Nape ni mwanzilishi wa CCJ

Sijaona unafiki wowote wa MPENDAZOE kwa maana mtu mnafiki ni yule anayejifanya kuwa na mawazo sawa na aliko ilihari anafanya mambo yanayopingana na alipo. Sasa kama azima ilikuwa ni kuondoka CCM basi Mpendazoe alifanikisha hilo na ana kila sababu ya kupongezwa kwa kuyakimbia maozo ya CCM na kutafuta mahari pa kuweza kutafuta usawa katika kuliendeleza taifa. Huyo Nape ndo mnafiki na ataendelea kuwa mnafiki kwa maana aliyajua yaliyo mabaya ya CCM na akata kuondoka kwa sababu ana uchu wa Madaraka kama walivyosema hapo juu aliamua kubaki humo ndani na huku roho yake ikimsunta kuwa mahari alipo si mahari pema hata kidogo.

Mpendazoe hakuondoka CCJ kwa sababu ya kutapatapa ila kwa hira walizofanyiwa na msajili wa vyama vya siasa anayeongozwa na fikra pungufu na zinazokufa kila kukicha za CCM kwa kukihujumu chama cha CCJ. Sasa kwa mpiganaji kama unaona sehemu moja unayojaribu inashindikana unatafuta another alternative. Upiganaji wa Mpendazoe ndo huo tunaouona wa kuweza kutafuta in anyhow njia ya kuweza kuwatumikia watanzania katika chama chenye mwelekeo wa kulikomboa taifa.

Kwa tafsiri yako ulitaka abaki kwenye chama ambacho Tendwa aliapa na Makamba kwamba hakitaweza kusajiliwa Tanzania. Hiyo ni sawa na mvuvi hodari aliye baharini baada ya dhoruba kutokea na mtumbwi wake kutobolewa kubaki humo eti aoneshe uhodari wake ilihari mtumbwi unazama. Ataonesha uhodari wake kwa kuogelea na kutafuta mitumbwi isiyozama ili aendeleze uhodari wake wa uvuvi. Kabla hajafanya hivyo hufanya awezalo ili auzibe lakini kama haiwezekani huondoka kusalimisha maisha yake na uhodari wake kama alivyofanya Mpendazoe alipopigana kukiokoa CCJ lakini kwa sababu juhudi zake zilishindwa na nguvu ya Dora akaamua kuogelea kutafuta mitumbwi isiyozama ingawa wengine wasiohodari walienda kwenye mitumbwi iiliyotota na ambayo itazama muda si mrefu(Mwenyekiti CCJ= CCM)

Nakubaliana na wewe kwenye blue. Na kwa msingi huo huo ni vizuri ukaelewa na Mpendazoe akaelewa kwamba hiyo revelation aliyoifanya kuhusu Nape haina tija kwa sababu hata hiyo ndege yenyewe haikuwahi kufanya take off. Mpendazoe anaelewa kwamba CCJ was supposed to be an association of like minded people who felt let down na namna CCM ilivyokuwa inashughulikia mambo muhimu hasa suala la ufisadi na mafisadi. Kama Nape alikuwa naye ana-share msimamo huo huo ni jambo la kupongezwa kwa kuchukia ufisadi na kwa ku-maintain consistency yake katika suala hilo hata baada ya kupewa wadhifa huu. Ndiyo maana narudia kwamba mpaka hapo sioni dhambi ya Nape kiasi cha kuwa ni scoop ya kuripotiwa kwenye gazeti au kuwa-treat nayo wakazi wa Mbamba Bay.
 
Mi naona Nape ni "buluguja" hana vission yeye anatafuta kutoka hivyo yupo tayari kupenyeza kila shimo ilimradi atoke.
 
Pamoja na 'revelations' hizi kuonesha Nnape ni mwanasiasa/mtu wa namna gani naamini pia inaonesha Fred Mpendazoe ni mwanasiasa/mtu wa namna gani! Kwangu mimi, wote si wanasiasa/watu wa kuaminika!
 
Kwa hiyo unachotuambia ni nini? Fine alikuwa mwanzilishi wa CCJ then what. Kwa sababu hata yeye alishiriki akiwa bado yuko CCM, je huo siyo unafiki. Kwa nini hakubaki ndani ya CCJ ili aijenge na kuifanya iwe maarufu badala ya kuhamia CDM? Hivi vyama ni kama mitumbwi ya kukuvusha ng'ambo kwa usalama. Lakini lililo la msingi ni kwamba yeye Nape yuko CCM na anatetea sera au misimamo ya chama chake , kama ambavyo na yeye Mpendazoe ana haki ya kutetea sera na misimamo ya Chadema.

Hii siyo contest ya loyalty kwa chama hiki au kile, na ndiyo maana leo tunaona mwanasiasa huyu yuko kule na kesho yuko huku. Hata hiyo loyalty hupimwa wakati ukiwa ndani ya hicho chama na siyo baada ya kuondoka. Je Mpendazoe anataka kutuambia kwamba alipokuwa CCM kwa miaka yote hii hakuwa na loyalty na kwamba jicho lake lilikuwa kwenye upinzani? Naweza kuelewa frustrations za Mpendazoe hasa baada ya vigogo wenzanke kumchuuza ahame na wenzake watamfuata halafu wakamtosa lakini in politics kupima upepo huwa imo. Nani alijua leo hii Ntagazwa angekuwa huko aliko au Dr. Slaa huyu? Katika siasa haya yote hutokea na yanapotokea mtu hutakiwa kila la heri kule aendako na akishindwa na kurudi hasutwi. Waone Makongoro Nyerere, Wasira, Nsazugwanko na hao akina Mpendazoe, Shibuda, Kahigi, Slaa, Ntagazwa na wengine wengi.
wewe mtetezi wake huwezi kuona tatizo sababu wote mnaongozwa na njaa wengine wanaongzwa na nia na dhamira ndio maana Mpendazoe anashangaa nape yule yule leo amegeuka na kuanza kumsifia jk aliyekua anamtukana kwamba hana uwezo wa kuongoza ama baada ya kupewa ukuu wa wilaya tu na kupewa uenezi mara uwezo wa jk umepanda ghafla Biblia inasema heri adui kuliko mnafiki nape ni hatari kwa taifa anaweza kufanya chochote ili apate madaraka, hongera cdm kwa kuzidi kuwaanika hawa wachumia tumbo ili umma uwajue, ndio maana alichukua pesa kwa jeetu patel kwa ajili ya kampeini zake za nec
 
Kwa hili tukimpata MKJJ atatuambia ukweli zaidi maana yeye alikuwa karibu sana na CCJ wakati huo na alikuwa mtu wa kwanza kutuletea katiba ya CCJ kama sikosei.

Kuhusu Nape nilijua jua halitakuchwa kabla jogoo hajawika na kweli ameanza kuwika tunasubiri awike tena mara ya pili na ya tatu ili kuchwe kabisa tuone kila kitu. Namjua Nape toka UVCCM ni mhangaikaji atatafuta popote pale ili afanikishe anachokitaka ndiyo maana alipobwagwa ubungo akajaribu bahati yake Chadema. Mtu kama huyu kurubuniwa ni rahisi sana unaweza kumchezea unavyotaka kama tu utakuwa unatimizia kile anahitaji. Kwa vita aliyoianzisha Nape itakuwa ngumu sana kwake kuishinda maana amezungukwa na maadui watatu kwa pande zote, ingekuwa ni maadui wa nje tu ningesema angeshinda lakini maadui wake si wa nje wala Chadema ni wa ndani ya chama.

Sote tunajua vita vyake na UVCCM kabla ya kuishinda hiyo akapewa nyingine ambayo ndiyo ngumu zaidi ya RACHEL ambayo hata mwenyekiti mwenyewe haiwezi sasa leo ameambiwa yeye ndiye amfunge paka kengere kwa ahadi ya kwamba tuko pamoja 'maneno yako ni yangu' lakini najua siku ya siku ataambiwa yale maneno ni yako, sote ni mashuhuda zile siku 90 zilitamkwa na Msekwa mwenyewe kule Dodoma lakini wenzake walipoona maji marefu akaambiwa hayo hayakuwa maazimio ya NEC. So nachoweza kusema ndugu yangu Nape watch out people are watching you wenzako watakuja kukukana very soon chaos.
 
- This is very interesting, maana looking at the times lini CCJ ilikufa na lini Nape ameenda kuwa DC Masasi haikubaliani kabisa, however Mpendazoe angeenda mbele zaidi kwamba anamuonaje Marando? Mtei ambaye naye alitokea CCM? anamuonaje Dr. Slaa ambaye naye alitokea CCM na alijitoa tu baada ya kunyimwa nafasi ya kugombea ubunge Karatu? anamuonaje Shibuda? Seif Hamadi? Na yeye mwenyewe anajionaje?

- Point yake ni nini hasa kwamba ni makosa kwa kiongozi kubadili au kutaka kubadili mawazo ya kisiasa? I am lost hapa!
, I mean talking about unafiki wa kisiasa? Nani ni mnafiki hapa?

William @ NYC, USA.
 
Yeye Nape amewaambia kabisa kawaulizeni jinsi kilivyo kufa. Hii statement nayo ni ngumu.Nafikiri alikuwa mamuluki kuwamaliza akina mpandazoe na ccj. Ndo maana amezawadiwa vyeo kwa kazi mzuri.
 
- This is very interesting, maana looking at the times lini CCJ ilikufa na lini Nape ameenda kuwa DC Masasi haikubaliani kabisa, however Mpendazoe angeenda mbele zaidi kwamba anamuonaje Marando? Mtei ambaye naye alitokea CCM? anamuonaje Dr. Slaa ambaye naye alitokea CCM na alijitoa tu baada ya kunyimwa nafasi ya kugombea ubunge Karatu? anamuonaje Shibuda? Seif Hamadi? Na yeye mwenyewe anajionaje?

- Point yake ni nini hasa kwamba ni makosa kwa kiongozi kubadili au kutaka kubadili mawazo ya kisiasa? I am lost hapa!, I mean talking about unafiki wa kisiasa? Nani ni mnafiki hapa?

William @ NYC, USA.
Hapa Mpendazoe anaongelea unafiki wa wanaojidai wapambanaji na kumkashifi mwenyekiti wao kama Nape na kubakia humo humo, hawa unaowataja kina Mtei, Seif, Marando, Shibuda, Slaa walipotofautiana na CCM kwani walibaki huko? wangebaki huko na wao tungewaita wanafiki kama Nape ndicho anachosema Mpendazoe.
 
Acha hoja za kitoto, ebu nionyeshe hapo alipopewa nafasi ya kuzijibu hizo tuhuma za EPA na Kuomba Kugombea Ubunge kwenye habari hii?

Nilichosema, kuna changamoto nyingi sana zinawazunguka watu wa Mbambabay na mazingira yao,hoja hizo zingezungumza zaidi zingewafanya watu wa Mbambabay walione tumaini la kesho kupitia Chadema, lakin kwa kuipoteza nafasi hiyo kwa kumuongelea CCJ ambaye ata hawamjui ni kitu gani,ni kuipoteza nafasi hiyo muhimu. Ni muhimu sana kuyasoma mazingira ya watu.

Wewe ndio mtoto, hukufuatilia alivyojibu kuwa yeye ndio aliombwa na Chadema? Gazeti hili la mwananchi ambalo habari yake tunaijadili hapa ndio waliompa nafasi ya kujitetea akajibu ulitaka warudie tena leo utetezi wa alhamisi?

Narudia tena tatizo ukiwa CCM akili unaficha kwenye mapaja.
Wananchi wa Mbamba bay wapo sawa na wale wa Ikungi Singida Mashariki alikotumia Nape kuituhumu Chadema na Dr Slaa. Labda kwa kuwaambia watu wa Singida mshahara wa Dr Slaa ndio aliwapa tumaini?

Watanzania wote wana haki ya kupewa taarifa, unaposema watu wa Mbamba Bay hawamjui Nape huwatendei haki na humtendei haki, kwamba huko hakuna vyombo vya habari?

Mlianza na ofisi za chadema kuwa uswahilini, mkasema nguvu ya umma ni ya wavuta bangi na jobless, mkasema vyama vya msimu, vya kichaga na leo unasema watu wa Mbamba Bay hawana haki ya kuwajuwa wanafiki kama Nape.

Rudisha network braza vinginevyo kama wewe ndio mtetezi wa CCM basi 2015 haitafika
 
Nape huyu ni mnafiki tu iweje atoe siri za nec kwa ccj kuwa wanataka kufukuza wanachama hadi mpendazoe akawa wa kwanza kujiondoa, leo ameaminiwa na ccm kuwa katibu wa itikadi basi kumbe mambo yote ya ccm yataanikwa tu huyo Nape
 
Hapa Mpendazoe anaongelea unafiki wa wanaojidai wapambanaji na kumkashifi mwenyekiti wao kama Nape na kubakia humo humo, hawa unaowataja kina Mtei, Seif, Marando, Shibuda, Slaa walipotofautiana na CCM kwani walibaki huko? wangebaki huko na wao tungewaita wanafiki kama Nape ndicho anachosema Mpendazoe.

- I mean ni Demokrasia at work, tatizo ni kama Mpendazoe kwa kujitoa CCM na kuingia Chadema amevunja sheria ya jamhuri au mnafiki, none ishu kama chama changu naona kinakosa mwelekeo ninayo haki ya kutumia kila njia za kisiasa kutafuta attention ya kusikilizwa na chama changu, kwani CCM haijui waliotaka kuanzisha CCJ?

- National politics ndivyo zinavyochezwa, CCM waliwajua sana wale wote walioshiriki CCJ, lakini inafanyika tathmin ya chama ya kisiasa, kuona umuhimu wao wakiachiwa watoke, chama kinaona haikwezi kua-afford, kwa hiyo wanaitwa na kuulizwa tatizo lao wanasema na sometimes wanapewa nafasi katika chama kurekebisha waanayoona hayafai, that is how national politics is played, Mpendazoe was not a threat to CCM wakamruhusu aondoke na wengine wote walioruhusiwa kuondoka, it has nothing to do na unafiki it is simply how national politics are played!

Es!
 
jamae, nape hayuko peke yake. Mnakumbuka kipindi kile jk anautaka urais? Ccm ilikaribia kuvunjika kwa tetesi kuwa jk angekihama. Hata hivyo si kama namtetea huyu dogo. Nataka kuonyesha unafiki wa siasa. Leo kauli za shitambala mnazisikia? Kauli za tambwe mnazisikia? Kauli za ngawaiya mnazisikia? N.k n.k. Jk alimaliza pale aliposema, akili za kuambiwa... Malizia[/QUOTE]
Changanya na za kwako
 
- I mean ni Demokrasia at work, tatizo ni kama Mpendazoe kwa kujitoa CCM na kuingia Chadema amevunja sheria ya jamhuri au mnafiki, none ishu kama chama changu naona kinakosa mwelekeo ninayo haki ya kutumia kila njia za kisiasa kutafuta attention ya kusikilizwa na chama changu, kwani CCM haijui waliotaka kuanzisha CCJ?

- National politics ndivyo zinavyochezwa, CCM waliwajua sana wale wote walioshiriki CCJ, lakini inafanyika tathmin ya chama ya kisiasa, kuona umuhimu wao wakiachiwa watoke, chama kinaona haikwezi kua-afford, kwa hiyo wanaitwa na kuulizwa tatizo lao wanasema na sometimes wanapewa nafasi katika chama kurekebisha waanayoona hayafai, that is how national politics is played, Mpendazoe was not a threat to CCM wakamruhusu aondoke na wengine wote walioruhusiwa kuondoka, it has nothing to do na unafiki it is simply how national politics are played!

Es!
haa haa MKuu naona unajitahidi kuwa mtetezi saana wa magamba mapya hongera.
lakini tusikimbiane mkuu tena siku zijazo.
 
kati ya vitu ambavyo haviwezi kuvumilika katika jamii ya waungwana ni usaliti, tuhuma ambazo zimetolewa na fredy mpendazoe za kuwa wewe ni mmoja wa waanzilishi wa ccj ni mbaya mbaya na mbaya zaidi ni kitendo chako cha kudhoofisha chama cha mapinduzi kwa kutoa siri za vikao vya chama, najua mwenyekiti wako atakuita na atakwambia upime mwenyewe uzito wa tuhuma hizi, ila nakushauri kama kijana mwenzetu usisubiri uitwe, uchukue hatua stahiki za kuachia ngazi kwenye nafasi zote za uongozi ndani ya chama.

tutasikia mengi mwaka huu, kwani cdm wanacheza makida makida wamekuja na hoja nyingine, wameachana na ufisadi na katiba mpya, kipya sasa ni nape, tangu nape atoa makombora, siku hizi kila kiongozi wa cdm akipanda jukwaani anafungulia kaseti ta wimbo wa nape tu. Angalizo muachane na siasa za jina moja, nape mugeukie namna ya kutatua kero za watz!
 
Hii mada imenifurahisha kidogo labda na mimi nitoe mchango wangu kidogo.moja kwa moja nakubaliana na wale wanaomuona Nape Mnafiki kwa sababu.
1.Unapokua hukubaliani na sera za upande mmoja unachotakiwa ni kutundika madaruga yako na kwenda kule ambako unafikiri mtaongea lugha moja,na ndio maana sina shida na wale wanaohama kwa either kunyimwa madaraka ndani ya chama kwa kuonewa au vinginevyo.

