Nape Nnauye: Toka moyoni mwangu

kisipoondoka na nyumba kitaondoka na PM, mkuu ni wapi huko alikozomewa?

Geita huko, wananchi wa kata ya Nkome walimzomea sana hadi kutaka kumtia vidole machoni ikabidi akimbie na wapambe wake. Na wakamwambia asirudi tena huko na hawamtambui tena.
 
Lakini kuna watu si watafiti kazi yao ni kushabikia tu kama mazuzu, kwani ile kamati ya mashirika ya uma ni ya chadema au ni ya Bunge? CAG ni wa chadema au wa Serikali. Tambua hayo kwanza kuliko kuandika upuuzi wako wa kichadema hapa. @ duble.

Baada ya kuwekwa mezani nani akalishikia kidedea ili usiwe upepo bali liwe dhoruba? Na nani akaendelea kuongea tu bila matendo? Nani akafunika kikombe ili mwanaharamu apite?
 
Kamanda NAKUSHUKURU KWA KUSAHIHISHA NA KUELEZA UKWELI, DUBLE ALITAKA KUPOTOSHA UKWELI MAKUSUDI'........
Napelaga Tofauti ya JF na FB Ni FB unachagua marafiki(Wanaokusifia) na kuwakataa wale wanakuambia ukweli ambao wewe hutaki!Hapa JF pipo are dare to talk open(Uongo,Unafiki mwiko).

Mytake: Nikiona Kauli za viongozi na maka wa CCM huwa nakumbuka huu msemo!"When the character of a Nape is not clear to you, look at his boss".
 
Kwakuwa mnalipwa kunitukana hapa ndo maana mnaamini kila mtu analipwa kwa kila afanyalo hata kwenda uwani analipwa
...mkuu kama haya unajitolea basi una moyo mgumu. Uenezi unafanya bure wewe!?Hongera.
 
kazi yake inadefine anachosema..VUVUZELA!! hata kama wameelemewa.!!
yeye anasema akina mwita wanalipwa je yeye ile kazi yake majukwaani halipwi?
 
[LIST said:
[*] Nape Nnauye TAKWIMU ZINAONYESHA KINONDONI PEKEAKE TENA KWENYE MATAWI TU ACHILIA MBALI KATA NA WILAYA TUNAO MAPROFESA, WANAJESHI WASTAAFU, MA DOCTARI, GRADUATES NK WAMEGOMBEA , ANAYEDANGANYA ETI WATU HAWATAKI KUJAZA FOMU NANI?38 minutes ago
[/LIST]

Mmmh, hao madokta na maprofessor watakuwa ni aina ya akina Dr Bana, waganga njaa. Sidhani kama Dokta wa kusomea kabisa ambaye yupo busy na shughuli zake atakaa chini afikirie kuwa balozi au hata diwani kwa tiketi ya CCM hivi sasa. Labda ubongo wake uwe umeshake kidogo.
 
Safi sana nape, hawa wamefanya jf kama hati miliki ya chadema msikate tamaa hakuna kizuri kikachokuja bila vikwazo

haya ya nape c majibu ni maswali,usifananishe kinondoni na arumeru,huku mashina yenu yameng'oka
 
Sina haja ya kunukuu maneno yaliyoandikwa kwenye vitabu wakati sijazaliwa. hebu twende hapo Iraq tu, baada ya majeshi ya Marekani kuiteka Baghdad lakini bado yule waziri wa Habari Al Sahaf alikuwa na ushuja wa kijinga na kujisifu kwamba hakuna hata Mmarekani mmoja atakaekanyaga Baghdad na Baghdad ndio litakuwa kaburi lao na kwamba Baghdad ilikuwa haijatekwa!!

Lakini ukweli halisi yule jamaa mpaka sasa anaishi uhamishoni, sasa Nape ni mganga njaa tu, subilini kwenye uchaguzi wao wa ndani mwaka huu JK amuweke kando hamtoamini masikio yenu.

Nape ni mtu ambaye hajui alifanyalo na nadhani bado hamfahamu vyema JK kwamba anaweza kuteuwa sura mpya kwenye CCM Taifa baadaye mwaka huu, na ndio mtawajuwa walivyo wanafki hawa vVijana wazee.

Jk mwenyewe atapigwa kando!
 
Nnauye Junior badala ya kughadhabika huu ulikuwa uwanja wako wa kuflow na majibu ya kihoja na kuonyesha uwezo wako wa ufahamu na uongozi.ni fursa pia ya kupokea maoni tofauti na kuyafanyia kazi.ama ulitaka hoja zako zipigiwe makofi na nyimbo za kidumu chama cha mafisango?

Take your cup of coffee na uje ushushe mistari..angalia mifano ya Dr W.Slaa anaposhiriki mijadala humu...achana na kujidanganya fb usijepata kesi ya under 18 huko
 
Huyu ni miongoni mwanasiasa machachari tena adimu aliye na bahati ya kufanyia kazi zake gizani huku akishirikiana kwa karibu sana na vipofu na kuongozwa na sera zilizoandikwa kwa dead language ya kiyunani na kiebrania, itamchukua kerne nyingi kutambua alipo na kuipata njia sahihi kuelekea mlango uloandikwa revolution/ movement 4 change
 
Nape ni katibu mwenezi wa madudu majambazi na wezi. CCM tuliyoijua siyo hii. Mie naomba siku akimfuata Millya tumgomee kumpokea ikiwezekana tuseme kama Lusinde "Kudadadeki......tukuchane tusikuchane..... Tukuchane......." Afie hukohuko kwa magamba. Hana adabu kwa watz. Kwanza anaweza kuwa Freemason si mnaona cheni ya freemason shingoni. Mnaongea na pepo au shetani Luthifer" Angalieni lisiwarukie. Mie natoka mtandaoni lisini-cameroon.
 
[*] Nape Nnauye HIVI NI UJANJA MTU KUHAMA CHAMA NA CHAMA KINGINE KIKAMPOKEA AU CHAMA MAKINI KITAJIKITA KUTAFUTA WANACHAMA WAPYA KUTOKA KUNDI KUBWA LA WATANZANIA WASIO KUWA NA VYAMA??? UNAJIKITA KUCHUKUA SCREPERS?!!!!!!41 minutes ago



yaani hata kuandika SCRAPER imemshinda ..... huyu sio kiongozi

YAANI NIMECHEKA hadi machozi yamintoka .. 'Haya sema CHUMA CHAKAVU '....'SHUMA SHAKAVU' lala chini ulambwe viboko .. Ingilishi ikushinde Na kiingredha nacho ushindwe ???!!sasa isitoshe hata kimombo huwezi basi wewe bure babisaa Na hili ni balaa.. Sasa waliosoma shule za wageni kiingredha cha ingilishi taabu namna hii sasa sisi Wa shule za kata tusemeje..
 
Mimi ningeomba anijibu kati ya CCM na CDM ni yupi anayecheza ngoma ya mwenzake?

Watakujibu kuwa Serekari ya CCM ni sikivu kwa wananchi ndio maana wanatekeleza ilani ya CDM. Ila wamechemka kwenye kucopy hoja ya CUF ya maakama ya Kadhi.
 
CCM = Chama Cha Majambazi/Mauaji/Mipasho
Tutaongea, tutagombana, tutatukanana mpaka mate yatakauka mdomoni mambo yatakuwa yaleyale.
Tatizo sio mawaziri, hata akivunja baraza la mawaziri kila mwaka haitasaidia kitu, ujambazi utaendelea kama kawa
Tatizo ni yeye mwenyewe JK, alipata urais kisanii na kifisadi (Kagoda etc), anaendesha nchi kisanii, anateua wasanii kisanii nao wanamfanyia na kutufanyia usanii; usanii unaendelea kama kawa mpaka 2015 atakapotoka
Kazi ipo!
 
hicho kilikuwa chama cha baba , hizo sera zako sio mahali pake hapo. Hizo ni sera safi sana hazistahili CCM hata kidogo
 
Kwakuwa mnalipwa kunitukana hapa ndo maana mnaamini kila mtu analipwa kwa kila afanyalo hata kwenda uwani analipwa
Mkuu sijui mpwa wako Benjamini au Baraka (kama anapita JF)atajisikiaje kusoma hii sentesi!!
Utasema eti hizi ni mbinu na lugha za kisiasa!!!No!
Siasa ni sayansi.Hamkusoma hivyo Kivukoni Chuo cha Chama miaka hiyo?
Hiyo kauli haibebi taswira ya 'Binadamu wote ni ndugu zangu'.
Ulikuwa na maneno zaidi ya 100 kutumia kumjibu mhusika bila kulazimika kutumia hayo maneno uliyotumia.

Kuhusu wanachama 'SRAPERS' kama wakuu walivyokusahihisha,hujaweza kufafanua ukaeleweka.
Katika siasa tunachojali ni idadi na ubora.Unapopata 'kondoo' mpya,hakuna muda wa kujiuliza kondoo huyo alikuwa chama gani kabla..Hata kama kujua hilo ni muhimu, hilo huja baadaye na wala haliwezi kuwa kipaumbele cha kwanza.
Yesu Kristo alitumia mkakati huo huo...aliwafuata watoza ushuru,wasio na elimu ,makahaba na mafarisayo..na alipowageuza nia zao hakujali tena historia zao,na wote wakawa na hadhi na fursa sawa katika ufalme mpya.Petro,asiye na elimu,alikuja kuwa MWAMBA imara wa kanisa la Kristo.
Ndio maana wewe Nape,pamoja na vyeo vyako,bila kujali Digrii yako ya UZAMILI linapokuja suala la kupiga kura, unaruhusiwa kupiga kura MOJA tu ,sawa na mama muuza supu sokoni.
Watu hutofautiana vipaji na karama.Vivyo hivyo ushawishi.Tunapopata mtu moja au wawili wenye ushawishi toka chama fulani ni furaha kwetu maana tunakuwa na uhakika wa kuwavutia wale akina mama wauza supu zaidi kuwa wanachama na hatimaye kuwa wapiga kura.
Kwa mfano,CHADEMA ikimpata LUSINDE itakuwa imepata hasara,lakini itapata faida kwa kumpata DEO FILIKUNJOMBE!
Right?
 
Back
Top Bottom