Napendekeza TZS 1000 kwa mtu mmoja ili Kivuko Cha Kigamboni kijiendeshe kwa faida!

Hayo ndo matatizo ya kula kwa baba mpaka umri huo ndo maana kichwa chako hakina tofauti na nazi,kichwa empty,kichwa maji,endelea tu na msingi wako wa shikamoo
 
Watu wanalishana upumbafu humu JF! hivi mnajua gharama za kuendesha kile kivuko kwa siku ni kiasi gani? kuna mafuta, kuwalipa walinzi wa aina tatu ( Security Guards, Suma JKT, Polisi wa Kawaida), wafanyakazi wa dirishani na wale wanaochana ticket. Hapo bado hujawalipa madereva, hujapitisha askari na wanajeshi bure, wachilia mbali ticket fake zinazoingizwa pale na wakubwa.
Sasa yote hayo ukiyaangalia inatoa picha ya kwamba TZS 200 haitoshi kabisa, napendekeza mtu mmoja bila kujali umri alipie TZS 1000. Kwa upande wa vyombo vyote vya moto viwango vianzie TZS5000 - TZ10,0000 ili kuisaidia serikali na wafanyakazi kuongeza mapato.

Twende taratibu mkuu. Pale Nansio port - Mwanza port, hakuna kivuko cha serikali kipindi hiki (labda kama wameanza tena jana). Nauli ilikuwa Tsh. 5,000/- early 2011 kwa kichwa. Lakini kufikia early dec 2011 hakuna meli hata moja ya serikali iliyoko majini ku ferry watanzania wenzetu eneo hilo. Kuna vivuko vya watu binafsi na nauli ni hiyohiyo na wana run biashara vizuri tu.
 
hebu tuwekee mahesabu sahihi, KUNA JUMLA YA WAFANYAKAZI WANGAPI? MATUMIZ MENGINE YANAGHARIM SH. NGAPI? KUNAVUKA WASTANI WA BINADAMU WANGAPI KWA SIKU? MAGARI MAKUBWA NA MADOGO YANAVUSHWA MANGAPI KWASIKU?
Mimi sijui kwa makadirio ni watu wangapi na magari mangapi,ila ni watu wengi na magari mengi pia.Ukipiga hesabu hata kwa ile 100 ya zamani bado ni mpunga mrefu saana,kwa hiyo bado siafiki suggestion ya mtoa mada,iliwezekana wa-Libya kupata huduma nyingi bure kabisa kwa nini ishindikane kwetu sie.Tutasingizia Libya ni nchi Tajiri na siye Maskini kitu ambacho si kweli.Libya wana mafuta lakini nasi tuna-hidden reserve ya mafuta,tuna madini tele,mbuga za wanyama,sources of natural gas n.k,hakuna kisingizio,ufisadi ndo kikwazo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom