Napendekeza, mwizi akiwa amevaa hijab asikamatwe!

emalau

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
2,779
3,100
Uchaguzi mdogo jimbo la igunga umenifungua macho na masikio na kuweza kutambua uelewa wa baadhi yetu, sijui kama ni makusudi au hisia tumeamua kuweka akili zetu pembeni. DC alituhumiwa na CHADEMA kwamba alikuwa anafanya mipango ya uchakachuaji. badala ya watu kuongelea tuhuma wanaongelea mavazi aliyovaa DC, hii inawezekana ni kutaka watu wasiongee ukweli ambao ni wizi wa kila uchaguzi unapofanyika na badala yake waongelee mavazi.

Kwa kuwa mavazi ya dini yanaonekana ni muhimu kuliko matendo ya mvaaji, napendekeza mwizi, fisadi, jambazi akiwa amevaa hijabu, kanzu au baraghashia asiguswe. Hata akionekana kwenye kamera za supermarket akificha bidhaa kwenye hijab asiguswe kabisa maana hilo ni vazi tukufu !!!

Nawakilisha wana JF
 
Crap. Nenda kawaambie mbumbumbu wenzio uchafu wako huu! Kukamata mtu ndi kumdhalilisha na kutaka kumbaka?
 
Nakumbuka ule ujambazi uliowahi kutokea pale Ubungo NBC miaka kadhaa iliyopita mojawapo ya wale majambazi alikuwa amevaa vazi linalotumiwa na wakina mama wa Kiislamu kujisitiri mpaka usoni kumbe ndani alikuwa na SMG ameificha, sasa kwa mujibu wa wanazuoni hawa huyu naye hakustahili kuguswa.
 
Tusiyageuze hayo mavazi kinga ya wahalifu.
Mhalifu yeyote wa dini yeyote wa chama chochote wa kabila lolote akiwa amevaa nguo yeyote lazima ashughulikiwe mara moja.
 
Crap. Nenda kawaambie mbumbumbu wenzio uchafu wako huu! Kukamata mtu ndi kumdhalilisha na kutaka kumbaka?

ccm wameishiwa sera, akili zimejaa matope ndiyo maana wanahubiri upumbavu badala ya kujibu/kujenga hoja.

yeyote anayeishabikia ccm lazima atakuwa na upungufu wa akili.
 
Hivi utajuaje kama huyu ni mwanaume au mwanamke? mwizi au si mwizi?

muslim-man-in-women-clothes.jpg
 
kudadeki navaa kanzu nazama sehemu napiga bingo mtu akiniuliza tu nasema anachafua kanzu shenzi..........

wakati unafanya hivyo jihakikishe unakadi ya uanachama ya ccm.
kwa ccm hakunaga uhalifu wa aina yeyote, maadam uwe mwanachama wao.
 
Wakuu kuna kosa limefanyika,inabidi Chadema wafanye 'maamuzi magumu' na kukubali kuna ukiukwaji umetokea.Hebu someni raiamwema ya jana karibu makala nne zinazungumzia mada ya DC na hamna hata moja inayotetea hoja za Chadema.
Chadema waliwekewa mtego wameingia kichwa kichwa na sasa tunaongelea DC wa Igunga badala ya hoja za uchaguzi.
 
Vaa hijabu, vaa kanzu, vaa vioviote vile halafu iba, tukishika tunaanza na icho kivazi chako, mwisho wa siku tunakuachia mimba...
 
Nimeipenda sentensi yako hii. Kama hutamind naomba niiweke iwe signature yangu kwenye profile yangu ya JF, ila nitakuquote;

"Kwa kuwa mavazi ya dini yanaonekana ni muhimu kuliko matendo ya mvaaji, napendekeza mwizi, fisadi, jambazi akiwa amevaa hijabu, kanzu au baraghashia asiguswe."

Halafu haya mavazi ya kidini kama hijab au burka ni ishara tu za mfumo dume unaotumia dini kuzidi kuwatawala wanawake. Mimi ningekuwa na nafasi ya kisiasa ningepiga vita uvaaji wa alama zote za kidini kwenye public offices iwe ni rozari, au barghashia, au hijab;
 
Mwizi na hijab au mavazi mwngine yo yote hawana uhusiano. DC alikuwa katika kikao cha kisiasi tena kwenye eneo la chama pinzani - akifanya nini? Hili ndilo muhimu. Kama hijab ilivuliwa au la, hilo si kipaumbele. Kipaumbele ni demokrasia katika chaguzi zetu.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom