Napendekeza CCM ifutwe

Lukolo,
Mkuu waneno mazito sana haya. Hata kama Chadema au Dr.Slaa hatakubali uungane ktk msafara wake basi atumie aya zako kwani zimegomga hali halisi ambayo kusema kweli Wadanganyika wengi wameshindwa kutazama CCM ilipotoka na leo ni chama gani?
Nashukuru sana Mkuu Mkandara. Naamini mabadiliko ya kweli yapo mlangoni. Maana hii CCM ambayo inajiita ya kwetu kwa hakika si yetu hata kidogo. Ni yao na watoto wao.
 
Ndugu zangu,
Usiku wa leo nimekosa kabisa usingizi kwa kuufikiri mstakabali wa nchi yangu chini ya chama filisi cha CCM. Msongo huu wa mawazo ulinifikisha mahali pa kujiridhisha kwamba chama hiki yafaa kifutwe nchini. Nina sababu moja au mbili kuu za kuwaza hivyo kama ifutavyo:

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilisajiriwa kama ni chama cha wakulima na wafanyakazi na katika bendera ya CCM kuna alama za jembe na nyundo kama uwakilishi wa wakulima na wafanyakazi. Lakini hivi sasa CCM imekiuka mkataba wake wa usajili kwa kuwatosa wakulima na wafanyakazi na kuamua kuwa chama cha kifamilia, cha wafanyabiashara, matajiri wakubwa, mafisadi, majangiri, wahujumu uchumi na majambazi. Wapo watakaoubishia mtazamo huu. Lakini napenda kuwapa vielelezo vifuatavyo:

  • [.

  • Hapo kwenye red umenikumbusha baba wa taifa.................... I really miss him!
 
Hata wale wanaoruhusu kuingiza bidhaa feki ikiwemo maziwa Feki. wote hao wanatakiwa watafutwe na kuadhibiwa vikali sana. Makosa hayo yote yanatokana na very poor system put in place by CCM (Chama Cha Mafisadi). Tanzania Haiwezi kuendelea CCM ikiwa Madarakani. Hiyo ni True :confused2:
 
ifutwe kabisa kwa sababu si si chama cha wakulima tena. angalia viti maalum vilivyotengwa. kuna viti vya vijana, wanawake, walemavu na wafanyakazi. mafisadi na vibaraka wao wenye nyadhifa sehemu mbali mbali za kijamii ambao wana fedha wanapata tiketi za kugombea na kutua rushwa hadi wanachaguliwa.
Kiongozi wao mkuu aliisha kiri kuwa kila mtu kwenye chama hicho anatoa rushwa ila rushwa zenyewe ndizo zinatofautiana!!
 
Mkuu Lukolo, ni sahihi kabisa uliyoyasema.
Kosa kubwa lilitendeka wakati wa kuingiza mfumo wa vyama vingi katika nchi yetu. Mali mbalimbali walizonazo CCM hadi leo, zilitafutwa kwa nguvu ya wananchi wote wakati wa mfymo wa chama kimoja, hivyo basi, kabla ya kukubaliana na mfumo wa vyama vingi mali hizi ilitakiwa zitaifishwe na vyama vyote vya siasa viaze afresh. Hapo ndipo demokrasia halisi ya vyama vingi ingekuwa na mantiki katika nchi hii. Hadi sasa vyama vingine ni ngumu sana kupata nguvu na kuwapita CCM maana wanakila utajiri. Vilevile wana ofisi kila kijiji katika nchi hii, kitu ambacho hakuna chama kinachoweza kuwa na ofisi kila kijiji. Ofisi hizi zilitakiwa zisitumike na chama kwani zilijengwa na wananchi wote wakati huo
 
100 % true..

Ukweli ni kwamba CCM haikutaka kutoka rohoni mfumo wa vyama vingi, mfumo huu unasemekana ulipachikwa tu kutokana na fukuto na mgandamizo kutoka kwa nchi na jumuia ya 'wafadhili'...nimeweka quotes hapo kwene wafadhili kwa kusudi kabisa. Kama ulivosema mabadiliko ya katiba kuruhusu mfumo wa vyama vingi kuanzia July 1992, hayakuanzisha jamii mpya. CCM iliendelea kuwa ileile ya ubinafsi,ujeuri, na kuweka masikioni pamba ktk kusikiza kero na madhila ya watz. Na ikachukua miundombinu yote tuliyoijenga pamoja na kuitaifisha! kama kawaida ya kazi ya chama cha kupindua (kuchakachua)

Bahati mbaya watz waliokuwa na mwamko na mwangaza kuhusu utaratibu huu mpya wa vyama vingi walikuwa ni kiduchu sana, au tuseme kwa kinywa kipana kwamba walikuwa almost negligible, na CCM ika-capitalize hapo hapo..Sasa unakumbana na tatizo tokea kwa CCM as a filthy party which wants to rule forever at any cost na kumaintain incumbency, chama kinachojiita cha wakulima na wafanyakazi, chama kinachojiita cha mapinduzi lakini ilhali kina bow-down kwa wafanyibiashara, pia unakumbana na serikali na watendaji wake ambao kwao by default chama na serikali ni kitu kimoja, na pia unakumbana na tatizo la vyama vipya kupata changamaoto mbalimbali za kuji-establish.

Na ktk changamoto mpya sasa CCM inazidi kuelekea kwene mwenendo mpya ktk cycle yake ya evolution, stage inayoitwa kuganga njaa kwa gharama yeyote na state funded swindling. It is really a one sad story indeed..lakini cha msingi we have the chance now to turn the tables kwa kupitia polls zijazo, halafu tutaona nini cha kufanya baada ya hapo.
 
Halafu bila hata aibu wanatangaza Chama kimemzuia Kikwete kushiriki kwenye midahalo!!! Hivi Kikwete si ndiye Mwenyekiti wa Chama cha Mafisadi na ndiye mwenye sauti ya juu kuliko mtu mwingine yeyote ndani ya chama hicho filisi. Kwa maneno mengine Kikwete kama angetaka kushiriki kwenye mdahalo angeweza kabisa kufanya hivyo bila yeyote yule kumzuia sasa wanatuzuga Watanzania eti Chama kimemzuia Kikwete kushiriki midahalo. Maneno ya kweli hapa ni Kikwete anajijua ni kilaza na kushiriki midahalo hiyo ndiyo itakuwa mwisho wa ndoto zake za kubaki madarakani sasa kaamua kujificha nyuma ya ukuta wa chama filisi cha mafisadi.
 
NJIWA, Are you serious? Inasikitisha sana kusoma mawazo kama haya! TANU na ASP vilipata wapi uzoefu wa kuongoza vilipoongoza mara baada ya uhuru? Nasema kwa masikitiko kuwa mawazo haya ni MAWAZO MGANDO yasiyostahili kutiliwa maanani. Tusitegemee chama kutoka peponi kuja kuongoza Tanzania. Watanzania wakiamua kuvipa madaraka ya kuongoza nchi vyama vya upinzani vilivyopo nchi haitayumba. TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA.
 
Duu! Lukolo umemaliza yote Maneno ni makali yenye kutia uchungu! tumepoteza hope ya maisha yetu na familia zetu ktk utawala huu usio na haya wala huruma, tunateswa na wachache wenye power na pesa, hatuna pa kukimbilia the justice system is highly corrupted, polisi wanatutesa, Wanajeshi wanatutesa na kutuua, shule zetu za kata kwa watoto wetu hazina walimu wala resources zakutosha, we have been neglected katika ardhi yetu wenyewe na CCM bado inatuburuza katika mateso ya kusaga meno Mungu ailaani na Mungu Ibariki Tanzania:mad2:

uwezo tunao wa kutosha kabisa, sababu tunazo nyingi lukuki. Sisi ndio wapiganaji wa leo tunaotakiwa kuikomboa tanzania yetu. Kwa pamoja mm na ww tunaweza. ndio tunaweza! Historia ni mwalimu popote pale duniani nguvu ya uma ulio dhamiria kwa kumaanisha haijawahi kushindwa. Saa ya ukombozi ni hii na tanzania bila c c m inawezekana. Hatuhitaji mwekezaji wa kuliwezesha hili wala hawatashuka malaika wa kutunasua kwenye makucha ya hawa majangiri. Sisi wenyewe tunaweza na wakati ni huu ambapo sisi tumeshika mpini. Ufaransa waliweza kwa nini sisi tushindwe?
 
sasa ikifutwa CCM.. hii nchi itakuwa Njia panda .. bado hakuna chama chenye uzoefu wa kuongoza tanzania yetu

sasa hilo ulilonalo naweza kuliita ni tatizo la kimtazamo au la kifikra zaidi. Inamaana kwa mtazamo wako kuna chuo maalumu kinachotoa degree za uzoefu? Au kuna duka la kuuza huo uzoefu? Kwa taharifa yako watanzania wengi wanao uzoefu wa kutosha maana mateso waliyosababishiwa na genge hili la waporaji wanaojitambulisha kwa alama ya jembe na nyundo ni mwalimu wa kutosha. Au haukubaliani na usemi usemao shida ni mwalimu?
 
Well said!! Nafikiri hadi hapa Njiwa amejifunza kwamba aliweka post yake bila umakini wa kutosha. Amesahau kwamba huko Madagascar, DJ kawa Rais? Yeye alipata wapi uzoefu? Shida zitawafanya watu wajue nini wafanye kwa maslahi ya nchi yao.
 
Lukolo,

Viongozi wengi wa upinzani wametueleza kuwa matatizo yetu yamaesababishwa na CCM na hili halina mjadala. Sisi kama wapiga kura ndio wenye hukumu ya mwisho kwani ni wajibu wetu kupiga kura na kulinda kura zetu hapo 31/10/2010. Ukombozi uko mikononi mwetu na lazima tujitoe mwaka huu nafasi ipo.
 
Naungana na mtoa hoja kuwa kuongoza hakuhitaji uzoefu,kwani kikwete alipochaguliwa 2005 alitoa wapi uzoefu je alishawahi kuwa raisi???hayo ni mawazo mgando.....na ambayo ccm wameyatumia ili kuendelea kuchukua jasho letu kiulaini.sijawahi kuona yeyote aliyeingia madarakani eti kwa kuwa ana uzoefu.tz amkaaaaaaaaa.saa ya ukombozi ni sasa,ole kwetu kama tusipoamka na kuchangamka
 
Vyombo vyote vya serikali ni vya watanzania. Jeshi, Polisi, Usalama wa taifa TRA na kadhalika. Walio katika vyombo hivyo ni damu katika damu yetu, mifupa katika mifupa yetu. Sidhani kama yupo askari jasiri atakayemfyatulia risasi baba yake mzazi kwa sababu ya kutii amri ya fisadi fulani. Wananchi tushikamane Tanzania ni yetu na sisi ndio watanzania, pasipo sisi hakuna Tanzania, hakuna Majeshi, hakuna serikali na hakuna CCM. Katika sisi ndio kuna nchi inaitwa Tanzania na watanzania na vyote vilivyomo ni mali yetu tuliyopewa na Mungu. Tukitaka kiongozi tumtakaye hakuna wa kutuzuia, tukitaka chama tukitakacho hakuna wa kutuzuia. Shime watanzania, mustakabali wa nchi yetu uko mikononi mwetu.
 
