Nape: Wema ametupa heshima kubwa, tutamuweka kwenye rekodi zetu

Kuna mtu alietengeneza app yake akawaalika viongozi wakagoma kwenda? Toa mfano. Nijuavyo hii ya wema Ni hatua kubwa sana MBELE KWANI SASA DUNIA NZIMA WANAWEZA KUZINUNUA KAZI ZA WEMA NA TAIFA LITAPATA KODI NA MAISHA KUSONGA MBELE.
Aisee wewe hatari, dhahabu na Almasi hazijaleta kipato ije application ya Wema. Dunia nzima wanamjuwa wema ahhhhhh. Nchi hii inatia huruma kweli.
 
Waziri anaacha BUNGE sbb ya Wema Sepetu apps... Mungu uko wapi..? Umetuacha pekee yetu bwana, umetusahau duniani, tu yatima, hatuoni, eeh Mungu hadi lini utarudi..? Ungekuwepo haya yote yasingetokea, uuuhh..!!
 
Hao ndio fisiem walijua namba tutaisoma sisi raia tu. Wao walio karbu n jiko hawataguswa. Eeeeh
Mbele kwa mbele fisiem fisiem
 
Nape nae asitake kutuzingua,aache mapenzi na ulafiki ktk sakata hili,pia anatakiwa ajue kua huyu sio laisi wa malafiki na washikaji huyubyupo kikazi zaidi ndiomaana kachagua watu wa kazi ili afanyenao kazi na sio vinginevyo,,,,ukimchekea nyani utavuna mabua hakuna cha Wema wala lafikiake Wema kama anausika Shelia ifuate mkondowake sasa kama na yeye alikua mwema angethamini taifanlake na kujalibwaTz wenzie.
 
Waziri anaacha BUNGE sbb ya Wema Sepetu apps... Mungu uko wapi..? Umetuacha pekee yetu bwana, umetusahau duniani, tu yatima, hatuoni, eeh Mungu hadi lini utarudi..? Ungekuwepo haya yote yasingetokea, uuuhh..!!

Sikuwa nimeiona hii thread wala kusikia hii app! haya maajabu! mawaziri wetu ndio walivyo hawajui majukumu yao na hawana viapaumbele.
 
Sikuwa nimeiona hii thread wala kusikia hii app! haya maajabu! mawaziri wetu ndio walivyo hawajui majukumu yao na hawana viapaumbele.
Ndugu yangu, ni waziri huyu huyu ambaye ana madaraka ya kuweza kuamka asubuhi bila kushauriana na yeyote akakifunga kituo cha redio au gazeti kwa muda anaotaka yeye hata kama kimeajiri watu elfu na kinalipa kodi vizuri!
 
Waziri wa habari, michezo na sanaa Nape Nnauye amesema msanii wa filamu Wema Sepetu amewapa heshima kubwa kwa ku launch application yake ya Wema Sepetu ambayo itakuwa inatoa taarifa za Wema.

Aliyasema hayo alipokuwa amehudhuria hafla hiyo aliyodai amehairisha kuhudhuria vikao vya bunge ili asiikose, pia amesema serikali itamsaidia na kumtangaza.



WAZIRI NAPE AZINDUA MFUMO WA KISASA WA WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akizindua mfumo wa kisasa kabisa wa msanii wa filamu hapa nchini,WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION mbele ya waandishi wa habari, katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.Picha na Geofrey Adroph(Pamoja Blog)


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye akizungumza kabla ya kuzindua mfumo wa kisasa kabisa wa msanii wa filamu hapa nchini,WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION mbele ya waandishi wa habari,katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.


Msanii wa Bongo Movie na aliyewahi kuwa Miss Tanzania Maadam Wema Sepetu akizunguma mbele ya waandishi wa habari katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar kabla ya kuzindua huduma yake WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION,ambayo itakuwa ikijumuisa matukio yake yote sambamba na video mbalimbali yatakayowekwa kwenye mfumo wa teknolojia ya kisasa kupitia simu za mikononi.

Mtaalamu wa huduma za mitandao kutoka Push Mobile, Haji Yussuph akifafanua jambo kuhusiana na huduma hiyo ya WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION

Meneja wa Biashara wa Hartmann Trader ambao ndio watoa huduma ya Wema Sepetu Mobile Application,Cecil Mhina akifafanua namna huduma hiyo inavyoweza kutumika na pia maelezo kadhaa namna ya kujinga na kupata taarifa mbalimbali na video kupitia huduma hiyo

Munalove(kushoto) akimwelekeza mama mzazi wa Wema Sepetu jinsi ya kujiunga na WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION mara bada ya kufanyika kwa uzinduzi huo

Msaniii wa Bongo Movie, Wema Sepetu akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye baada ya uzinduzi wa huduma hiyo kufanyika mbele ya waandishi wa habari, katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini

Msanii wa Bongo Movie na aliyewahi kuwa Miss Tanzania Maadam Wema Sepetu akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wake wa huduma ya WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION

Wema Sepetu akiwa amemkumbatia mama yake mzazi mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi huo.

Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi
Mkuu; mi Nilidhani application ya "dawasco"au "tanesco",warahisishe huduma zao...kumbe "Wema pepetu" bhana
 
Ndio maana jamaa ame questions kuhusu kukamatwa kwa Wema na Madawa ya Kulevya Kumbe CCM. Haju safari hii wote tunaisoma namba.
 
Back
Top Bottom