Nape ni mwanzilishi wa CCJ

Hii kama si ila bali sifa kwa Nape hivi!

Anaonekana mpiganaji ambae yuko tayari kuichinjia baharini CCM kama haijajisafisha.

Btw haiingii akilini kuwa CCM haikujua kuwa Nape ni mwanzilishi wa CCJ. Wamempa cheo wakijua alichokifanya.
 
Bwana Butola kama unadhani hii ni strength kwa Nape ni mawazo yako wengine tunaona ni kama kijana kadandia treni kwa mbele, unafikiri ndani ya CCM hakuna watu wanaoweza kusema kama anavyofanya yeye, jibu ni rahisi tu wanajijua madhambi yao hawataki kuanzisha vita vya mawe wakati wao wako kwenye nyumba ya kioo, wamemtanguliza Nape kama kafara wao sasa aangalie watakavyomruka hataamini macho yake. Ni hivi karibuni tu utasikia Nape anavutwa shati na kutulizwa amuulize Magufuri na Tibaijuka, si umesikia kuna vigogo sita waanzilishi wa CCJ ambao bado wako CCM na vyeo vyao sasa unadhani watapenda kutajwa kama alivyotajwa Nape.

Mkuu Quinine..

Utaniambia siku moja, ndani ya CCM hii sio issue kwa sababu ata kabla ya kumpa hiyo nafasi waliyajua yote haya, na nje ya CCM hii ni opportunity kwa Nape na CCM, hii ni sawa na kumpatia pasi ndani ya 18, hatari!!

Hii publicity ya Nape kama mtu aliyekuwa hajaridhishwa na mambo yalivyokuwa yanaenda ndani ya CCM inampa sasa opportunity nzuri ya kuwafikia wote waliokuwa wamekatishwa tamaa na CCM na ufisadi uliokuwa unaendelea..
 
Mkuu wala hakuna shida hapo.

Ninachokiona hapa ni Chadema sasa kuanza kucheza ngoma ya Nape na kumpa Nape sifa ya "mpambanaji aliyekuwa hajaridhishwa na mambo yalivyokuwa yanaendelea ndani ya CCM", hii itawapa zaidi hamasa wananchi ya kutaka kumsikiliza zaidi na kumwamini pale anaposema CCM inabadilika na sasa mafisadi hawana nafasi, itamsaidia sana hii publicity kujenga case yake ya CCM mpya iliyojivua gamba.

Hoja hii itawafanya wasio wanaCCM wamwamini zaidi anapozungumzia kubadilika kwa CCM na kuwapa mtazamo wa pili wale waliokuwa wamekatishwa tamaa na CCM kama alivyokuwa yeye sababu ya kurudi kundini.

Hii ni strength kwa Nape na wala sio weakness kama mnavyodhani, hii publicity ya Nape kama mtu aliyekuwa hajaridhishwa na mambo yalivyokuwa yanaenda ndani ya CCM inampa sasa opportunity nzuri ya kuwafikia wote waliokuwa wamekatishwa tamaa na CCM na ufisadi uliokuwa unaendelea.

Chadema walipaswa walione hili kabla majuto hajawa mjukuu.

hata makamba alikuwa mropokaji kama nape!!ccm kujivua gamba ni kuwango'a mafisadi tu na si kujibishana na cdm,kwani walishafanya hivyo miaka 6 iliyopita bila mafanikio.
 
Mkuu Quinine..

Utaniambia siku moja, ndani ya CCM hii sio issue kwa sababu ata kabla ya kumpa hiyo nafasi waliyajua yote haya, na nje ya CCM hii ni opportunity kwa Nape na CCM, hii ni sawa na kumpatia pasi ndani ya 18, hatari!!
Kumbe CCM huwa wanafanya madudu kwa makusudi leo ndio umenipa mwanga hata Makamba na Tambwe waliwaweka pale makusudi wakivuruge chama ili waje kujivua gamba, kwa hiyo unataka kusema wamemuweka Nape makusudi akibomoe chama then baadaye waje wajivue gamba jingine if that then it is a good strategy.
 
Now I'm getting to the Understanding kwa nini CCJ Ilikufa

1: Usaliti: Mpendazoe aliwekwa Mbele halafu akasalitiwa na Wenzake
2: Uchu wa Madaraka: Kwamba baada ya CCJ kufa Kijana akaenda CHADEMA kuomba kugombea Ubunge kwa Jimbo la Ubungo akatoswa akapiga U-turn
3: Baada ya kupewa Ukuu wa Wilaya akaitosa kabisa CCJ

Kwa Hiyo NAPE ni Msaliti na MPENDA Madaraka I think hii ni Tafsiri yangu
 
nimegundua kwamba anachofanya Nape ni makusudi kabisa kuhakikisha ccm inadhoofika ..... !
 
Bwana Butola kama unadhani hii ni strength kwa Nape ni mawazo yako wengine tunaona ni kama kijana kadandia treni kwa mbele, unafikiri ndani ya CCM hakuna watu wanaoweza kusema kama anavyofanya yeye, jibu ni rahisi tu wanajijua madhambi yao hawataki kuanzisha vita vya mawe wakati wao wako kwenye nyumba ya kioo, wamemtanguliza Nape kama kafara wao sasa aangalie watakavyomruka hataamini macho yake. Ni hivi karibuni tu utasikia Nape anavutwa shati na kutulizwa amuulize Magufuri na Tibaijuka, si umesikia kuna vigogo sita waanzilishi wa CCJ ambao bado wako CCM na vyeo vyao sasa unadhani watapenda kutajwa kama alivyotajwa Nape.

Mkuu CCM kama chama cha siasa lengo lake ni kuendelea kuongoza serikali, hawawezi kujimaliza wenyewe, na ndio sababu ya kujivua gamba.

Huu ndio ujumbe wa Nape juu ya CCM Mpya....

"Lakini pia kule Dodoma tumetoka na maazimio kadhaa lakini kubwa ni kwamba tunaelekea katika mambo mapya, tumesema ‘Towards New CCM.' Kwa hiyo tutakiimarisha chama kuanzia ngazi ya chini kabisa. Kama nilivyosema awali kwamba tunaboresha mfumo wa kuwapata wanachama wapya."

Nape anasema kwa mfumo wa siasa uliopo leo, CCM haikuwa na njia nyingine zaidi ya kukubali mabadiliko hayo makubwa kuwahi kufanyika ndani ya chama hicho kwa maslahi ya chama na Tanzania kwa ujumla.

"Kuna mapinduzi makubwa yanakuja. Viongozi wetu wajipime upya. Maadili kwa wengi wao yamepotea. Kwa hiyo basi nawaomba wajipime upya kama kuna mtu anajiona ni mchafu na hataki kubadilika basi ajiondoe kabla ya kuondolewa,"

Katibu huyo wa NEC Itikadi na Uenezi aliwataka wanachama wa CCM ambao walihama kwa hasira au kutokana na ufisadi, warudi kwani sasa Chama ni kipya.

"Sasa tunajenga CCM mpya kwa mazingira na mahitaji ya wanachama... hakuna sababu ya kununa tena. "Nimepata salamu nyingi ya watu, hasa vijana kutaka kurudi baada ya kujivua gamba, nasema rudini,"

alisisitiza. Alisema kazi ya kijivua gamba kwa Chama itaendelea kwa awamu hadi kufikia ngazi zote.


Sasa wakati Nape akiendelea kuutangaza ujumbe huu, Mpinzani anakuja na kuanza kumfagilia bila kujua kuwa huyu jamaa alikuwa hapendezwi na mambo yalivyokuwa yanaenda ndani ya CCM na alikuwa na mpango wa kuunda chama cha kupingana na ile CCM ya Zamani, huku si kumfanya aonekane ni mtu makini zaidi na anayejua analolifanya?huku si kuufanya ujumbe wake wa CCM Mpya uaminike zaidi kwa wananchi?tafakari..
 
Hili gazeti mbona halijaibalance hii taarifa?zimewekwa tuhuma za EPA na tuhuma za Nape kugombea Ubunge kupitia Chadema bila kuweka majibu ya Nape kwenye masuala hayo, hii sio sahihi, i guess hili ni la Tanzania Daima hili, gazeti la Uhuru la Chadema.

Kimsingi sioni hoja hapa, CCM inatambua kuwa kuna wanachama wake waliokuwa wamekatishwa tamaa na mwelekeo ya chama chao na ndipo walipokuja sasa na mpango wa kujivua gamba ili kuwarudishia wanachama hawa matumaini mapya na kuwafanya warudi kundini, kwa mantiki hiyo CCM hawana shida na Nape kuwahi kutaka kujitoa na kuanzisha CCJ, sasa pilipili wasiyoila yawawashia nini Chadema? naona Nape anawapa tabu sana.

