Elections 2010 Napendekeza hiki kiwe kichwa cha habari kesho kwenye habari leo....

urasa

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
434
2
what goes around comes around!kutokana na kichwa kikubwa cha habari leo kwenye gazeti la umma habari leo kusema"ahadi za slaa hazitekelezeki",napendekeza pia kesho waandike ahadi zifuatazo za jk hazitkelezeki:
  • hospitali ya sinza kuwa ya mkoa
  • kigoma kuwa kama dubai
  • ununuzi wa meli kubwa na mya ziwa victoria
  • ujenzi wa viwanja vya ndege vya kisasa,kigoma,bukoba
  • bajaj 400 kwa wajawazito
  • bonde la ruvu kuwekezwa ktk kililmo cha mbogamboga
  • kujenga machinga complex kila wilaya ndani ya dar
naomba wana jf tuongeze nyingine kuwasaidia habari leo,najua waliandika hivyo ili kupooza joto la magazeti ya mwanahalisi,mwananchi,raia mwema na tz daima ya j5 ambayo huwa very critical na huifanya siku ya j5 serikali kupata mshituko
 
Napata kigugumizi maana,mbona hizo za miaka 50 iliyopita hazijztekelezwa??>Nimejaribu kupata picha ,kuwa Muhimbili,UDSM,IFM,CBE,DIT,MBEYA and ARUSHA Tech,KCMC,Bugando,etc na mengine mengi aliyafanya Mwalimu pamoja na kutokuwa na wasomi kama ilivyo sasa.
 
Hata miradi anayoizindua sasa ni ya mkapa,sasa sijui yeye ametekeleza nini kwa miaka yake 5
 
JK hajabuni mradi hata mmoja...anatembelea nyota ya Beny Mkapa na kuelea kwa pete za...
 
Jamani, hebu leo tumalize Mzizi wa FITINA:

UDOM alibuni nani?

Mie ninavyofahamu ni kuwa MJENZI ni KIWETE, hili halina ubishi.

Je kwenye kubuni, na kuanza maandalizi ya waalimu, wanafunzi, vifaa vya kutendea kazi nk, alikuwa Mkapa au Kikwete?
 
Yaani jamani mnataka kusema kwamba 'Mwanakwetu' hajafanya kitu chochote cha maendeleo tangu aiingie madarakani miaka 5 iliyopita?
 
kichwa cha habari "Ahadi za kikwete hazi tekelezeki" kama wanaweza kweli
 
wee haja buni kitu hivi unajua Mkapa alikua ameshaanzisha mchakato wa kufungua chuo Dodoma na ndio maana alipo ingia tu akanza kuropoka tuna fungua chuo . we unafikiri muda kilio funguliwa na muda alio ingia angeweza kufanya hivyo , chuo kina hitaji mandalizi kibao na budget ya kutosha na waalimu
 
Yaani jamani mnataka kusema kwamba 'Mwanakwetu' hajafanya kitu chochote cha maendeleo tangu aiingie madarakani miaka 5 iliyopita?

kafanya vingitu 1. kusafiri kila kukicha
2. kwenda kubembea nje
3. kuoa kisirisiri
4.kafungua miradi mingi alianzisha mkapa
5.kugawa mabilioni ya hela kwa....
 
kichwa cha habari "Ahadi za kikwete hazi tekelezeki" kama wanaweza kweli

yeah kwa kweli kama kweli wao hawana upendeleo waweke hiki kichwa cha habari kesho.ila nahisi wakiweka kuna mtu ataishia kama babu Seya
 
Hata miradi anayoizindua sasa ni ya mkapa,sasa sijui yeye ametekeleza nini kwa miaka yake 5

Yeye kajenga chuo kikuu cha Dodoma, Kamleta rais wa marekani, kapata mgawo wa vyandarua (kila nyumba vyandarua viwiliviwili), kaimarisha uhusiano wa kimataifa kwa kufanikiwa kutembelea nchi nyingi zaidi kuliko marais wengine, kajenga shule za yeboyebo, kakarabati barabara alizojenga Mkapa, kashusha thamani ya shilingi, kaongeza mlipuko wa bei ili wafanyabiashara wapate faida zaidi pia kaanzisha harakati za kuuvunja muungano na mengine mengi. Au hayo siyo mafanikio?
 
Kwa familia zetu extended baba, mama, watoto 4, mpwa na binamu. Nani ajifunike net hizo 2? au wengine wafilie mbali?
Tunahitahji elimu ya kutokomeza mazalia ya mmbu si kujificha ndani ya net.
Chagua Dr. Slaa kwa afya bora.
 
Back
Top Bottom