMA
 
Hali hairuhusu kwa nini??

Kama umeshajua hali hairuhusu kwa nini wewe unaruhusu?

Ila hata kuwa mshika mapembe kuna raha yake.
 
mhh iyo kali
ninkinakwamisha wewe usimuoe sasa?
pesa?ndoa si pesa una za MATEMBELE NA DAGAA fanyakweli....KUMCHUNGULIAMCHUMBA WAMTU SI VYEMA

Tatizo ni nimemaliza masomo juzi tu na bado sijabahatika kupata kazi na sitaki kulelewa mimi na mke wangu!
 
Hali hairuhusu kwa nini??

Kama umeshajua hali hairuhusu kwa nini wewe unaruhusu?

Ila hata kuwa mshika mapembe kuna raha yake.

Hizo raha zisije nitokea puani!! tumejaribu kutokuwasiliana lakin tatizo ndio linaongezeka!!
 
Hakuna tatizo lolote hapo,unajimix tu mwenyewe.kama unamalengo nae kaa nae uongee nae.kama ataweza kukusubiri mpaka utakapo jipanga.kama hawezi..tel her to go kwa mtu wake.Usipende kuwa mshika pembe.naamin mwanamke akikupenda,atakusubiri tu.no matter what.
 
Msipotezeane time please, mlishajaribu haikuwezekana. Avunje uchumba ili na hauko tayari....haikuwa yako hiyo...tafuta dungayembe mwengine.
 
Kwa kweli huyo binti aliamua, hata kama kashinikizwa bado aliamua kuwa na huyo mchumba...
Hizo feeling mnazoziendekeza huja na kuondoka jamani mbona hili somo gumu kueleweka?
Upendo huamua na kushikilia maamuzi no matter what! We kamtafute wa kukubali kulishwa dagaa(huyo atakuwa kakupenda hasa). Umwachie mchumba mwenye maamuzi apate mke
 
Haujamaanisha unachokisema kuwa unaona kufanya hvyo ni kumkosea Mungu..
Ukiwa tayari na kumaanisha kuwa hautaki kuwa na mahusiano ya kingono na huyo binti,nistue..
 
hii kazi kweli ila tujaribu kwanza kumwelewa.....

Kaka nahis wewe unaweza kunielewa!! hapa tatizo ni moyo hautaki kukubali matokeo!! tumejaribu kutokuwasiliana ila imeshindikana!! sasa tufanye nn?!!
 
Tatizo ni nimemaliza masomo juzi tu na bado sijabahatika kupata kazi na sitaki kulelewa mimi na mke wangu!
Subiri upate kazi na kipato.., (na uwezo wa kumlea yeye na familia yako), baada ya hapo fuateni process za talaka ili muweze kuwa wapenzi wa kweli mbele ya jamii na sheria na sio wezi (sababu mkishikwa utapelekea rafiki yako kufukuzwa, kupewa talaka na kupata aibu, mbele ya jamii)
 
Kaka nahis wewe unaweza kunielewa!! hapa tatizo ni moyo hautaki kukubali matokeo!! tumejaribu kutokuwasiliana ila imeshindikana!! sasa tufanye nn?!!
Ni hatua zipi ulizotumia ili kuhakikisha kuwa imeshindikana?Naona pengine njia unazotumia ni sawa na story za sizitaki mbichi hizi.
 
Asante kwa ushauri!!
 
Kama bado wote mnapendana na hawajaoana then what are you waiting for? Pambana, ila lazima ufikirie kwa nini mligombana na mmerekebishaje is it permanent? As long as hajaolewa na anakupenda, narudia tenaa, anakupenda Sio wewe walazimisha, mchangamkie.

QUOTE=Pindima;3712377]Tulikua wapenzi kwa muda mrefu ila kulitokea kutokuelewana kwenye mwezi wa 2, kwa kushindikizwa na familia yake wakaamua kukubali posa ya mtu mwengine! Ila sasa mapenz yamerudi tena kwa kasi kubwa mimi kumuoa siwezi kwasasa kwasababu maisha hayaruhusu!! Sasa tatizo tunajiona ni wakosaji kwa mungu na kwa huyo mchumba wake,kiukweli tumeamua tuwe marafiki tu lkn mioyo haikubali!! Tafadhalini tupeni ushauri wa kusahauliana kwan tuyatendayo si haki!![/QUOTE]
 
Ni hatua zipi ulizotumia ili kuhakikisha kuwa imeshindikana?Naona pengine njia unazotumia ni sawa na story za sizitaki mbichi hizi.

Hatua nilochukua (1) kukata mawasiliano. (2) kukaa nae mbali ( 3) kutokutaka kisikia chochote kinachomuhusu yeye!!
na yeye ameyafanya yote hayo ila mwisho wa siku ndio kujiongezea maumiwu!!
 
Hivi ni mchumba au ni mke tayari kama ni mchumba basi inabidi ufanye hima na kuongea na wazazi na familia ili huyo mchumba asije geuka kuwa mume..

In short hapa una muda mfupi sana (kwahio usingoje hadi upate kazi, nenda hata kopa posa, kazi utapata baadae) sababu akishaolewa huenda mwana asiwe wako tena
 
Hatua nilochukua (1) kukata mawasiliano. (2) kukaa nae mbali ( 3) kutokutaka kisikia chochote kinachomuhusu yeye!!
na yeye ameyafanya yote hayo ila mwisho wa siku ndio kujiongezea maumiwu!!

Ok, kwani wazazi wake waliweka pingamizi gani kwako? Kama litakuwa la wewe kuwa mwanafunzi na wao walitaka pedeshee ndo aoe binti yao basi pingamizi hilo halina mashiko, linaweza kuvunjwa. Ila nawe unatakiwa kuwa serious isije kuwa unamhitaji kumtumia tu na kumkosesha mume wake wa ukwe-ee!
 
Kaka nahis wewe unaweza kunielewa!! hapa tatizo ni moyo hautaki kukubali matokeo!! tumejaribu kutokuwasiliana ila imeshindikana!! sasa tufanye nn?!!

Habari yako kwanza!!

Kaka hayo ni majaribu tu ya Shetani. Hakuna kisichowezekana kama kweli una nia ya dhati, inabidi ujue kuwa huyo sio wako ni mchumba wa mtu tayari na achana na habari za kuusingizia moyo.
Inatakiwa maamuzi yako yashinde tamaa hapo ndipo utafanikisha hilo lengo la kuachana vinginevyo mtandelea tu. Ebu jiulize kama huyo jamaa ndo angekuwa wewe halafu yeye ndo angekuwa anakumegea demu wako, how cud u feel?

Mnapotezeana muda tu, kwanini usingetumia muda huu kutafuta wako wa kweli ambaye mtakuwa free kufanya mambo yenu maana hofu yangu ni siku jamaa atakapogundua halafu na yeye akukamate akukamue, utalalamika?
Achana na huyo dmu mkuu. HUU NI USHAURI WANGU!!
 
Tatizo ni nimemaliza masomo juzi tu na bado sijabahatika kupata kazi na sitaki kulelewa mimi na mke wangu!
Nshawahi kaa kitaa miaka mbili nahenyea kibarua. Muda wote huo nlikuwa nakula ugali wa wife. Sijawahi kujuta na sitokaa nisahau. Kwenye penzi la dhati, haijalishi nani ni bread winner. Fuata moyo wako kijana, usijitese kisa Pesa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom