Nasari jana jioni kata ya maji ya Chai ktk Picha

Hao wamekuja kusikiliza porojo, wanajuwa kabisa kuwa chadema hawana sera ya kuitekeleza Arumeru, watatekeleza kipi wakati Serikali ni ya CCM?

Hapo sasa!
Kama wameshindwa kwa miaka 50, wataweza leo? Nassari Goo!
 
sera zilikuwa zinawaboa nini?m maana wote ukiwachek sura zao ni za huzuni kama vile wako msibani. mwalimu anayefanya wanafunzi wake wamuogope huyo hafai kuwa mwalim pia mgombea ambae wakati anamwaga sera zake anawafanya wananchi wawe kama vile matangani hafai kuwa kiongozi kwani haoneshi dalili za kuleta joy kwa wananchi. pole sana kijana mwenzangu

Sio zilikuwa zinawaboa ndugu,ni machungu jinsi nchi inavyoliwa na wachache halafu tunabaki maskini.
Hata ingekuwa wewe ungesikitika.Mimi binafsi nilihudhuria mkutano wake Jmosi iliyopita kijana ana sera
ambazo usipokuwa mvumilivu unaweza kulia.He is very smart than normal.
 
Hao wamekuja kusikiliza porojo, wanajuwa kabisa kuwa chadema hawana sera ya kuitekeleza Arumeru, watatekeleza kipi wakati Serikali ni ya CCM?

Hapo sasa!

Kaka/dada, watu siku hizi wanatembea bwana, maeneo mengi yenye wabunge wa Chadema yako vizuri zaidi kuliko amabyo CCM wana tawala, hebu twende pamoja tuone:-
  1. Musoma mjini, Mbunge ni bwana Vicenti Nyerere, kwasasa wazee wa Musoma kutibiwa sio tena issue kwao, wanatibiwa bure tena bila usumbufu, yaani wanaona tofauti ya Mbunge wa CCM na upinzani hasa Chadema.
  2. Kigoma kaskazini kwa bwana Zitto Kabwe, nenda kwenye vijiji vya Kalinzi, Mkigo manyovu n.k, vijana wamerudi Kijijini kwani kilimo cha kahawa na ndizi kimeanza kuwalipa, wana shida tena ya soko la kahawa yao wala ndizi zao, nauli walikuwa wana lipa Sh 700-10,000 kwenda huko but kwasasa ni Sh 2500-3000, hivyo wanaona tofauti ya mbunge wa CCM na Chadema.
  3. Kule Geita, tarafa ya pale mjini inaitwa Kalangalala, diwani wa chadema anafanya vitu mpaka unamkubali, aliye wahi kuwa diwani kwa miaka karibu 20 huyu wa CCM hakuwahi kufanya chochote, huyu kwa muda mfupi tu, nasikia alipewa TSh 36,000,000 za maendeleo, alifanya yafuatayo, maabara ya sekondari mbili zilizoshindikana alimaliza na kununua vifaa vyake, nyumba ya mwalimu mkuu ilishindikana aliimailza na yenyewe, aliweza kuwajengea soko zuri pamoja na ofisi, akiwa katika hatua za finishing, huyo aliyekuwa diwani alikwenda mahakani eti bwana Diwani amejenga kwenye Makaburi ya Waislam. Vibari vya ardhi vinaonessha kuwa diwani was right, ujenzi umesimama hadi sasa.
  4. Kule Tarime enzi hizo Chadema ikiwa madarakani, watoto wote wa sekondari walikuwa wanasoma bure, nenda kaulize sasa hivi, ndo maana bwana Nyambli Nyangwine wala hathubutu kurudi huko mara kwa mara tena.


So issue hapa sio kuwa madakani, zipo pesa nyingi tu kwenye halmashauri za wilaya ambazo Mbunge pamoja na baraza la madiwani endapo wata kuwa na Vision na wakaacha ufisadi walau kwa asilimia 50% tu mabo yatakuwa mazuri, Kupenda CCM ni kuichukia Tanzania na vizazi vyake.
 
Kazi kwisha Arumeru jana wakitoka kwenye kampeni ccm walivamia msafara wa cdm kijana mmoja akaanza kukata watu mapanga cdm wakampa kichapo mno ndo polisi wakaja kumuokoa
 
View attachment 50270View attachment 50271View attachment 50272View attachment 50273

Jana jioni kamanda Joshua Nassari alimalizia mkutano wake wa sita kwa siku hiyo katika kata ay maji ya chai ambapo kama kawaida watu walisikika wakipiga ukunga pale walipokumbushwa machungu wanayokumbana nayo kila siku kwa miaka 50.
Pia alionyesha fimbo nyingine na mgorori aliyopewa nawazee wengine katika mikutano ya mapema jana ikiwa ni niishara ya kumkubali na kuwaongoza kama alivyo fanya Musa.