2.Unapokua ndani ya fungate ya chama fulani maana yake ni kwamba umekubaliana nacho hivyo yapasa uendane na sera hizo,kama kuna usiyokubaliana basi uyamalizie humo.

3.Unapokua unatumikia chama,mwajiri au ni sehemu ya familia fulani yapasa kulinda haki ya kupata na kutotoa siri za upande uliopo kwani kwa kufanya vinginevyo wewe si mwaminifu,ni mtu hatari katika hiyo jamii.

Ujumbe wangu;
Nape kama hakukubaliana na CCM alipaswa kuachana nao(kuvua Gamba-maana halisi)halafu akaenda upande mmoja CCJ,au CDM tukajua anachokipigania,lakini sio kutoa siri za CCM ukazipeleka kuzianzishia CCJ,(hapo hakuna confidentility,)na huo sio uongozi.Unafiki ni kitu kibaya sana.Huwa unabeba kitu kinaitwa undumila kuwili.Unaloliongea sio unalolitenda na kumaanisha ,bali kuna jingine nyuma ya pazia.Kwa hiyo napata shida na wale wanaotaka kumpa ushujaa kijana huyu.

Na ndio maana kwa mwajiri mzuri unapotaka kazi kwako moja atataka kujua uzoefu wako,maana ya kwanza kujua kama umekutana na challenges kiasi gani ambazo utamsaidia pindi ukianza kazi,lakini la pili na la muhimu ulikotoka uliondokaje? Hapo ndio kwenye umuhimu mkubwa,kwani unapokua huendani na mwajiri wako utaomba kuacha kazi kwa kufuata taratibu husika bila kuharibu sifa ya mwajiri wako kwa sababu ulikua sehemu ya ile familia,mabaya au mazuri ni sehemu ya maisha yale,unatakiwa kuyaacha na kwenda kuanza maisha mapya.kama unapiga mawe piga ukiwa nje sio ndani,na ukipiga ukiwa ndani tuna haki ya kukufukuza.

Naomba nisiwachoshe nina mengi ya ku-mtima tutaongea wakati mwingine.kina NAPE NI WATU HATARI KWA TAIFA LETU.
 
haa haa MKuu naona unajitahidi kuwa mtetezi saana wa magamba mapya hongera.
lakini tusikimbiane mkuu tena siku zijazo.

- No mkuu you know me, ukweli ni ukweli, uongo ni uongo na siasa ni siasa, Mtandao 2005 walishajitayarisha kuingia Chadema, wala sio siri sasa nini cha ajabu hapa? Huyu Mpendazoe anaonekana kuwa mchanga sana kisiasa unakimbia chama kwa sababu umeambiwa utafukuzwa? Mbona wenzake wote aliokua nao CCJ, bado wapo CCM na wote wamepewa nafasi za uongozi wa juu?

- Huko Chadema angalieni sana hawa viongozi wachumia tumbo, sasa huyu mkimpa siri zenu siku akinyimwa nafasi akatoka si atazitoa tu! No wonder CCM walimruhusu aondoke! walishajua kwamba ni hafai!

ES!
 
- I mean ni Demokrasia at work, tatizo ni kama Mpendazoe kwa kujitoa CCM na kuingia Chadema amevunja sheria ya jamhuri au mnafiki, none ishu kama chama changu naona kinakosa mwelekeo ninayo haki ya kutumia kila njia za kisiasa kutafuta attention ya kusikilizwa na chama changu, kwani CCM haijui waliotaka kuanzisha CCJ?

- National politics ndivyo zinavyochezwa, CCM waliwajua sana wale wote walioshiriki CCJ, lakini inafanyika tathmin ya chama ya kisiasa, kuona umuhimu wao wakiachiwa watoke, chama kinaona haikwezi kua-afford, kwa hiyo wanaitwa na kuulizwa tatizo lao wanasema na sometimes wanapewa nafasi katika chama kurekebisha waanayoona hayafai, that is how national politics is played, Mpendazoe was not a threat to CCM wakamruhusu aondoke na wengine wote walioruhusiwa kuondoka, it has nothing to do na unafiki it is simply how national politics are played!

Es!
Ofcourse it is simply how national politics are played and how people are being fooled.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom