nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
Na Irene Mark
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amesema chama hicho kimejipanga kutumia rasilimali zake zenye thamani ya zaidi ya sh bilioni 50 kujiimarisha kiuchumi ili kupunguza utegemezi wa ruzuku.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi ndogo za chama hicho jijini Dar es Salaam jana, Nape alisema wamewaalika wafanyabiashara 30 wa Chama cha African National Congress (ANC) cha Afrika Kusini, ili kujifunza namna ya kutumia vema rasilimali za CCM.
Alisema ujio wa wafanyabiashara hao wa ANC ni sehemu ya mageuzi ndani ya chama chao na kwamba wataingia nchini leo kwa ziara ya siku tano ambapo watashiriki kongamano la kibiashara lililoandaliwa na Tanzania Chamber of Commerce, Industries and Agriculture (TCCIA).
"Itakumbukwa kuwa katika maamuzi ya kufanya mageuzi ndani ya chama yanayoendelea, Chama Cha Mapinduzi kiliamua kuongeza juhudi katika kukifanya chama kipunguze au kumaliza kabisa utegemezi wa ruzuku katika kuendesha mambo yake.
"Hivyo basi, ziara hii ni sehemu ya utekelezaji wa maamuzi hayo… lengo ni kujipanua kiuchumi na kujifunza namna bora ya kuwekeza hasa tukizingatia kuwa ANC ni chama kikongwe kwenye siasa barani Afrika hivyo wenzetu wana uzoefu zaidi.
"Wakati wenzetu wanachangishana kuendesha vyama vyao sisi tutawekeza," alisisitiza Nape na kuongeza kwamba watatumia vema makampuni yanayomilikiwa na CCM.
Alibainisha kuwa malengo ya ziara hiyo ni kutafuta fursa mbalimbali za uwekezaji zitakazodumisha na kuendeleza uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya ANC na CCM ikiwemo kubadilishana uzoefu wa makampuni ya vyama hivyo.
Alisema wafanyabiashara hao watatembelea kambi za Mazimbu mkoani Morogoro zilizotumika kuandaa wapigania uhuru wa ANC wakati wa harakati za ukombozi wa nchi yao.
Alisema wataalamu mbalimbali wa CCM na jumuiya zake watashiriki kwenye ziara hiyo ili kujifunza na kupata uzoefu katika uanzishaji, usimamizi na uendeshaji wa vitega uchumi vya chama.