M4C​

Embu angalieni sura za hawa watu kwenye hizo picha. Yani ni za huzuni kubwa na zakuonyesha kukata tamaa ya maisha. Jamani wananchi wanahitaji maendeleo na kuondolewa kwenye janga la umaskini na matatizo mengine. Kazi kwenu wana Arumeru mchague nani alinde shamba la mahindi kati ya Nyani na Simba
 
sera zilikuwa zinawaboa nini?m maana wote ukiwachek sura zao ni za huzuni kama vile wako msibani. mwalimu anayefanya wanafunzi wake wamuogope huyo hafai kuwa mwalim pia mgombea ambae wakati anamwaga sera zake anawafanya wananchi wawe kama vile matangani hafai kuwa kiongozi kwani haoneshi dalili za kuleta joy kwa wananchi. pole sana kijana mwenzangu[Watakuaje na furha wakati wameelezwa chanzo cha shida zao, hivyo wanahasira na aliye wafanya wawe walivyo]
 
joy itatoka wapi mkuu wakati watu wameuzwa na waliopokea fedha hawawajali? we untaka kampeni za kuchekesha then ukirudu nyumbani huna chakula? tafakari rasilimali za wana arumeru zilivyo na maisha yao yalivyo?
 
Hao wamekuja kusikiliza porojo, wanajuwa kabisa kuwa chadema hawana sera ya kuitekeleza Arumeru, watatekeleza kipi wakati Serikali ni ya CCM?

Hapo sasa!

mimi si mfuasi wa itikadi za chama chochote cha siasa hapa tz.lakini kama mtanzania nimekua mfuatiliaji wa shughuli za kisiasa na sera mbalimbali hasa zinapotokea chaguzi kubwa na ndogo ndogo...
yote haya ni utekelezaji wa mfumo wa demokrasia,uhuru wa watu kuamua na kuchagua.
sasa huwa kwa kweli huwa nashindwa kuwaelewa CCM pale tu wapokuwa wakinadi wagombea wao ktk kampeni na kudai msimchague mgombea wa upinzani kwa kuwa serikali iliyopo madarakani ni ya CCM. hivi kwa nn basi tunasema tunafuata demokrasia na huku tunawaelekeza wananchi nani wa kumchagua na nani wa kumtosa? kwa nini kila chama kisinadi tu sera zake na kuacha maamuzi ya nani ashike hatamu kwa wananchi?...kumbuka wapiga kura si lazima wawe wafuasi wa vyama vya siasa.
nawakilisha.
 
Kinachonifurahisha kwenye mikutano ya CHADEMA ni aina ya wahudhuriaji. Wote ni watu wazima 18+ tofauti na kule kwa mahasimu wetu kisiasa. Kama Nasari akifanikiwa kuwashawishi wote waliopo mkutanoni kumpa kura, anakuwa amejihakikishia kupata kura za wote wanaokuja kumsikiliza. Tofauti na yule mwenzetu anayewahutubia watoto wa shule ambao hawapigi kura.

1_Sioi akisalimia wananchi kwenye mkuatno huo wa Ngarasero, Usa River.jpg

Good observation Lukolo, halafu hawa hapa hata ikifika 2020 wengi wao watakuwa bado hawajafikisha umri wa kupiga kura. Kumbe huyu jamaa ni mtaji mzuri kwenye shule zetu za awali (Kindergarten).
 
CCm wanajua walikwisha tengenza mazingira toka zamani kwa kuahakikisha elimu ya uraia haimfikii ktu yeyote! Elimu ya uraia ndiyo silaha pekee itakayowatoa hawa manyang'au madarakani! Watu hatuelewi kwa nini tupige kura! Mimi niao uhakika ipo siku CCM itaabishwa kama Mzee Wade wa Senegal!!! atu wanajipa license to rule!!
 
Hao wamekuja kusikiliza porojo, wanajuwa kabisa kuwa chadema hawana sera ya kuitekeleza Arumeru, watatekeleza kipi wakati Serikali ni ya CCM?

Hapo sasa!

Mentality yako siyo sahii, kwani kama serikali ni ya CCM ndio sababu mpinzani hawawezi kufanya changes?Kama uwelewa wetu wa mambo ni huu basi elimu ya uraia kwa wananchi wa taifa hili bado ni changa sana. Kama ulikuwa haujuhi ulichokuwa unasema ni kwamba tusiwe na viongozi wa jamii kutoka upinzani ktk nchii hii.Swali langu kwako ni kwamba mpaka leo bado haujaona faida ya kuwa na upinzani wenye nguvu ktk nchii hii?
 
all the best KAMANDA J.NASSARI

Karibu DOM karibu mjengoni

shughuli matatizo ya wananchi tulikwama,tulipora mali za walala hoi,ni wakati wa kufanya mabadiliko.
 
Big up Nassari Mungu wa Wahaya yuko paoja nawe tunakuombea usiku na mchana...........alichikituma Maji marefu kikamwangukie Nchemba.....
 
Hao wamekuja kusikiliza porojo, wanajuwa kabisa kuwa chadema hawana sera ya kuitekeleza Arumeru, watatekeleza kipi wakati Serikali ni ya CCM?

Hapo sasa!
Kwa hiyo wanafurahia CCM kuwaibia mashamba kama Dori Farm ambalo Mkuu Mkapa alisema atawarudishia????? Kwa vile Wameru umewaona ni wajinga wanafurahia CCM isiyo ongea porojo kuendeleza wizi wa wazi wazi wao waendelee kuwachagua, au vipi????

 
Back
Top Bottom