Napendekeza kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa waziri mkuu kifutwe: kinaleta mtafaruku zaidi

Analytical

Senior Member
Mar 7, 2011
149
73
Mara ya kwanza niliposikia kuhusu kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa papo nilidhani anayehusika na anAmajibu ya kueleweka. Lakini tangia kianze, kimekuwa kikileta confusion zaidi ya utatuzi wa mambo yanayoulizwa, matokeo yake ni Spika wa Bunge kuanza kulazimisha kumkingia kifua waziri mkuu. Nikijaribu kuyaorodhesha maswala ambayo yameshazua utata ni pamoja na:.
1. Suala la mauaji ya Albino- Hapa aliishia kulia Bungeni baada kuleta contradiction juu ya hatua zinazoweza kuchukuliwa kwa wauaji wa Albino..
2. Suala la mauaji ya Arusha- Ambapo aidha kwa kujua au kutojua aliishia kuwa hakimu na kuwatuhumu CHADEMA kuwa wanahusika na mauji, ambapo ilipelekea Mbunge wa Arusha, Godbless Lema kuomba muongozo, ni hatua gani zinaweza kuchukulia pale mtu mwenye cheo kama cha waziri mkuu anapolidanganya Bunge. Tunajua wote kilichotokea, ni kwa Spika kumkaripia Lema na kumwambia alete ushahidi wa Maandishi, ambao mpaka leo haujawahi kusomwa Bungeni..
3.Suala la mawaziri wanaoishi hotelini, ambapo alisema hakuna waziri anayeishi hotelini. Hii si aibu kwa waziri mkuu bali hata kwa serikali, pale ambapo waziri mkuu anakuwa hajui kitu obvious kama hicho. Mbunge alipotakiwa kumtaja waziri alifanya hivyo na PM akabaki kimya.
4.Suala la posho za wabunge-Ilinishangaza sana waziri mkuu kujustify posho eti wabunge huwa wanasumbuliwa sana na wananchi kuwapa chochote, na eti kuwa hiyo posho ni wanawatunzia tu wananchi pesa zao. Hivi jamani kama waziri mkuu anakiri wananchi huwa wanawasumbua wananchi kuwaomba chochote, kwa hiyo solution ni kwa wabunge kulipwa posho, hii inatuambia nini watanzania? Je nani amewafikisha hapo wananchi wa Tanzania mpaka wakawa ombaomba? Je hili ndio suluhisho la kudumu? Nadhani hii si sawa. Hebu chukulia baada ya kauli hii kila mwancnhi aeekee Dodoma kuomba wabunge pesa hivi patatosha kweli?

My take: Inaonekana either waziri mkuu huwa hayuko informed kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa, au huwa anatumia maoni yake kujibu masuala ya kitaifa, kitu ambacho ni hatari kwa mustakabali wa taifa, au kudanganya na propaganda ambazo viongozi wetu wengi wamezoea.

Nawasilisha.
 
Wewe si mtu makini hata kidogo, ungekua muungwana ungeorodhesha japo maswali matano aliyoyajibu vizuri ili tutoe maoni sahihi, wewe unamshangaa kwa kutoa maoni yake binafsi kujibu maswala ya kitaifa, wakati wewe ume pick 4 questions na unaona hawezi.
 
Kama PM anajibu maswali vizuri basi kwa nini Spika anamkingia kifua? Na PM mzima anapolia Bungeni kuna haja gani ya yeye kuendelea kufesheheka kiasi hicho? Kwa ujumla maswali ya papo kwa papo hayatoi majibu sahihi zaidi ya kuishia kujikanyaga tu!
 
Mkuu naunga mkono hoja! Haina tija kwa mtu aliye chini ya mamlaka ya Rais kujibu masuala ambayo wakati mwingine yapo juu ya ukomo wake wa kimamlaka. Anaishia tu kujibu "hili lipo juu ya mamlaka yangu linamhusu Rais" niimeshuhudia mara kadhaa akijibu hivyo. Tuache kuiga mengine na matokeo tunakuwa majuha. Anauza sura tu na kuletesha huruma.
 
Mara ya kwanza niliposikia kuhusu kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa papo nilidhani anayehusika na anAmajibu ya kueleweka. Lakini tangia kianze, kimekuwa kikileta confusion zaidi ya utatuzi wa mambo yanayoulizwa, matokeo yake ni Spika wa Bunge kuanza kulazimisha kumkingia kifua waziri mkuu. Nikijaribu kuyaorodhesha maswala ambayo yameshazua utata ni pamoja na:.
1. Suala la mauaji ya Albino- Hapa aliishia kulia Bungeni baada kuleta contradiction juu ya hatua zinazoweza kuchukuliwa kwa wauaji wa Albino..
2. Suala la mauaji ya Arusha- Ambapo aidha kwa kujua au kutojua aliishia kuwa hakimu na kuwatuhumu CHADEMA kuwa wanahusika na mauji, ambapo ilipelekea Mbunge wa Arusha, Godbless Lema kuomba muongozo, ni hatua gani zinaweza kuchukulia pale mtu mwenye cheo kama cha waziri mkuu anapolidanganya Bunge. Tunajua wote kilichotokea, ni kwa Spika kumkaripia Lema na kumwambia alete ushahidi wa Maandishi, ambao mpaka leo haujawahi kusomwa Bungeni..
3.Suala la mawaziri wanaoishi hotelini, ambapo alisema hakuna waziri anayeishi hotelini. Hii si aibu kwa waziri mkuu bali hata kwa serikali, pale ambapo waziri mkuu anakuwa hajui kitu obvious kama hicho. Mbunge alipotakiwa kumtaja waziri alifanya hivyo na PM akabaki kimya.
4.Suala la posho za wabunge-Ilinishangaza sana waziri mkuu kujustify posho eti wabunge huwa wanasumbuliwa sana na wananchi kuwapa chochote, na eti kuwa hiyo posho ni wanawatunzia tu wananchi pesa zao. Hivi jamani kama waziri mkuu anakiri wananchi huwa wanawasumbua wananchi kuwaomba chochote, kwa hiyo solution ni kwa wabunge kulipwa posho, hii inatuambia nini watanzania? Je nani amewafikisha hapo wananchi wa Tanzania mpaka wakawa ombaomba? Je hili ndio suluhisho la kudumu? Nadhani hii si sawa. Hebu chukulia baada ya kauli hii kila mwancnhi aeekee Dodoma kuomba wabunge pesa hivi patatosha kweli?

My take: Inaonekana either waziri mkuu huwa hayuko informed kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa, au huwa anatumia maoni yake kujibu masuala ya kitaifa, kitu ambacho ni hatari kwa mustakabali wa taifa, au kudanganya na propaganda ambazo viongozi wetu wengi wamezoea.

Nawasilisha.

Mkuu umesahau na haya;
5. Swali la kudai nchi na serikali itayumba mafisadi wakikamatwa kwani wana nguvu.
6. Swali la kudau hataki shangingi huku msafara wake unahitaji mashangingi 50 na ndege mbili.
Mengine ?
 
Back
Top Bottom