nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
Katibu Mwenezi wa CCM Taifa Nape Nauye, alisema wakati umefika kwa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara Zanzibar (JUMIKI) kufutwa na mrajisi wa serikali Zanzibar. Kwani kuwepo kwa kundi hilo kuna zidi kuhahatarisha amani na umoja wa kitaifa tangu kuvamia shughuli za kisiasa Zanzibar.
Naye Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa amethibitisha kuwepo na vurgu katika eneo la Rahaleo majira y
a saa 1 usiku juzi baada ya kufanya maandamano wakitoka kwenye mhadhara katika Msikiti wa Msumbiji Magonakubwa na kupelekea majengo likiwemo tawi la CCM kuchomwa moto, thamani ya nyumba na bendera ya CCM. Uvamizi huo umesababisha uharibifu mkubwa wa mali na kituo cha umeme kunusurika kuwaka moto wakimwaga mafuta ya petroli katika jengo la ghala la kuhifadhia samani za nyumba na kuchoma moto pamoja na bendera ya Chama cha Mapinduzi.
Inasadikiwa Mashambulizi haya yamefanyika kwa siraha za jadi na mawe. Naye katibu ameomba kufanyika uchunguzi wa kina baada ya kukana kuusika kwa kundi lake katika sakata ahilo.
Kadhalika Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja Kanali mstaafu Mahamoud Mzee alisema kitendo kilichofanywa na wafuasi wa Uamsho hakikubaliki mbele ya sheria. Alisema Zanzibar inaweza kuingia katika vurugu kubwa kama wananchi wataamua kuchukua sheria mkononi kupambana na watu wanaofanya vurugu. Ikumbukwe ni Mwezi Mei mwaka huu Jumuiya hiyo pia ilihusishwa na vurugu za ku choma makanisa na baa, visiwani humo.
Source; Mwanza Indigenous Society