Nasema hivi! Siogopi mtu yeyote yule ktk hilii vyovyote iwavyo.

ibra919

Member
Apr 16, 2012
23
6
Ndio siogopi mtu hasa ktk swala ninalo ona linalenga kuninyima haki yangu kama mtanganyika hata kama nimezaliwa ndani ya inayo itwa Tanzani.Ngoja niwaambieni ndugu zangu wana wa JF mimi nimebahatika kuiona katiba ya nchi yangu ya Tanganyika,Japo kwa mbinde lakini nimeipata na nafanya mpango wa kuiweka wazi ktk ukurasa wetu wa JF.Nilrudi kwenye hoja=:haiwezekani mtu mmoja anakaa nyumbani kwake au ofisini kwake na kutuamlia mambo gani tuyaseme na yapi tusiyaseme? inauma na inakera kujifanya wewe ndio mwenye hati miliki ya watanzani,naomba niseme kuwa mimi ni miongoni mwa WATANGANYIKA wanao dai TANGANYIKA yao, hivyo nawaomba watanganyika wenzangu tuungane kuidai Tanganyika yetu kumbukeni kuwa sheria ya nchi inatutaka tusizungumie MUUNGANO kwa nia ya kuuvunja ila kwa nia ya kuuboresha.
Sasa kama hivyo ndivyo njooni tuungane kudai Tanganyika yetu jukuumu hili tusiwaachie wana UAMSHO pekee walioko visiwani,kwani kukaa kimya kwetu kunaonyesha kuwa sisi tumeridhika na huu mungano wa upande mmoja.Hii itatufanya tuamue mstkabari wetu juuu ya maisha ya watoto na wajukuu wetu, kwa kuiambia tume ya katiba mpya kuwa tuna itaka Tanganyika kama ilivyo nzanzibar maana hatuwezi kuzungumzia katiba ya muungano wakati sisi katiba yetu imefukiwa ndani ya aridhi. TUAMKENI


NAOMBA KUWASILISHA
 
Mimi naitaka Kanda yangu tu. Tanganyika kwani ni mdudu gani ati.
 
nonsense,hata U.S.A ukizungumzia kuhusu zile states zigawanyike...ni uhaini(treason).....kiukweli tunataka muungano ulioje ndio mpango mzima...
 
Kama mmeelekezwa muandikeje katiba yenu nanyi mmekubali, basi mjue hiyo katiba si yenu bali ya aliyewaelekeza muiandike.

Ili uandike katiba umepaswa kuzingatia kwa awali kabisa kuwa unaanza kuandika kutokea ukurasa 0, na unaingia kwenye (chumba) mchakato wa kuandika hiyo katiba bila desa. Hutakiwi kukopi na kupest.

Nimeona mpiga chapa wa serikali ameanza kuyachapa manakala meeeengi ya katiba ya sasa ili kutengeneza masingira ya kudesa. Leo narudia kuwaambia wananchi wenzangu kuwa ikiwa katiba itaandikwa kwa mfumo wa sasa SIIKUBALI, NA NINAWAAGIZA WANANGU WAENDELEZE MCHAKATO WA KUIANDIKA KATIBA YAO HATA IKIGHARIMU MIAKA 100 KUFIKIA LENGO!!!!
 
nonsense,hata U.S.A ukizungumzia kuhusu zile states zigawanyike...ni uhaini(treason).....kiukweli tunataka muungano ulioje ndio mpango mzima...

Muungano uvunjike, usivunjike mi sijui. Nnachotaka ni Tanganyika yangu iliyokua huru desemba tisa 1961.
 
nimeshaamka niko macho meupeeeeeeeeeeeee tanganyika irudi mara moja kisha tuungane na zanzibar sisi tukiwa tanganyika mbona kuna muungano wa tanzania kenya uganda rwanda na burundi na tunaiita jumuia ya EA na hii ya tanganyika na zanzibar tuiite jumuia ya tanganyika na zanzibar kila mtu abaki na jina lake na dola yake
 
Mimi nataka East Africa federation wala sifikirii mkoa wa Zanzibar!!
 
nimeshaamka niko macho meupeeeeeeeeeeeee tanganyika irudi mara moja kisha tuungane na zanzibar sisi tukiwa tanganyika mbona kuna muungano wa tanzania kenya uganda rwanda na burundi na tunaiita jumuia ya EA na hii ya tanganyika na zanzibar tuiite jumuia ya tanganyika na zanzibar kila mtu abaki na jina lake na dola yake

Nalori gwa kumyitu...se se se....mweeee akana aka!!, kali na mahala fijo, Kyala akusajeghe
 
muungano uvunjike, usivunjike mi sijui. Nnachotaka ni tanganyika yangu iliyokua huru desemba tisa 1961.

iliyokuwa huru ni tanzania bara mkuu si tanganyika si huwa unaona wanavyosema kwenye sherehe za uhuru wa tanzania bara!??
 
Back
Top Bottom