Lakini lingine...hivi unaenda Mbambabay unaongelea mambo ya Nape na CCJ wakati wananchi unaowaambia ata hawajui kama CCJ ni mdudu au ni mnyama? Huku ni kupoteza nafasi ya kuwaeleza wananchi mambo yanayowahusu wao na maisha yao na namna gani Chadema itayabeba matarajio na changamoto zao kwa kesho bora zaidi.
Huna lolote, kwani tuhuma za Nape dhidi ya Chadema si alitoa akiwa Singida? Au wananchi wa Singida wameendelea kuliko wa Mbamba Bay? Hakika CCM inaelekea kufa maana ubaguzi na dharau kwa wananchi imeshamiri kiasi hiki.Iwe Mbamba bay au Dar ujumbe umefika na ndio maana wewe uliyepo mjini umepata taarifa hii. Halafu kwamba Nape hakupata nafsai ya kujibu wewe sio mfuatiliaji au unaleta ushabiki. Hivi kuwa CCM akili lazima zihamie tumboni? Siku zenu zinahesabika
 
Mkuu wala hakuna shida hapo.

Ninachokiona hapa ni Chadema sasa kuanza kucheza ngoma ya Nape na kumpa Nape sifa ya "mpambanaji aliyekuwa hajaridhishwa na mambo yalivyokuwa yanaendelea ndani ya CCM", hii itawapa zaidi hamasa wananchi ya kutaka kumsikiliza zaidi na kumwamini pale anaposema CCM inabadilika na sasa mafisadi hawana nafasi, itamsaidia sana hii publicity kujenga case yake ya CCM mpya iliyojivua gamba.

Hoja hii itawafanya wasio wanaCCM wamwamini zaidi anapozungumzia kubadilika kwa CCM na kuwapa mtazamo wa pili wale waliokuwa wamekatishwa tamaa na CCM kama alivyokuwa yeye sababu ya kurudi kundini.

Hii ni strength kwa Nape na wala sio weakness kama mnavyodhani, hii publicity ya Nape kama mtu aliyekuwa hajaridhishwa na mambo yalivyokuwa yanaenda ndani ya CCM inampa sasa opportunity nzuri ya kuwafikia wote waliokuwa wamekatishwa tamaa na CCM na ufisadi uliokuwa unaendelea.

Chadema walipaswa walione hili kabla majuto hajawa mjukuu.
Only a f**l can belive that ccm has changed namafisadi hawana nafasi,sishangai watu mnapo itetea ccm kwa sababu kuna watu ambao wana direct interest kwenye ccm.Lakini kwa wale tunaotizama kwa jicho la tatu hatuwezi tukakubaliana na hilo.Fisadi gani ambaye hana nafasi ccm.Vinara watatu bado wapo na nafasi yao katika chama kwa sababu bado ni wanachama wa ccm.JK ambaye ndio mlezi wa ufisadi na fisadi (refer list of shame) yupo.Fisadi yupi ambaye hana nafasi sasa.Kawambieni wajinga kwamba mafisadi hawana nafasi ndani ya ccm.Ukiulizwa hata wewe kujivua gamba maana yake ni nini,hakuna lolote waambieni watu ambao hawajaenda shule kama wale wa singida wanaolishwa sumu na akina nape na chilly
 
Hili gazeti mbona halijaibalance hii taarifa?zimewekwa tuhuma za EPA na tuhuma za Nape kugombea Ubunge kupitia Chadema bila kuweka majibu ya Nape kwenye masuala hayo, hii sio sahihi, i guess hili ni la Tanzania Daima hili, gazeti la Uhuru la Chadema.

.

When you have too much Guess unapoteza Objectivity Mkuu Jaribu kuyaweka Mapenzi yako kwa Nape Pembeni ili Uone Mapungufu yake na Umsaidie lakini Kulindama Tanzania Daima inaonesha Una Chiki Binafsi Mkuu
 
Mkuu Mbopo kama huoni tatizo wewe utakuwa na tatizo, uaminifu wa Nape kwa chama chake uko wapi mtu anataka kukisaliti chama kabaki huko kwa sababu ya u-DC bado mnaamini kweli ni loyal kwa chama if so then something is wrong somewhere in CCM, kitakuwa ni opportunistic party ndiyo maana kuna siku Prof. Safari na Marando walisema kama ni unafiki Nape ni number one siku ile sikuwaelewa.

acheni kumsakama Nape....Stephen Wassira alikuwa nani na saivi ni nani? Hizo ni siasa tu na kwenye siasa uadui haudumu
 
CCJ yamuumbua Nape
• Alitumika kuandaa katiba, kupokea fedha, kutafuta ofisi ya CCJ


SIRI za Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, zinazomhusisha na mipango ya kuwahi kukigeuka chama chake na kuanza taratibu za kujiunga na Chama Cha Jamii (CCJ), zimezidi kuanikwa na wale aliokuwa nao katika mipango hiyo.

Baada ya wanasheria na wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mabere Marando na Profesa Abdallah Safari, kumtaja Nape kuwa mmoja wa wana CCM wanafiki, jana ilikuwa ni zamu ya Fred Mpendazoe kueleza kile alichokiita "unafiki, usaliti na uhaini wa Nape Nnauye ndani ya CCM anayojifanya kuipigania."

Mpendazoe aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Kishapu kwa tiketi ya CCM katika Bunge lililopita, alijitoa mapema mwaka jana na kujiunga na CCJ kabla ya kuhamia CHADEMA.

Akihutubia mamia ya wakazi wa mji wa Mbamba Bay katika mfululizo wa maandamano na mikutano ya hadhara ya CHADEMA inayoendelea kwenye mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Mpendazoe alisema sasa ameamua kuliambia taifa ukweli kuhusu Nape Nnauye ili umma wa Watanzania uepuke kudanganywa na propaganda za CCM zinazotolewa na kijana huyo.

Huku akiweka wazi kuwa yeye ni mmoja wa waanzilishi wa CCJ, Mpendazoe alisema kelele zote anazopiga Nape kuitetea CCM leo hii ni za kinafiki kwani tayari alishakiona chama hicho hakifai na akashiriki katika mipango yote ya kuanzisha CCJ.

Akitoa mfano wa jinsi Nape alivyoshiriki katika kuanzisha CCJ, Mpendazoe alisema kijana huyo alishiriki kuandika katiba ya chama hicho.
Alisema ndiye aliyepewa jukumu la kutafuta nakala za katiba za vyama vingine tawala nchini Afrika, ili kupata katiba nzuri ya kuigwa katika kuandika Katiba ya CCJ.

Aliwaambia wakazi wa Mbamba Bay kuwa Nape alilitekeleza vizuri jukumu hilo, kwani alifanikiwa kuipata Katiba ya Chama cha ANC kinachotawala Afrika Kusini, ambayo alisema ndiyo iliyotumika kwa kiasi kikubwa katika kuandika Katiba ya CCJ.

"Huyu Nape anayepiga kelele za kuitetea CCM kujivua gamba ni mnafiki mkubwa pengine kuliko wanafiki wote hivi sasa. Nathibitisha kwa wananchi wa Mbamba Bay na Watanzania wote kwa ujumla kwamba Nape Nnauye alishiriki kuanzisha CCJ. Nilikuwa naye; tulikuwa wana CCM sita. "Nape ni mhaini ndani ya CCM kwa sababu alishakula njama za kutaka kuiangusha, tofauti na Nape, mimi nilijiamini mapema na nilijitoa CCM mapema baada ya kuona hiki chama hakiwafai Watanzania.

Sasa leo wanajivua gamba halafu Nape wanampa cheo. Niwaulize, hivi kati ya Nape na Lowassa yupi ni mbaya na kwa CCM? Ni Nape aliyeona CCM haifai na kushiriki kuanzisha CCJ ili kuiangusha au ni Lowassa?" alihoji Mpendazoe na umati ukajibu "Wote hawafai." Kisha aliendelea:
Tulifanya naye vikao vyote vya siri hadi tukaanzisha CCJ, leo anaitetea CCM, ni mnafiki mkubwa", alisema Mpendazoe na kushangiliwa.

Katika hotuba yake hiyo iliyoonekana kuteka hisia za mamia ya wasikilizaji, Mpendazoe alisema CCJ ilianzishwa kwa siri kubwa na Nape alishiriki kikamilifu katika kuhakikisha mawasiliano yao yote yanakuwa ya siri kwani walifungua mtandao maalumu wa kuwasiliana kwa internet.
Hata hivyo, alisema baadaye wenzake waliufuta mtandao huo baada ya kubadili mawazo dakika za mwisho, hasa baada ya kuahidiwa vyeo na Rais Kikwete.

Alisema hata pale ilipolazimu kukutana, yeye, Nape pamoja na wengine, walikuwa wakipendelea kukutana kwenye vinywaji eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam ili wasitiliwe shaka na maofisa Usalama wa Taifa aliosema walikuwa wakiwapeleleza wana CCM wote waliohisiwa kula njama za kuanzisha chama kipya.

Mpendazoe aliyewahi kuwa msemaji wa CCJ taifa kabla ya chama hicho kunyimwa usajili wa kudumu, alisema Nape alibadili mawazo ya kujiunga CCJ dakika za mwisho baada ya Rais Jakaya Kikwete kumuahidi na hatimaye kumteua kuwa mkuu wa Wilaya ya Masasi. Alibainisha kuwa kitendo hicho kinaonyesha jinsi kijana huyo asivyo na msimamo na alivyo na uchu wa madaraka.

"Lengo letu la pamoja lilikuwa ni kupinga uongozi mbaya wa CCM na ufisadi tukiwa nje ya CCM, maana haiwezekani kupambana na ufisadi ukiwa ndani ya CCM. Ukifanya hivyo unakuwa adui. Lakini kumbe mwenzetu ndani ya moyo wake kilichomsukuma kuanzisha CCJ ni kukosa cheo kikubwa ndani ya CCM.

Sasa hilo sikulijua, nililijua baada ya Rais Jakaya Kikwete kumteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi. Hapo alibadili mawazo ya CCJ. Ni kijana msaliti, mnafiki na asiye na msimamo, hafai kuongoza watu, ana uchu wa madaraka … kama si kupewa ukuu wa wilaya Nape asingekuwa CCM leo. "Alikuwa anatazama tu majaliwa ya tumbo lake. Huyu naye ni fisadi lakini hajavuliwa gamba, wanafiki watupu", alisema Mpendazoe na kuamsha shangwe zaidi.

Aidha, alieleza kuwa ili kuwaepuka maofisa Usalama wa Taifa, wakati mwingine walikuwa wakifanya vikao vyao vya kuanzisha CCJ ndani ya gari pamoja na Nape akiwepo.

Alieleza zaidi kuwa Nape akiwa idara ya mambo ya nje ya CCM katika ofisi ndogo ya chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam, ndiye aliyekuwa akiiba siri za CCM zilizohusu kuwafukuza wote waliohisiwa kuwemo kwenye mpango wa kuanzisha chama kipya cha siasa.
Alieleza kuwa Nape anayemjua yeye ni mtu asiyeukubali uongozi wa Rais Jakaya Kikwete katika chama na serikali, kwani katika vikao vyao vya mwanzoni kabisa walivyoazimia kuanzisha CCJ, kijana huyo alikuwa akimkosoa Kikwete na kuelezea udhaifu wake.

"Na ndiye tuliyekuwa tukimtuma kwa wafadhili kupokea fedha za kuanzishia CCJ. Ndiye aliyetafuta pango la ofisi ya CCJ. Kwa kuwa yeye alikuwa kijana zaidi, alifanya mambo mengi ya kufuatilia kwa siri taratibu za uanzishwaji wa chama.

"Kikwete anaongoza chama feki, CCM ina watu ambao walishamdharau kama Nape na ambao wanamuona ni kiongozi dhaifu…lakini kwa sababu mwenyewe aliwapa vyeo bila kuwajua, leo wamelazimika kubakia ndani. Mimi siwezi na ndiyo maana leo nipo CHADEMA nikiendeleza dhamira ile ile ya kuwanusuru Watanzania na ufisadi," alisema na kushangiliwa tena.

Aliwataka wakazi wa Mbamba Bay kutorudi nyuma na kurubuniwa tena na CCM inayosema imejivua gamba, kwani suala hilo limejaa usanii na unafiki mkubwa. Alisisitiza kuwa kote alikopita na CHADEMA amejiridhisha kuwa chama hicho sasa ndiyo kipenzi na tumaini pekee la Watanzania.

"Mimi sitarudi nyuma kama Nape, nitasonga mbele na CHADEMA, tumekwenda kwenye vijiji na miji mingi, CHADEMA ndiyo tumaini pekee la Watanzania….ndugu zangu tusirudi nyuma, huu ndiyo wakati wa kujikomboa. Kila haki na wakati wake…tusiipoteze fursa hii," alisema. Wakati Mpendazoe akitoa tuhuma hizo juzi, Nape alikaririwa na vyombo vya habari kuwa hajawahi kushiriki katika CCJ huku akiwatuhumu wanaomhusisha nayo wanafanya hivyo kwa lengo la kumchafua.
 
acheni kumsakama Nape....Stephen Wassira alikuwa nani na saivi ni nani? Hizo ni siasa tu na kwenye siasa uadui haudumu
Hii hiamaanishi tuwape blank cheque wanasiasa wasaini kiwango wanachotaka. Taifa lipo njia panda kiuchumi na kijamii, ktk mazingira kama haya wanahitajika watu wanaosimamia ukweli daima na sio vigeugeu ambao wanasukumwa na maslahi binafsi. This guy Nnauye IS USELESS..alianza kupigapiga kelele ili 'kilio' chake kisikizwe, sasa ameskizwa na kilio chake kimetambulika ni kilio cha namna gani (tumbo lake).
 
Huo ni unafiki wa Nape,ni kiongozi asiyeweza kusimama imara katika chama pale kinapo pata msukosuko,kama tofauti kidogo ndani ya Uvccm ilitaka kumhamisha chama je watakapo tofautiana na katibu wake itakuaje? Au tuseme aliyekua mbaya wake wakati ule (Katibu aliyeondoka) kuondolewa madarakani ndiko kuliko mpa imani ya kuendelea na CCM? Na kama ndivyo akitokea mwingine wa kutoelewana naye tuseme atakihama chama chake?.

Nape anapigania vita asiyoijua atangaze sera za chama chake aache kmfuata mtu binafsi
 
Pole mkuu hapo juu hii ndio siasa na imempata mchezaji Taabu ya ccm huwa inamsaka mtu 1 mmoja ambalo ni kosa ktk siasa mwone nape anavyo haha. kumchafua Slaa kashindwa kwan alifikiria slaa atamjbu wanao mjibu wengine,anaenda mbele zaid na kusema cdm imebaka democrasia si kweli ila nape hajui maana ya democrasia

Atalia sana na amewekwa kama vuvuzela pole kijana Nape kuwa Vuvuzela
 
Hii inaonyesha jinsi gani mwenyekiti wa CCM asivyokuwa well informed! Na ninachokiona hapo ni kuwa yeye hukurupuka katika maamuzi yake mengi na wala huwa haangalii yupi ni mtendakazi na badala yake yeye hufikiria kulipa fadhila tu. Ukweli ni kwamba huyo mwenyekiti wa CCM ndo anakiua chama hiki na wala si wengine. Toka alipoanza kuwazushia akina Salim Mohamed Salimu kwamba ni mwarabu hapo ndo alianza kuharibu. Pia ameamua kuwaweka watu wengi kwenye chama na serikali ambao sio kompitenti kabisa ndo ndo maana chama kinayumba na uchumi pia uko taabani. yeye anaendelea kutabasamu as if hajui jema na baya. Watu wameamua kukaa pembeni na kuangalia chama kinavyosambaratika. Naamini ndani ya CCM bado kunawengi ni wanafiki tu
 
Vita umeanza mwenyewe, sasa unalia nini?
Nape unarusha mawe, Vita umeianzishaa!
Mawe warusha vyovyote, hata hauna malengo
Ulianza na Mafisadi, sasa umewagwaya

Mara Slaa mwana zuoni, jiwe ukamrushia,
Umekuwa kama chizi, Unarusha bila dira,
Dawa ya moto motoni, Dawa ya mawe unaipata,
Ulianza na Mafisadi, Aibu umeipata

Aibu umeipata, Mafisadi sasa wako
Sasa unawatetea, Magamba ni nguo zako
Umma hauna chelea, wanapima kwa vigezo
Ulianza na Mafisadi, sasa umetota jasho

Vita umeianzisha, subiri utaipata
Wameanza kupuuza, kumbe hauna dira
Dira yako yote tamaa, na uchu wa madaraka
Ulianza na Mafisadi, sasa unawatetea

Eti kwa ufinyu wako, wadhani bado twalala,
wataka kutuadaa, ili kutupumbaza,
Hatudanganyi kwa kanga, kwa chumvi wala kofia
Ulianza na Mafisadi, mbona wamekushinda

Shirikisha akilizo, Fikiri kabla ya kunena,
Mja na mwana vitendo, Tanzania ndio baba,
Tetea kwanza nchi yako, ndipo utaeleweka,
Mafisadi ulianza nao, sasa unawatetea.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom