Nape: Nchi hii ina wenyewe na wenyewe ni CCM!

Nape katema pumba ambazo ndio wana magamba wanavyowaza wa hii nchi ni mali yao binafsi na ndio maana waiuza watakavyo wanajua sisi wenye nchi wenyewe hatuwezi wafanya chochote kwa kuwa wanatumia poli, usalama wa taifa, PCCB nk kuwalinda na kuibia nchi hii
 
Bado sijaona tofauti ya uropokaji kati ya Nape na Makamba, Nape mropokaji. CCM inaelekea kaburini, Inakufa, inaenda kuanguka
 
Some statements are 50 years too late. Bro usingizi mnono.
Nape/ Nepi Whatever.......... huyu si mwanasiasa ni a political morron anayeendelea kunufaika na mfumo wa magamba toka nyuma. Si mtu wa kumtilia maanani, na with new constitution we will make sure mazezeta kama ghawa wanapotea kabisa katika ramani za kisiasa hapa nchini. Power will intoxicate the best hearts, like wine the strongest heads. No man is wise enough or good enough to be trusted by unlimited power. Nepi we kno the fact that political pigs like you would grow fat where lambs would starve.....your days are nu........
 
Kila mtu hapa anasema 2015 ndio mwizi anashikwa. Kwani? Haiwezekani Kesho Tuanza kupiga kura of "No Confidence"??? Au kama hatupewi hiyo nafasi tuingie barabarani kwa amani kabisa kuionesha Tanzania Kina Nani Ndio Wamiliki Halali?
 
Si bure lazima Nape atakuwa na problem,uwezo wake wa kufikiri unapungua Siku hadi Siku..Tumuombee jamani arudi kwenye Hali yake ya zamani..

Sasa tukimwombea uwezo wake ukaongezeka na hali yake ikarudi kama zamani, CDM itashindaje?

Tulipaswa kumwombea aendelee kuropoka na chuki na jazba kwa wananchi iongezeke, hence ushindi kwa CDM.
 
Akasisitiza wao wapo tayari kusema tuandamane hadi ikulu kuindoa serikali na hawaoni aibu amani endapo itapotea!

Akasema serikali haiwezi kulikubali hilo, naye Nchemba akasema walimu wanaposimamia
uchaguzi wakumbuke kuwa wao ni watumishi wa serikali na endapo CDM isingesaidiwa na walimu basi CDM ingepata kura 1000!

Naomba CCM mkubali tu kuwa umaarufu wenu umekwisha kabisa na sio kuwasingizia walimu. Na msilete ugomvi na walimu kwani ndio wanaotumika kwenye chaguzi zote.

Au hii ni ishara ya chama kufa unapoanzisha uadui na kundi la watu uliokuwa unawategemea?
 
sisi tusiokuwa wa CCM, hatuna nchi,tumefukzwa nchini kwetu na kubaguliwa ndani ya nchi yetu,tuende wapi? tuitafute haki ya uananchi hapa kwetu,nadhani kauli ya Nape c kauli yake binafsi ni kauli ya Chama na ni ajenda ya chama na anaungwa mkono na wanachama wake,Natoa mwito kwa wasio kuwa wana CCM wote popote mlipo muitafute haki yenu ya msingi.Popote mlipo ndani na nje ya Tanzania kumbukeni haki yenu inapokonywa na watu wachache waliolewa madaraka.
 
I personally agree with ths Nape dude. Nchi ya CCM mpende msipende those are the facts. Angalieni people who rule the country are in what political party? The so called high class sijui rich society wote CCM. Sie wengine tu lie tu. hiyo nchi ishauzwa and people who own it ni wana CCM. Those are the facts
 
Taarifa ITV muda huu namwona Nape anadai nchi hii ina wenyewe na wenyewe ni chama cha mapinduzi!

Hivi huyu mtu ana akili kweli? Ina maana wote wasio katika CCM hawana haki na hii nchi?

you are very right bro..mnavyopeana madaraka ndani ya chama kwa migongo ya wazazi wenu ie ww mwenyewe,makamba jr etc,mnavyofisidi nchi ni kama mali ya ccm kweli but time will tell na hizo kauli zako zitakucost
 
Hili jambo si la kubeza,ni jambo kubwa sana,kuna haja tena kwa haraka tuambiwe tusio wana CCM nchi yetu ni ipi,na tupewe muda kujiandaa kuondoka kuelekea kwenye nchi yetu sisi tusio wana-CCM,nahofia isije ikatokea kukamatwa kwa kosa la kuishi nchi ya CCM pasipo kibali,nafikiri hapa kuna agenda ya siri,na kwa vile Nape ni mropokaji huenda amewahi tu kuropoka kabla ya utekelezaji wa jambo lenyewe,inanikumbusha Makamba aliwahi kumkataa Bashe kuwa si raia bila kujali wizara ya mambo ya ndani ilikuwa ikitambua hilo.
Na kama Nape asipojitokeza kutuambia nchi ya wasio wanakaya wa CCM iko wapi,Itatulazimu kulifanyia kampeni kubwa jambo hili na ikibidi kwa maandamano ya amani tukiitaka Serikali ituambie iko wapi nchi ya wasio wana CCM.na ituambie lini CCM waliimiliki nchi hii.
Hawa watu wamelewa madaraka,wamekuwa wapofu,viziwi,na tena wanaonekana ni mataahira waliopata laana ya ufisadi.hivi kweli unawezaje kutamka kitu kama hicho?upande mwingine wanajidai kuhubiri umoja,amani,wanajidai kukemea utengano,je hiki ni kitu gani?ila huyu dogo ni kweli anafikiri kutumia masaburi,hata waliomchagua na anawaongoza wote napata mashaka na fikra zao,nadhani linazidi kutimia ambalo nimewahi kuliseama hapa jamvnini,CCM wamelaaniwa kwa yale wanayowatendea watanzania,kwa dhuluma,unafiki,wizi,unyonyaji wa kila aina,utapeli,mauaji,fitina,uongo na maovu yote wanayo yatenda kila kukicha kupitia tiketi ya chama chao,kimewafanya wakapata laana hata kupoteza uwezo wa kufikiri na kutafakari jambo,hata kama ni jambo ambalo halihitaji elimu ya darasani wao ni issue,wamefikia hatua ya kuazima calculator kwa kupiga heasabu ya 1+1.
Tujihadhari sana na Magamba haya na kauli za kiuwendawazimu zinazotolewa na kina Nape.
 
Wana JF leo nimepata mshtuko wa ajabu baada ya kumsikia Nape akihutubia wana CCM pale Manzese na pamoja na mengi aliyozungumza amesema "Nchi hii ina wenyewe na wenyewe ni CCM".

Je huu ndio uzalendo kweli? Nchi hii ni ya CCM? Na sisi ina maana nchi yetu ni ipi?

Kwa maoni yangu serikali ya CCM imekuwa kama serikali ya mkoloni mzungu, aliyeamini kuwa Africa ni ya kwao na sisi wananchi ni watu wa kutawaliwa. Mashujaa wetu wakawafurusha wakaondoka.

Mawazo yangu ni kuwa wakati umefika wa kuifurusha CCM kwa nguvu ili wajue kuwa nchi hii wenyewe si wao wasio na uchungu na nchi hii kwa kuwafuga mafisadi bali wenye nchi ni wale wenye uchungu wa nchi hii.

Saa ya ukombozi ni sasa.

Nape ni wa kupepewa!!! Huyu ndiye ambae hajijui anatumika kama mpagazi ndani ya ccm, lakini fikra zake ni kama mtoto aliyezaliwa na ukosefu wa Oxygen fikra zake haziko makini. Labda hajitanbui kuwa kwanza hana moral authority ya kutamka hayo mbele ya watanzania, anatakiwa atambue kuwa ccm ndiyo inawenyewe ambamo yeye ameajiriwa kama house boy tu!! na ndio maana wenyewe walipochukia yeye na wenzake walikatazwa kufika Igunga. Sasa akae chonjo na kidomidomi chake maana wakati wowote wanamwondoa.
 
Sasa tukimwombea uwezo wake ukaongezeka na hali yake ikarudi kama zamani, CDM itashindaje?

Tulipaswa kumwombea aendelee kuropoka na chuki na jazba kwa wananchi iongezeke, hence ushindi kwa CDM.

Kaka umesahau kuwa unatakiwa umwombee adui yako mema na aishi siku nyingi, ili unapobarikiwa ajionee kwa macho!
 
Hili jambo si la kubeza,ni jambo kubwa sana,kuna haja tena kwa haraka tuambiwe tusio wana CCM nchi yetu ni ipi,na tupewe muda kujiandaa kuondoka kuelekea kwenye nchi yetu sisi tusio wana-CCM,nahofia isije ikatokea kukamatwa kwa kosa la kuishi nchi ya CCM pasipo kibali,nafikiri hapa kuna agenda ya siri,na kwa vile Nape ni mropokaji huenda amewahi tu kuropoka kabla ya utekelezaji wa jambo lenyewe,inanikumbusha Makamba aliwahi kumkataa Bashe kuwa si raia bila kujali wizara ya mambo ya ndani ilikuwa ikitambua hilo.
Na kama Nape asipojitokeza kutuambia nchi ya wasio wanakaya wa CCM iko wapi,Itatulazimu kulifanyia kampeni kubwa jambo hili na ikibidi kwa maandamano ya amani tukiitaka Serikali ituambie iko wapi nchi ya wasio wana CCM.na ituambie lini CCM waliimiliki nchi hii.
Hawa watu wamelewa madaraka,wamekuwa wapofu,viziwi,na tena wanaonekana ni mataahira waliopata laana ya ufisadi.hivi kweli unawezaje kutamka kitu kama hicho?upande mwingine wanajidai kuhubiri umoja,amani,wanajidai kukemea utengano,je hiki ni kitu gani?ila huyu dogo ni kweli anafikiri kutumia masaburi,hata waliomchagua na anawaongoza wote napata mashaka na fikra zao,nadhani linazidi kutimia ambalo nimewahi kuliseama hapa jamvnini,CCM wamelaaniwa kwa yale wanayowatendea watanzania,kwa dhuluma,unafiki,wizi,unyonyaji wa kila aina,utapeli,mauaji,fitina,uongo na maovu yote wanayo yatenda kila kukicha kupitia tiketi ya chama chao,kimewafanya wakapata laana hata kupoteza uwezo wa kufikiri na kutafakari jambo,hata kama ni jambo ambalo halihitaji elimu ya darasani wao ni issue,wamefikia hatua ya kuazima calculator kwa kupiga heasabu ya 1+1.
Tujihadhari sana na Magamba haya na kauli za kiuwendawazimu zinazotolewa na kina Nape.

Aaah? Jamani tusiongee na mbwa ila tuongee na mwenye mbwa hata Nape??? acheni abwake maana anataka kujikosha kwa Rostam na wenye ccm, we are thinkers lets not talk about people and events but ideas
 
Hayo maneno yanawakera wanasiasa wenyewe na wana kawaida ya kuudhiana, tumewazowea.

Kwa asiye na chama hakuna cha kuumiza kichwa hapo, hiyo itaitwa "siasa tu". Wanasiasa walishaongea mengi, mengine makubwa kushinda hayo na watu waliyapuuzia!!

Kwa asiye na chama kama ana kazi yake anajua kwa uhakika kuwa itaendelea tu, hatofukuzwa Tanzania eti kwa sababu "nchi ina wenyewe". Anajua hawamaanishi, ni siasa tu.

Hali haiwezi kuwa hivyo kwa "wapiganaji" ambao ndiyo hasa walengwa, huku uswahilini tunasema "ujumbe umefika" na kwamba safari hii Ccm nao wanawatia maneno ya maudhi wapinzani wao ambao hawajazowea.

Nafikiria, kama Ccm wangekuwa na saikolojia mbaya kama ya wenzao sijui ingekuwaje wanapoitwa chama cha mafisadi, wanapoambiwa watatolewa ikulu kwa "nguvu ya umma", wanapoambiwa viongozi wao wapigwe mawe.

Agh, ni siasa tu. Tumezowea...
 
Aise hata mie nilipoona hiyo news nikapigwa na butwaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!,ati hii nchi ni ya CCM, kweli nikaona ana akili za kipepeo,chama chenyewe kina harufu ya UFISADI
Kwanza hata walichokua wanakifanya pale jana ni matumizi mabaya ya pesa huku wananchi wa nchi hii wakitaabika kwa hali ngumu ya maisha
 
At least angesema nchi ina wenyewe na wenyewe ni mafisadi na mafisadi ni magamba kidogo ingeleta maana
 
Atuombe radhi watanzania haraka sana la sivyo huo ndio utakuwa mwisho wake katika siasa.
 
Taarifa ITV muda huu namwona Nape anadai nchi hii ina wenyewe na wenyewe ni chama cha mapinduzi!

Hivi huyu mtu ana akili kweli? Ina maana wote wasio katika CCM hawana haki na hii nchi?

huyu ni mtoto kisiasa hana akili kabisa,tanzania ni ya watanzania sisiemu haina hati miliki ya tanzania. Ila ni chama cha mafisadi
 
Back
Top Bottom