Nape: Wapinzani ni failures!

Msendekwa

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
442
168
Nape Nnauye, kupitia taarifa ya habari Chanel 10 anadai wote walioanzisha vyama pinzani wametoka CCM na kwamba walikuwa failures kule(watu walioshindwa kufuata taratibu ndani ya CCM, wamezoea vya kunyonga!)
Swali kwake:
Alipoenda kuanzisha CCJ, alikuwa winner?
 
Oooh!!Kasau kwamba wananchi wote walikuwa ccm kwa kupenda au kulazimishwa. Na sasa machaguo yameongezeka kwa wale waliolazimishwa kwenda wanakotaka.Kama ccm ingekuwa na uwezo wa kibinadamu, ingewatapika kitambo.
 
Kwa mantiki isiyopinda basi yeye alifeli kote, maana alishindwa CCM akataka kukimbilia chama fulani akakataliwa ,masharti yake pia akajaribu kuanzisha CCJ ambayo nayo hakuweza. So he is a double failure.

Lakini pia atoe mfano wa watu walioshindwa kufuata taratibu huko CCM wakaanzisha vyama vingine na sasa wameshindwa kuendeleza kile walichokiamini kuwa kina manufaa kwa Watanzania. Au anaanza kurudia tena jina alilopewa na Heche.
 
Mh! Nepi kweli chama hakina msemaji, hivi kwa nini apewi karipio hata anaposema mambo yanayo kidhalilisha chama au ndo CCM wanaishi kikambare kila mtu ana ndevu hajulikani mtoto wala mkubwa
 
Achana nae huyo mlopokaji wa magamba. Ipo siku atayalamba matapishi yake. Mi naona anaitamani sana nafasi ya ubunge hata wa kuteuliwa maana anaona kijana Januari Makamba kalamba dume. Sasa inabidi ajipigie debe kwa kuropoka chochote ili amfurahishe JK labda anaweza akaambulia chochote. Anajitafutia uhalali wa kuendelea kuwepo kwa nguvu (looking for political legitimacy) kumbe ndani ya CCM yenyewe hajui kuwa yeye ni reject kwa wazee. Atabaki kuishi kwa matumaini hadi atachakaa. Akija kusituka kujifunika shuka itakuwa tayari ni asubuhi. Ni bora akae kimya, hiyo ndo inaweza kumpa heshima anglau.
 
Jamani uyo ni vuvuzela ajiulize kwanza wakati Wa ufisadi ulipoanza lowasa alijiuzulu uwaziri mkuu baadae Kamati kuu ya cc ikakaa wakaamua wavue gamba wote waliousika akiwemo rostam ,chenge na lowasa wakimaanisha wajiuzulu nafasi zao zote ukiwa na ubunge rostam akaachia wengine ikashindikana sasa mwulizeni uyu nape (vuvuzela)hawa magamba sta wameongezeka Kama wale Wa kwanza walikuwa wanaua chama na wameshindwa kuwatoa vipi hawa Sita waliomwagwa na rais juzi wateafanyaje yeye na cc Yao je si ndio chama kinaukata na kupoteza dira.
 
Nape, tunakuruhusu ongea yote yanayokusibu kwani chama kinajichuja mafisadi wanabaki wasafi wanaondoka. Hata wewe utaondoka najua kwa sasa unatimiza tu wajibu.
 
Well said, wape wape hao vilaza vidonge vyao. Leo nimeamini kwa mara nyingine kuwa Nape mwana wa Nnauye ni jembe.."WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
Sijaona makosa kwenye maneno yake. As far as CCM is concerned, taratibu za CHAMA NI RUSHWA, rejea kauli za Katibu mkuu wao Bw. Mangula alivyosema baada ya kushindwa kwenye chaguzi zao za ndani...

NAPE YUKO SAHIHI, CHAMA CHENYE TARATIBU ZA RUSHWA HATUKIWEZI!
 
Back
Top Bottom