Elections 2010 Nasaha zangu kwa wapiga kura

Konaball

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
2,949
1,940
Sasa tupo mlangoni, tunaingia katika hatua ya mwisho ya uchaguzi nayo ni kupiga kura. Ni Jumapili Oktoba 31, mwaka huu. Wazanzibari wote waliowahi kujiandikisha na wanazo shahada zao watapiga kura kuchagua Madiwani, Wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Awali ya yote tunapenda kubainisha kwamba, kwa yeyote anayeshiriki katika uchaguzi huu - akiwa ni mpiga kura, au mgombea, au msimamizi: KURA ZA WANANCHI ZISICHEZEWE NA CHAGUO LA WANANCHI LAZIMA LIHESHIMIWE.

Hii ni mara ya nne Watanzania kushiriki katika uchaguzi chini ya mfumo wa vyama vingi vya siasa; awali ilikuwa mwaka 1995. Lakini safari hii wananchi wana ufahamu mpana zaidi wa ni nini mfumo wa vyama vingi na ni nini upinzani; wanafahamu kwamba mfumo wa chama kimoja cha siasa haikuwa ni amri ya Mwenyezi Mungu bali ilikuwa ni mapenzi ya watu.
Miaka mitano inayokamilika hivi sasa imewapa Watanzania fursa ya kuufahamu uwezo, udhaifu na bila shaka mustakabali wa chama tawala.

Leo Watanzania wanafahamu ni chama gani kilikuwa madarakani wakati wenzao zaidi wakifa na wengine kihangaika kwa njaa na ukosefu wa maji safi na salama.
Leo Watanzania wanafahamu ni serikali ya chama gani ilikuwa madarakani wakati Dada zao na Mama zao wakitumbukia katika biashara ya ngono kuuza miili yao (uchangu doa) ili wapate pesa ya kupata chakula chao.
Leo wananchi wanafahamu ni chama gani kilikuwa madarakani wakati Mama zao wakiangukia katika biashara za Mama ntilie ili kupata kipato cha kukidhi mahitaji yao ya kila siku na Vijana wakitumbukia katika ujambazi na unyangaji au umachinga.
Leo Mtanzania anaingia katika chumba cha kupigia kura akifahamu fika ni serikali ya chama gani ilikuwa madarakani wakati iliposhindwa kutumia jeshi la polisi kudhibiti uingiaji wa madawa ya kulevya na kudhibiti matumizi ya madawa hayo wakati maelfu ya vijana wanaathirika, lakini serikali hiyo hiyo haikawii kutumia jeshi la polisi kwenda kuwatawanya wananchi wanaohudhuria mikutano ya kampeni inayohutubiwa na viongozi wa vyama vya upinzani.
Leo Mtanzania anaingia kupiga kura akiwa na kumbukumbu 'mbichi' ya chama kilichotajika sana kwa ufisadi,rushwa na mizengwe ya kuhujuimana wao kwa wao na ubadhirifu wa pesa za wananchi kama pesa za Epa na Ufisadi wa Richmond.

Tunaamini kila mpiga kura, baada ya kujikumbusha haya, ataweza kuamua ikiwa atapiga kura yake kukirejesha chama tawala madarakani au ataipa nafasi kambi ya upinzani idhihirishe umahiri wake.
Lakini, kupambanua kati ya chama tawala na upinzani pekee hakutoshi; upambanuzi pia unatakiwa miongoni mwa vyama vilivyoko katika kambi ya upinzani.
Kwa mfano, "ni chama kipi kimetangaza ilani yake ya uchaguzi na sera inayolenga kumkomboa mwananchi; sera inayozungumzia bayana masuala elimu, afya na matibabu, ajira, uboreshaji wa kilimo na soko bora la mazao, mfumo bora wa kodi, vita dhidi ya rushwa na ubadhirifu serikalini, na uongozi bora".

Chama ambacho sera zake zina elekea kutekelezeka na wala sio chama ambacho kinaigia madarakani kwa mbwembwe halafu, miezi michache baadaye kinawatangazia wananchi eti, "ilani ya uchaguzi haitekelezeki".
Leo Watanzania wanafahamu ni kiongozi gani ameonesha mwelekeo wa kuheshimu na kudumisha umoja wa Watanzania kiasi kiongozi huyo akinadi sera zake huzungumza kuunda serikali iliyomakini na yenye kuleta tumaini jipya kwa Watanzania baada uchaguzi huu.

Baada ya ukumbusho huu tunaamini kila mpiga kura ataingia katika chumba cha kupigia kura akijua ni nani au ni chama gani akipige kura; ili apate tumaini jipya na maendeleo.
Baada ya kuongea na wananchi sasa tunarudi kwa chama tawala na pia Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Wawili hawa tunawakumbusha kwamba kura za wanachi ziheshimiwe, chaguo la wananchi liheshimiwe na Ubabe usikaribishwe nchini.
WATANZANIA WOTE MLIOJIANDIKISHA JITOKEZENI MKAPIGE KURA, NA BAADA YA HAPO MSISAHAU 'KUWA WATULIVU KATIKA SIKU YA KUPIGA KURA'
 
Back
Top Bottom