Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,795
- 71,214
Mkuu mie nadhani kila mahali panapaswa kupeleka ujumbe ule utakao eleweka kwa wahusika. Kama watu waliangua kilio Rostam alipotangaza kuachia ngazi (Ingawa hatuna uhakika kama kilio kile ni cha kweli au walinunuliwa kulia) muda huu wa kampeni ulikuwa mfupi sana kuwaelewesha kuwa mliye mlilia ndio fisadi mkubwa na chanzo cha matatizo mengi hapa nchi.Binafsi ningependa kusikia jibu la swali hili. Kwani nami ninalo hivyo hivyo. CDM imetambulika zaidi kutokana na kuongoa vita dhidi ya ufisadi; lakini Igunga ambako anatoka RA - mwenye kuhusishwa na kashfa kadha wa kadha za ufisadi na ambaye alithubutu kujitokeza siku ya ufunguzi wa kampeni - hoja ya ufisadi haitajwi, RA hatajwi wala kuonesha kuwa ni maamuzi ya wana igunga yalimleta RA.. .. nasubiri sana jibu la swali hili maana linaendana na swali la kwanini Kafumu hakuusishwa na RA katika mambo fulani fulani...
MMKJ, inahitaji muda wa kutosha kumshawishi Padre kuwa shekhe au Shekh kuwa Padre maana sio jambo analoliamini. Mbinu ya kuliweka pembeni kwa muda suala hilo ilikuwa muafaka