NAPE: Watu wameshindwa kujitokeza kupiga kura wakiohofia kumwagiwa Tindikali

Nashukuru Mzee Mwanakijiji kwa comment yako,nahisi umepotoka kwa kiasi fulani kwa kukariri kuwa silaha ya CHADEMA ni issue ya ufisadi tu...Na ndio maana ulipoona kuwa hii silaha haikutumika sana umepata wasiwasi kidogo..well,kwenye vita unapaswa uwe na silaha mbalimbali na mbinu mbalimbali za kuweza kupambana na adui yako,hii ni kwasababu kila silaha au mbinu inafaa kwa mazingira husika tu...Uwezi ukawa unapigana vita kwenye jangwa ukavaa makombati ya kijani na nyeusi hapo utachemsha,uwezi tumia mshale kwenye vita vya silaha za moto mkuu!! Sasa CHADEMA kutotumia silaha ya ufisadi ni mbinu ya kawaida katika vita,na hata hivyo sidhani kama hii silaha haikutumika kama ambavyo wengi mnasema,baadhi ya maeneo niliwasikia Dr Slaa,na M/Kiti Mbowe wakisema jambo hili....Lazima chama kiwe na mbinu mbadala za kupambana katika uchaguzi,sasa Rostam alikuwa ametoka,utasema alikuwa fisadi itasaidia nini kwa wakati ulipo wakati sio mgombea?

Lakini pia Mwl Kashindye aliyekuwa mgombea wa CDM na Leopald Mahona aliyekuwa mgombea wa CUF walisema wazi kuwa kuna baadhi ya mambo aliyoyafanya Dr Kafumu akiwa kamishina wa Madini yameletea taifa hasara kubwa,sasa mlitaka wasemaje ndio mkubali kuwa walisema?

Conclusively;
Lazima chama kiwe na mbinu mbadala za kupambana,sio lazima kila siku msikie ufisadi! ufisadi! ufisadi! wananchi wanahitaji sera pia,TUTAWAFANYIA NINI na TUTAWATOAJE KWENYE UMASKINI HUU..Tusikariri!!!!
Wewe acha maneno mengi, mliogopa kwa sababu ya nguvu aliyo nayo RA igunga.
 
Gracious,
SI KAZI YANGU KUWAFURAHISHA CHANDIMU, WALA CHANDIMU HAWANA MAMLAKA YA KUNIFUNDISHA CHA KUFANYA, ETI LEO NIFANYE AMBACHO CHANDIMU MNATAKA NIFANYE??? ,imekla kwenuu.... Mwl. Aliwhi sema...... Ukiona adui yako anazifia slaa zote za maangamizi jua umekosea. FURAHA YANGU NI KUWAKERA CHANDIMU SO MKIKEREKA NIJUA NIKO VIZUIIIIIII

Wewe ni mjinga na haujui ulisemalo,hivi kwa nini unakuwa mlopokaji wa mambo yasio na tija kwa watu?yaani ni bora ungekaa kimya kuliko kutoa upumbavu wako mbele ya kadamnasi,shame on you.
 
Hii inaonekana wazi kabisa kuwa CDM wako tayari kushirikiana na hao wanao waita mafisadi wa CCM ilimradi wapate ushindi.
 
Kaka Nape nadhani angepata taarifa za kina toka NEK au wapiga kura sababu haswa kabla ya kutoa matamko kwenye vyombo vya habari. iLA KAMA NI KWELI KASEMA BASI tutambue yeye ni miongoni mwa NEC
 
Binafsi ningependa kusikia jibu la swali hili. Kwani nami ninalo hivyo hivyo. CDM imetambulika zaidi kutokana na kuongoa vita dhidi ya ufisadi; lakini Igunga ambako anatoka RA - mwenye kuhusishwa na kashfa kadha wa kadha za ufisadi na ambaye alithubutu kujitokeza siku ya ufunguzi wa kampeni - hoja ya ufisadi haitajwi, RA hatajwi wala kuonesha kuwa ni maamuzi ya wana igunga yalimleta RA.. .. nasubiri sana jibu la swali hili maana linaendana na swali la kwanini Kafumu hakuusishwa na RA katika mambo fulani fulani...
Mzee Mwanakijiji,

Nimekuwa najiaminisha kuwa pengine silaha hiyo haikutumika kwa kuwa chama chetu kina ghala lililosheheni silaha za kila aina. Lakini nikikumbuka hapo nyuma Eng mmoja humu alivyovurumisha shutuma za mwemyekiti wetu kuwa mmoja wa waliowahi kuvuta mshiko toka kwa Rostam, naingiwa na hofu kuwa Rostam anaweza kuwa untouchable hata miongoni mwetu.
 
Ww ni mtanzania kweli au mrundi 'hofa' maana yake nini?

Mimi natoka South Africa,nina uraia wa nchi mbili...nashukuru kwa kunisaidia,kumbe nilikosea hapo? Inatakiwa iweje? Japo nasikia una "F" ya kiswahili kidato cha nne,pale Msakaleli Secondary Uliposomea.....
 
kwa maneno mengine alimaanisha wananchi wa igunga hawana imani na ulinzi wa polisi na serikali yao, kama Rais mwenyewe aliahidi atawadhibiti wote, askari nao wakamwagwa na bado wananchi wakaogopa kwenda kupiga kura.
 
Wewe acha maneno mengi, mliogopa kwa sababu ya nguvu aliyo nayo RA igunga.

If that is the case? Basi CDM ni chama makini kinachoweza kusoma majira na nyakati.....na ndio maana nikasema silaha hiyo haikuwa sahihi kwa Igunga...sasa ulitaka nisemaje?
 
Mbona viongozi kibao wa CDM wako hapa JF kwa majina tofauti na wengi kazi yao ni kutukana hovyo. Bora yake yeye amekuja na ID yake ya kweli .

Unayo evidence,sio unabwabwaja kama bosi wako nape.Acheni taarab,jibuni hoja
 
Maskini Jamani hakuna mwanasiasa nilikuwa namkubali kama nape, niliposikia kachaguliwa kuwa mkuu wa wilaya nikafurahi na alipopewa ukatibu nikajua kiti kimepata mtu, cha ajabu sio nape niliyekuwa namkubali , huyu wa sasa hivi sijui kapatwa na nini? anasema watu walijitokeza wachache wakihofia tindikali hivi kweli nape anakumbukumbu kichwani?

Hivi green gurd ni ya nani, janja will ni vikundi vya chama gani? halafu chaguzi nyingi za hivi karibuni idadi ya watu wanojitokeza inakuwa kidogo na chama tawala na serikari yake watuambie kwa nini watanzania wanogopa kujitokeza kupiga kura ili hari sifa wanazo. mi nilitegemea ataongelea kuvu kubwa ya vyombo vya dora kuwa inawatisha wananchi wa vijijini , jaribu kufikiri wananchi wa igunga kwa mara ya kwanza wanaona gari la polisi lenye maji ya kuwasha wanaambiwa limekuja kwa ajiri ya uchaguzi. nakwambia wenye mionyo mwepesi hatoki kupiga kura na ccm inafurahia kwani itatumiea mtaji wa wanachama wake,
pia nilitegemea nape atazungumzia kuporomoka kwa ccm mwaka jana walipata kur 36,000 igunga ndani ya mwaka mmoja wanapata 26,000 kama kura 10,000 zimepotea ndani ya mwaka 1 vipi baada ya miaka 4? du nape anaboa hana tofauti na Tabwe hiza
 
Mzee Mwanakijiji,

Nimekuwa najiaminisha kuwa pengine silaha hiyo haikutumika kwa kuwa chama chetu kina ghala lililosheheni silaha za kila aina. Lakini nikikumbuka hapo nyuma Eng mmoja humu alivyovurumisha shutuma za mwemyekiti wetu kuwa mmoja wa waliowahi kuvuta mshiko toka kwa Rostam, naingiwa na hofu kuwa Rostam anaweza kuwa untouchable hata miongoni mwetu.

