Kafara
JF-Expert Member
- Feb 17, 2007
- 1,396
- 411
Samahanini kwa kuchelewa kuingia,foleni kiasi Dar!
Lakini kipekee na kwa heshima kubwa namshukuru sana sana Ndugu yangu John Mnyika kwa kuingia na kuamua kuweka mambo sawa hapa ili mjadala uendelee vizuri!
Nilitumia neno KUROPOKA kwasababu nlikosa neno sahihi la kumwambia anayeponda/kusema na hasa yale ambayo kwakweli hayakutokea,tena anayasema kama vile ameyashuhudia kwa macho na masikio yake. Kama kuna mtu KAKWAZIKA kwa neno hilo samahani sana sijakusudia kudharau mchango wa mtu yeyote hapa JF,hata wale ambao kila wakiingia hapa hawataona jema la Nape, nao ni mtazamo wao,nawashukuru,kwani pengine kwa kusema hayo huniwezesha kujiangalia vizuri niko aawa au la.
Sasa ntajibu moja baada ya jingine,karibuni kwa mjadala.
shukurani kwa kuonyesha ustaarabu. huu ndio uungwana