Nasari kupoteza ubunge wake kama Lema

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,442
Tetesi za uhakika kutoka ndani ya CCM ni kwamba kuna timu ya watu Tisa(9) wamepewa kazi ya kutafuta na kukusanya ushahidi wa maneno machafu yaliyotumika wakati wa kampeni, ili ifunguliwe kesi kupinga ushindi wa Nasari kwa madai kwamba mpinzani wake alisingiziwa kwamba ni shoga ilihali si kweli hivyo kupoteza mvuto kwa wapiga kura.

My take. Kama alivyodai mwana CCM mmoja kwamba nia yao kubwa siyo kwamba wanataka uchaguzi urudiwe ili washinde, nia yao kubwa ukiachilia mbali kwamba wanasahaulisha CHADEMA kujipanga namna ya kupambana ipatikane Katiba mpya iliyo bora pia ni kukifanya CHADEMA kiwe busy na masuala ya kesi na kutumia rasilimalizao chache zilizopo kughalamia michakato ya chaguzi ndogo ili ifikapo mwaka 2015 wasiwe na resources za kutosha kukabiliana na CCM.
 
hamna kitu. CCM ndo inalikaribia kaburi.

Mkuu lakini hizo mbinu hata mimi naona zitasababisha CHADEMA isijipange vema ku-deal na mambo mengine mda mwingi itautumia kuhangaika masuala ya kesi za uchaguzi na chaguzi ndogo
 
CDM ni nguvu ya umma tutashinda tu kwa lolote, na bado moto utawaka wataachia ngazi wenyewe!!!
 
Mkuu lakini hizo mbinu hata mimi naona zitasababisha CHADEMA isijipange vema ku-deal na mambo mengine mda mwingi itautumia kuhangaika masuala ya kesi za uchaguzi na chaguzi ndogo

vise versa ni kwamba, wanapelekea CDM ku-buy trust kwa wapiga kura zaidi na zaidi.
Sasa kama wanawapotezea mda kwa kesi while tendo hilo linaongeza mtaji wa kura kwa CDM watakuwa wao ndo wanajipotezea muda na mtaji wa kura.
wanachokifanya CCM ni sawa na kukata tawi la mti walilolikalia wenyewe.
 
Hakuna mafanikio katika maji taka bali ni kuzidi kunuka. Gamba lenyewe limewashinda.

Kinachoniuzi ni maamuzi ya kuamua kukimoa chama bila kujari ghalama za uchaguzi hebu fikiria mabilioni yatakayotumika Arusha kumrudisha tena Lema Bungeni.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom