NAPE: Nalipenda sana gwanda la CHADEMA

Nape soma alama za nyakati since there is no way sisiem ikawa clean karibu kwa watu ambao wakiongea vitendo vinaonekana!
 
mbona si mara yake ya kwanza kuvaa uniform za Chadema. Kumbuka wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais 2010. Alikubali kuvaa bendera ya Chadema.
 
Mimi kwa kweli huwa namuonea huruma pale ambapo huwa anatumia akili nyingi na za ziada kutetea hoja na mambo ambayoyanafanywa na chama chake ambayo kimsingi yeye binafsi anaufahamu ukweli kuwa anatetea kitu ambacho ni kinyume na mapenzi yake pamoja na matakwa ya watanzania. Najua kweli Nape ana uchungu na nchi yake lakin mazingira alipo hawez kusimamia kikamilifu anachokisema! Mlango u wazi njoo ujiunge na wapambanaji wenzako kaka!
 
huyu jamaa haipendi ccm, yeye anataka upinzani lakini pia anatamani fedha chafu za mafisadi
 
CHADEMA lazima iwe makini sana na hawa wote wenye nia ya kutaka kuhamia katika Chama. Unaweza ukawa mkakati wa Chama Cha Magamba kuelekeza mashambulizi yake kwa CHADEMA kutokea ndani. Yaani iwatume makada wake kadhaa ili wakiaminiwa kupewa nyadhifa ndani ya CDM hapo wajitangazie ushindi wa kukiangamiza CDM. Jihadharini na mamluki wapiganaji wangu!!
 
Afadhali ujisogeze karibu yao CHADEMA ili katika ufalme wao miaka ijayo wakukumbuke! maana inavyoelekea chombo chaenda mrama ila wenzio msimamo wao ni kuwa (katu hawali makombo japo yawe ya biriani)
 
Nape ameshaichoka Magamba kwani alichokuwa anakipigania Magamba hakitekelezeki , anaambulia matusi na fedhea.Anakaribisha kambi ya wapiganaji wa kweli.

Nape hahitajiki CHADEMA, hatuna nafasi ya mtu mwenye mdomo mchafu kama yeye, abaki huko huko, akitoka aende CUF au NCCR Mageuzi. CDM ina, na ni ya watu makini sio walopokaji kama Nape!

Nawaomba wadau msiendelee kutuchafua roho zetu, kumbukeni bado tunasherehekea ushindi wetu Arumeru, Mwanza, Mbeya na Songea. Mmetumwa na Magamba, nini!
 
Nnape hamia chadema kwenye basi lisilojaa kwa makamanda but anza kwanza na kutubu makosa yote mloyafanya ndani ya serikali ya magamba.karibu chadema ccm hamna mzuka wala mvuto kwa karne hii,mmeshachokwa na watanzania.
 
mmeamua kuegemea propaganda zenu kama za ben saanane na kundi lake dhidi ya nape kule india.Chadema mnapinga kujadili watu halafu hapa mnafanya nini.mwacheni nape
 
“Revolution is not a dinner party, not an essay, nor a painting, nor a piece of embroidery; it cannot be advanced softly, gradually, carefully, considerately, respectfully, politely, plainly and modestly.”
Mao Tse-Tung (Chinese stateman, the key figure in China in the 20th century, 1893-1976)
 
At least hana kashfa ya ufisadi anakaribishwa CCM, ila Mwakyembe na Sitta binafsi siwakaribishi ni wanafiki wabaki huko huko, January huwa namkubali anajenga hoja vizuri pia hana kashfa ya wizi. January, Nape njooni tupambane msijali wazee wenu tunalikomboa taifa letu (Tanganyika) pamoja. Peoples Power!
 
1.jpg

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw.Nape Nnauye akiongea na waandishi wa habari leo katika ofisi ndogo ya chama hicho zilizopo mtaa wa lumumba jijini Dar es salaam, juu ya uchaguzi mdogo wa ubunge ulifanyika jana katika jimbo la Arumeru mashariki, ambapo mgombea wa CHADEMA Joshua Nasari ameibuka mshindi kwa kura 32.972, chama cha mapinduzi kimekubali matokeo hayo yaliotangawa na Tume ya uchaguzi leo asubuhi


Nape kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi amempongeza kijana Nasari na kusema "Tunampongeza Joshua Nasari na hakuna hujuma yoyote uchaguzi ulikuwa huru na haki", lakini pia akawapongeza wananchi wa jimbo la Arumeru kwani hiyo ndiyo Demokrasia yao.

NIMEAMUA KUTUMIA VAZI LA CHADEMA KWA KUWA NALIPENDA ; NIMEKOSA UVUMILIVU, KIDUMU CCM

Watamfukuza huyu hebu tusubiri kidogo!!!!!!!!Hata hivyo kwa vijana wenye uelewa hasa waliokwenda shule lazima waone Tanzania inaelekea wapi, mkombozi pekee wanajua kuwa ni CHADEMA!!! VIVA CHADEMA!!!!!!! Ujumbe kwa Bwana Nape!!!!!!!!!!!

 
Back
Top Bottom