Gagnija.. hivi kweli tunaweza kabisa katika uwezo wetu wote wa kufikiria kuzungumzia kujiuzulu kwa RA bila kuzungumzia ufisadi wa Richmond, Dowans, EPA really? angekuwa RA ameacha ubunge kwa njia nyingine yoyote ile isipokuwa ya kujiuzulu tungeweza kufikiria labda isingekuwa vizuri kumtaja lakini mtu ambaye amethubutisha watu wote wamguse na hakuna wa kumgusa. I too believe he is more than almighty powerful!
 
If that is the case? Basi CDM ni chama makini kinachoweza kusoma majira na nyakati.....na ndio maana nikasema silaha hiyo haikuwa sahihi kwa Igunga...sasa ulitaka nisemaje?
Kwanini hukusema Haikuwa sahihi kwa sababu ya kumuogopa RA. Kwa maana hiyo sera zenu ni za kuridhisha watu flani na sio wananchi kama mnavyo jitangaza. Nyie mko njiani kuolewa kama walivyo olewa CUF.
 
Nadhani kuna ukweli kwenye madai yake. Unajua watu wa vijijini ni waoga sana. Kitendo cha Magwanda kwenda na mapanga kiliwafanya wanyong'onyee na waogope sana.

mbona husemi bastola ya rage? na police wengi walivyo vaa kama kuna vita .......kwani hujui ccm imefanya asili mia kubwa ya watu wa vijijini kuwa ni waoga kwa vitu vidogo vidogo ...
niliwahi siku moja kwenda sehemu ya mashambani kule naberera arusha na gari la kiamerika kubwa kidogo kila nikisimama niulize ninakoenda watu wanakimbia kisa hawaja wahi ona gari kama hilo..
 
Nape anaweza kuwa sawa,kwa maana hiyo watu pia waliogopa bastola ya Rage na wale mamluki walitoka afghanistan kama WANANCHI walivyotishwa na MUKAMA
 
Gagnija.. hivi kweli tunaweza kabisa katika uwezo wetu wote wa kufikiria kuzungumzia kujiuzulu kwa RA bila kuzungumzia ufisadi wa Richmond, Dowans, EPA really? angekuwa RA ameacha ubunge kwa njia nyingine yoyote ile isipokuwa ya kujiuzulu tungeweza kufikiria labda isingekuwa vizuri kumtaja lakini mtu ambaye amethubutisha watu wote wamguse na hakuna wa kumgusa. I too believe he is more than almighty powerful!
Ndugu yangu, hawa jamaa wanazungusha maneno lakini ukweli unaonekana.
 
Hii inaonekana wazi kabisa kuwa CDM wako tayari kushirikiana na hao wanao waita mafisadi wa CCM ilimradi wapate ushindi.

Your very sick.Plz take initiative to attend hospital immediately.....
 
mbona husemi bastola ya rage? na police wengi walivyo vaa kama kuna vita .......kwani hujui ccm imefanya asili mia kubwa ya watu wa vijijini kuwa ni waoga kwa vitu vidogo vidogo ...
niliwahi siku moja kwenda sehemu ya mashambani kule naberera arusha na gari la kiamerika kubwa kidogo kila nikisimama niulize ninakoenda watu wanakimbia kisa hawaja wahi ona gari kama hilo..
Wewe labda ulikwenda na kifaru
 
Your very sick.Plz take initiative to attend hospital immediately.....
Naona lugha imegeuka ghafla? Jibu swali sio unapaparuka hovyo. Kama hutaki kunijibu mimi basi mjibu Mwanakijiji
 
Back
Top Bottom