Nape: Ushindi Igunga si kipimo cha safari ya 2015

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Katibu mwenezi wa Chama cha Mapinduzi, Nape Mnauye, ameelezea kushangazwa kwake na Watanzania ambao wamekuwa wazichukulia chaguzi mbalimbali ndogo ndogo zinazoendelea katika sehemu mbalimbali nchini kama msingi wa kujadili hatma ya chama chake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Mnauye, ameyasema hayo katika mahojiano ya moja kwa moja kati yake na Jukwaa Huru kwa njia ya simu wakati alipokuwa akiongelea juu ya uchaguzi uliofanyika wikiendi iliyopita katika jimbo la Igunga ambapo mgombea wao alishinda na hivyo CCM kulirejesha jimbo hilo chini ya himaya yake.

Akielezea ushindi walioupata Igunga, katibu mwenezi huyo alisema kuwa hiyo ni ishara nyingine ya kwamba Watanzania bado wangali na imani na CCM licha ya ukweli kuwa kumekuwepo na kile alichokiita "kelele toka kwa watu wenye kujiita wapinzani" kutoka kona mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Bonyeza link hapo chini kusikiliza mahojiano hayo kama yalivyofanywa na mmoja wa waundaji wa kikosi cha Jukwaa Huru, kisha kama una maoni usisite kuyawasilisha na kama kuna ulazima wa kurejea kwa katibu mwenezi wa CCM, bilashaka Jukwaa Huru litafanya hivyo.

EXCLUSIVE INTERVIEW: Nape; ushindi Igunga si kipimo cha safari ya 2015 – Maskani ya uchambuzi yakinifu
 
Back
Top Bottom