Nape Nnauye nae kaibukia kanisa la ufufuo na uzima......

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
...Ametoa neno kwenye kanisa la ufufuo na uzima leo kuhusu rushwa na kusema kuwa viongozi wamekosa huruma kwa wananchi na wamekosa Mungu ndani yao.Amedai yeye sio mgeni kwenye kanisa hili la Gwajima na ameonyeshwa kukerwa na rushwa.

...Naona siasa na kanisa zinaendelea kupamba moto,ungemuona Nape ungesema kuwa ameanza kuwa mchungaji,alikuwa anaongea mpaka povu linamtoka mdomoni.

Source : TBC 1
 
Anawapinga kina mzee wa theluji wakialikwa makanisani lakini naye kumbe yumo. Anajaribu kurudisha imani ya wananchi kwa CCM
 
Hawa si ndio walisema watumishi wa Mungu wanaleta uchochezi? Imekuache sasa wameanza kukimbilia makanisani, kama wakienda huko watubu maovu wanayowatendea watanzania. Watanzania sasa hivi kimbilio letu ni makanisani tunajaribu kupata faraja ya maisha maana serikali ya CCM imeshindwa kuleta maisha bora. Nape na wenzake watubu uovu huo hivi huyo Gwajima hajamsalisha sala ya toba?
 
huyu kijana nahisi hangover hua zinamsumbua..hana nidhamu..niki relate zile kauli zake za kushikishwa ukuta, chadema chama cha wachaga..mara hutumika kama messenger kwenye vikao vya ndani vya chama na hutumwa tumwa bia yani namuona bonge la tapeli..na uso wake ulivo kama dalali sasa!!

mimi naishi mikocheni na leo ile ibada ilikua ndefu sana maana nilikkua naskia makelele ..

nna mpango wa kumshitaki Gwajima kwa Noisy Polution kuna mwanamke mmoja hua ana rap pale..sauti mbayaa kama Ana Abdala

Kweli kusoma si kuelimika..nafikiri psychology aliosomea haimsaidii...HEE SIKUJUA..KUMBE SISQO kawa balozi wa Bongo Malaysia..Hatareee
 
ukiwa katibu mwenezi wa ccm unawezakusema lolote. Hata usiloamini! Unaweza hata kukana jinsia yako. Kazi yako si kueneza tuu? Ndo Nape!
 
...Ametoa neno kwenye kanisa la ufufuo na uzima leo kuhusu rushwa na kusema kuwa viongozi wamekosa huruma kwa wananchi na wamekosa Mungu ndani yao.Amedai yeye sio mgeni kwenye kanisa hili la Gwajima na ameonyeshwa kukerwa na rushwa.

...Naona siasa na kanisa zinaendelea kupamba moto,ungemuona Nape ungesema kuwa ameanza kuwa mchungaji,alikuwa anaongea mpaka povu linamtoka mdomoni.

Nepi naye aache unafiki, rushwa ipi ina mkera? Hao mabosi wake ndo wala rushwa wakubwa kama inamkera basi asingekua chini yao

Kama Nape au mpambe wake anasoma hapa naomba watafute namna huyu bwana apate voice-couching. Nape anaongea kama mchiriku. Public communications iko kushoto kabisa kwa huyu dogo, sauti kali sana, ataharibu masikio ya watu!
 
Sielewi moyoni mwa nape nauye huwa kukoje anapozungumzia, rushwa, matumizi mabaya ya rasilimali, viongozi kutokuwa na hofu ya Mungu, kutokutenda haki nk. Hivi kweli anayoyazungumza analenga kufikisha ujumbe au ndo funika kombe mwana.......,
 
Ukemeaji rushwa uambatane na vitendo; kila anayeshiriki akamatwe na kufungwa. Siasa za bara letu hili ni maneno ya jukwaani tu; Nape aje humu atuambie hiyo chuki yake dhidi ya rushwa imeanza lini na imezaa matunda gani, na je, ni chuki ya chama chake dhidi ya rushwa au chuki yake yeye binafsi?
 
Bila kumsema nape naona huwa mnapungua uzito. Si mseme na wenezi wenu? Kila siku mnasema nape aliwakosea nini? Hamna kitu cha kufanya ni hiyo? Hivi kichwani mna ubongo au kamasi?
 
kakemea maovu ni jambo jema, hata kama halikutoka moyoni lakini alitumia jukwaa hilo kuwaasa wasikilizaji. kwenda kanisani si kosa labda kama angetumia kanisa kutukana dini nyingine.

Mimi nawaogopa zaidi wanasiasa wanaotembelea makanisa na misikiti kwa kificho wakiwa na mambo mabaya kuliko wanaokwenda wazi na tukasikia wamefanya nini kwenye nyumba za ibada.
 
Jamani , Nape nae mtanzania anayo haki ya kwenda jumba lolote la ibada na kusali kutokana na imani yake,tusiweke siasa kwa kila jambo,hongera sana Nape kwa kusali hakika mungu yu pamoja nawe na CCM imepata kiongozi mchamungu!
 
kinachonishangaza siku zote hadi siwaelewi vizuri hawa watu ni;
  • Wao ndiyo wameshika/wanatawala nchi chini ya utawala wa sheria na sheria zipo wazi
  • mafisadi wote wapo nao ndani ya chama
  • kila siku wanalalamika sasa sisi tufanyeje (tusiwachague mbona wao wanatuletea na kuwasifia)
 
Hili ndilo swali nililo nalo moyoni kila siku ninapowasikia majukwaani viongozi wa CCM na watawala wa serkali wakilalamika juu ya rushwa.
 
Kanisa la ufufuo la bwana Gwajima a.k.a Kanisa la Misukule limegeuka kuwa jukwaa la kisiasa. Gwajima ana mpango wa kumpeleka mwanasiasa madhabahuni kila Jumapili. Siku ya tarehe 05.02.2012 kanisa lilipambwa na rangi za chama tawala. Aliwaambia waumini wake kuwa tarehe 12.02.2012 wangekuwa na mheshimiwa Rais kanisani! Gwajima naye kwa uongo yuko juu. Alianza kwa kusema angemfufua Amina Chifupa wakati huo kanisa lake lipo pale Ubungo kabla ya kuhamia Tanganyika Packers.
 
Bila kumsema nape naona huwa mnapungua uzito. Si mseme na wenezi wenu? Kila siku mnasema nape aliwakosea nini? Hamna kitu cha kufanya ni hiyo? Hivi kichwani mna ubongo au kamasi?

Hivi wewe unaweza ukafananisha katibu mwenezi wa CDM bro Mnyika na Nape? Yaani kama kufananisha Tingatinga na Bajaji au Man U na JKT Oljoro.Huyu katibu mwenezi wa CCM kabadilika kutoka mwenezi kwenda katibu mropokaji..jamaa anaongea mno kila siku kwenye media tu.Akisikia EL kaongea nae anatafuta cha kusema.Halafu uwa hajui wapi hatumie sauti ya utulivu wapi hatumie nguvu..yeye muda wote ni kupiga kelele tu.
 
Kanisa la ufufuo la bwana Gwajima a.k.a Kanisa la Misukule limegeuka kuwa jukwaa la kisiasa. Gwajima ana mpango wa kumpeleka mwanasiasa madhabahuni kila Jumapili. Siku ya tarehe 05.02.2012 kanisa lilipambwa na rangi za chama tawala. Aliwaambia waumini wake kuwa tarehe 12.02.2012 wangekuwa na mheshimiwa Rais kanisani! Gwajima naye kwa uongo yuko juu. Alianza kwa kusema angemfufua Amina Chifupa wakati huo kanisa lake lipo pale Ubungo kabla ya kuhamia Tanganyika Packers.

Anataka kuiga ya Pastor Joshua wa Nigeria...na yeye ataanza kuleta unabii muda si mrefu,wanasiasa na dini wapi na wapi bwna? Yeye hawaalike waje kusikiliza neno na sio kutoa neno.
 
...Ametoa neno kwenye kanisa la ufufuo na uzima leo kuhusu rushwa na kusema kuwa viongozi wamekosa huruma kwa wananchi na wamekosa Mungu ndani yao.Amedai yeye sio mgeni kwenye kanisa hili la Gwajima na ameonyeshwa kukerwa na rushwa.

...Naona siasa na kanisa zinaendelea kupamba moto,ungemuona Nape ungesema kuwa ameanza kuwa mchungaji,alikuwa anaongea mpaka povu linamtoka mdomoni.

Source : TBC 1

GWAJIMA@ Mzee wa misukule feki; hivi bado kuna kondoo wanamuamini na kupeleka fungu la 10? WAJINGA NDIO .........
 
Back
Top Bottom