Nape: Wema ametupa heshima kubwa, tutamuweka kwenye rekodi zetu

...unaifungia television ya taifa kuonyesha wananchi habari za bunge, unawanyima wananchi haki wa kufuatilia habari zinazohusu uendeshwaji wa serikali yao na maendeleo ya taifa lao, unawakosesha wananchi haki na uhuru wa kuchangia mawazo mbadala kuhusu mustakabadhi wa taifa lao... lakini badala yake unaenda ku-promote application yenye habari zinazohusu maisha binafsi ya mtu. Kweli hii nchi ni ngumu sana.
 
Mi naona wema mwenyewe Kafanya juhudi binafsi za kuandaa hilo tukio na pia katumia ubunifu kumualika waziri.Hao vijana unaosema je wameshafanya hivyo na waziri akakataa kuhudhuria huo uzinduzi?
 
Watanzani tuacheni wivu wa kijinga mwenzenu keshafanya yake anategemea kupiga hela nyie mnabaki kulialia tu fanyeni ubunifu umizeni vichwa muone kama hamtatusua,mwenzenu kila kukicha anawaza jinsi ya kubaki kuwa madam wema asiechuja aweze kuyamudu maisha ya mujini nyie ni kuponda tu shauri yenu muda haumngoji mtu.Wema nakupa big up sana kwa juhudi zako pamoja na ubunifu wako songa mbele mama.
 
Kuna mtu alietengeneza app yake akawaalika viongozi wakagoma kwenda? Toa mfano. Nijuavyo hii ya wema Ni hatua kubwa sana MBELE KWANI SASA DUNIA NZIMA WANAWEZA KUZINUNUA KAZI ZA WEMA NA TAIFA LITAPATA KODI NA MAISHA KUSONGA MBELE.

Unaonekana ka TAAHIRA hivi
 
Waziri kaenda kuzindua nini? heshima gani imepatikana kupata habari zake pia? mie sijaelewa vizuri maana DUH...

Wanajua wao lililo nyuma ya pazia, sio kwa hili mmmmh
Kupata habari za madame ni heshima tosha. Teh teh teh
 
Ni kichekesho haswa
Atawawekea na habari zake za ma**ba
Ndio zinapendwa sasa tufanyaje! Huu ni upuuzi wa ngazi ya phd. Kuna apps kama milard ayo na nyingine nyingi tu hazijawahi kusifiwa eti hii ya madame ndio inasifiwa..tuwe tunapata habari zake za kifuska then what! Angekuwa ni mtu mwanaharakati anayeisaidia jamii kwa vitendo vinavyoeleweka ingekuwa sawa.
sipingi yeye kuwa na app coz kuna watu wanapenda kufuatilia utumbo wake, ila waziri kuzindua hiyo app ni kitu cha ajabu kwangu. Wema angeizindua kivyake vyake wala sina tatizo.
 
wema anaanzishaga vitu harafu havidumu

Mie ni Team wema lakini sasa habari za wema tutakazopata ni zipi ?? kama kila siku ndugu yetu habari tunazosikia ni Scandal tu ..msinitupie mawe napenda kujua tu
 
Nchi yangu Tanzania, zamani tulikuwa tunawacheka wacongo but naona sasa hivi tunaongoza kwa ujinga
 
sasa mbona tunalalamika tu, ..tutizame kwa jicho la pili..!
kwanza niseme mh waziri yuko sahihi kuhudhuria hiyo hafla maana alialikwa tena kwa special request na akaangalia timetable yake akaona wizara yake haikuwa na maswali ya kujibu bungeni, kwa hiyo akaona aende kutoa support kwa msaani wema sepetu ukizingatia yeye ndie waziri wa habari,utamaduni na michezo.,hayo maneno yakusema ameacha kwenda bungeni kwa sababu ya hafla hiyo na maneno mengine nadhani ilikuwa ni kama kunogesha sherehe, si unajua tena wanasiasa maneno mengi...sijaona kosa la mh Nape hapo
kina millardayo na jf na wengine sijawahi kusikia wamehitisha hafla kwa ajili ya kuzindua au hafla zozote wakamualika mh waziri akakataa kwenda!
acheni hizo fikra za kukosoa kila kitu kama za ukawa
let us be a little bit positive!
Mimi wema sepetu naskia tu kwani ana kazi gani?
 
Haya mambo eti hafla ya kufungua app ya kijinga no logik behind but vijana wenye vipaji hawawaoni nini??? Huku ulaya basi angekuwa anafungua kila siku maana Hata watoto wana app za maana zenye logik behind.
 
Back
Top Bottom