Well said brother/sister! Nafikiri idadi kubwa ya watanzania imeshaamua. Wanatuangusha wale wachache wenye njaa kali, wanaojipendekeza kwa CCM ili wapate elfu mbilimbili, Tshirt, Khanga na cap. Watu hawa wanasahau kwamba hivyo vyote ni vya kupita. Ningetamani kuona watanzania wanapokea hizo rushwa halafu wanaitosa CCM tar 31/10
 
Vyombo vyote vya serikali ni vya watanzania. Jeshi, Polisi, Usalama wa taifa TRA na kadhalika. Walio katika vyombo hivyo ni damu katika damu yetu, mifupa katika mifupa yetu. Sidhani kama yupo askari jasiri atakayemfyatulia risasi baba yake mzazi kwa sababu ya kutii amri ya fisadi fulani. Wananchi tushikamane Tanzania ni yetu na sisi ndio watanzania, pasipo sisi hakuna Tanzania, hakuna Majeshi, hakuna serikali na hakuna CCM. Katika sisi ndio kuna nchi inaitwa Tanzania na watanzania na vyote vilivyomo ni mali yetu tuliyopewa na Mungu. Tukitaka kiongozi tumtakaye hakuna wa kutuzuia, tukitaka chama tukitakacho hakuna wa kutuzuia. Shime watanzania, mustakabali wa nchi yetu uko mikononi mwetu.
 
Utatafutwa sana kwa hii threadi unajua ukweli unavyouma ndugu yangu?...........pamoja na hayop tuko pamoja mpaka kieleweke naamini wewe ni mmoja wa wale ambao hawako tayari kudanganyika tena.........
ndugu zangu,
usiku wa leo nimekosa kabisa usingizi kwa kuufikiri mstakabali wa nchi yangu chini ya chama filisi cha ccm. Msongo huu wa mawazo ulinifikisha mahali pa kujiridhisha kwamba chama hiki yafaa kifutwe nchini. Nina sababu moja au mbili kuu za kuwaza hivyo kama ifutavyo:

Chama cha mapinduzi (ccm), kilisajiriwa kama ni chama cha wakulima na wafanyakazi na katika bendera ya ccm kuna alama za jembe na nyundo kama uwakilishi wa wakulima na wafanyakazi. Lakini hivi sasa ccm imekiuka mkataba wake wa usajili kwa kuwatosa wakulima na wafanyakazi na kuamua kuwa chama cha kifamilia, cha wafanyabiashara, matajiri wakubwa, mafisadi, majangiri, wahujumu uchumi na majambazi. Wapo watakaoubishia mtazamo huu. Lakini napenda kuwapa vielelezo vifuatavyo:
  • muundo wa chama: Ni nani walioshika nafasi za juu za chama, nani ni wachangiaji wakubwa wa chama, ni kwa kiasi gani familia ya kikwete na makamba imeweka mizizi ndani ya chama? Baba mwenyekiti, mama mjumbe wa kamati kuu, mtoto mjumbe wa halmashauri kuu ya uvcc, mtoto ni mwenyekiti wa vijana chipukizi: Baba ni katibu mkuu wa chama, mtoto mshauri wa raisi na mgombea ubunge: Baba rais mstaafu, mtoto waziri. Hii ni mifano michache tu wapo wengi ndani ya ccm ambao utasikia historia zao zinaanzia kwa wazazi wao.

  • uendeshaji wa chama: Ni akina nani wenye sauti ya mwisho ndani ya ccm? Naamini hakuna atakayenibishia juu ya hili. Wahindi na wafanyabiashara wakubwa ndio wanaoiongoza ccm na nchi kwa ujumla. Hao ndo wanaopanga nani awe nani na wapi? Hao ndo ambao rais alisema wakikamatwa kwa wizi wa fedha za epa, na kupelekwa mahakamani nchi itayumba. Hao ndo mabosi na waajiri wa kikwete na ccm kwa ujumla wake. Si wakulima na wafanyakazi tena. Kwa kuwa wakulima na wafanyakazi hawana tena nafasi ya kuhoji wala kudai haki yao kutoka katika chama kinachojiita ni cha kwao.

  • nafasi za uongozi: Ukifuatilia kwa umakini utagundua kwamba uongozi katika nafasi ya ubunge na udiwani, kwa kiasi kikubwa zimechukuliwa na watu maarufu, wenye pesa za kutosha kununua kura, huku wakulima na wafanyakazi wa kawaida wa serikali wenye kipato cha kawaida na wasio na uwezo wa kununua kura wakiambulia patupu. Sehemu kubwa ya wagombea kupitia ccm ni matajiri waliojijenga kiuchumi na wafanyabiashara wakubwa, wakulima na wafanyakazi hawana chao.

  • mwenyekiti wa ccm aliwakataa wafanyakazi kweupe alipowahutubia wazee wa dar es salaam. Kwanza nauona huu kama ulimbukeni: Wanaodai maslahi bora ni wafanyakazi, lakini wanaohutubiwa ni wazee wastaafu, kuna uhusiano gani hapo? Lakini kikubwa ni kwamba huyu mwenyekiti alisema wazi kwamba serikali yake haina uwezo wa kuboresha maslahi ya wafanyakazi (ambao kiujumla ndio wanaochangia kuinua hali ya kilimo kutokana na kugawana kipato chao na wa kwao huko vijijini ambao ni wakulima). Wakati akikataa kuwatekelezea wafanyakazi mahitaji yao, alikuwa anajua kabisa kwamba ana msululu wa makampuni ambayo ameyasamehe kodi kwa miaka kadhaa ili yachume ambapo hayakupanda. Alikuwa anajua kabisa kwamba kuna meli ya kinana inabeba magogo na pembe za ndovu kijangiri, alikuwa anajua kabisa kwamba kuna rostam aziz ambaye amekalia mabilioni ya watz. Kwa hiyo aliwakataa wafanyakazi akawalinda wafanyabiashara, wageni, mafisadi, majangiri na majambazi wa uchumi wetu.

  • naamini pia kwamba ccm si chama cha wakulima na wafanyakazi kwa kuwa serikali ya ccm ndiyo ilishiriki katika kuviua viwanda vyote vilivyokuwa vinasindika mazao yetu ya kilmo, ndiyo iliyoua kiwanda cha mbolea, ndiyo hiyo iliyoingia mikataba mibovu ya kuimaliza nchi. Wakati ccm ikiingia mikataba ya tangold, meremeta, deep green, iptl, richmond na mingineyo ya hivyo, iliwashirikishaje wakulima na wafanyakazi? Wakati ccm inaidhinisha wizi wa mabilioni ya fedha epa kuyapeleka kwa wafanyabiashara wakubwa nchini ilikumbuka kwamba kuna zaidi ya asilimia 60 ya watanzania wasiokuwa na ajira wala mitaji? Na iliwashirikishaje hawa wote ambao ndio wanachama wa ccm?
kwa kuwa chama hiki kimekiuka mkataba wa uandikishaji wake ambao unaonyesha kwamba ni chama cha wakulima na wafanyakazi, na kikajikita katika kulinda na kusimamia maslahi ya wafanyabiashara, wanafamilia, mafisadi, matajiri na majambazi. Napendekeza kifutwe, na kuanzisha chama halali cha wakulima na wafanyakazi, na hao wafanyabiashara, mafisadi, matajiri na wengine wanaofanana nao waanzishe chama chao kingine.
 
Utatafutwa sana kwa hii threadi unajua ukweli unavyouma ndugu yangu?...........pamoja na hayop tuko pamoja mpaka kieleweke naamini wewe ni mmoja wa wale ambao hawako tayari kudanganyika tena.........
Nimeamua kujitoa mhanga ndugu yangu. Watakaponitafuta nitawataka wakanushe lililo la uongo katika hayo.
 
Back
Top Bottom