lifeofmshaba
JF-Expert Member
- Feb 19, 2011
- 867
- 219
Hivi huyo mbunge ni wa Chama Gani jamani? .... hvi kweli nape ni kakosa ustaarabu kiasi gani kutumia lugha ya matusi hivi?? kama mbunge alichaguliwa na wananchi na si yeye
---Ni mbunge wa CUF anachinganishwa na wananchi waki kimtindo kama ana badala ya kuwambia polisi
--- Nadhani kuna mambo waligongana alipokuwa huko kusini masasi maana hiyo tuhuma ya ulanguzi ni karibu ya kila mnunuzi wa mazao hapa nchini na serikali inalijua hiyo sana tu kama ilivyo kwa madawa ya kulevya
Thursday, 02 September 2010 07:42 |
CUF yaihenyesha CCM kilwa Elias Msuya WAKATI mgombea urais wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na mgombea Ubunge wa Jimbo la Kilwa Kusini kwa tiketi ya chama hicho, Suleiman Said Bungala (*****) wakichanja mbuga wilayani Kilwa, mgombea wa CCM katika jimbo hilo, Ramadhan Madabida amelazimika kusafirisha wanachama wa chama hicho kwa mabasi ili kuhudhuria ufunguzi wa kampeni zake zilizofanyika Kilwa Kivinje jana. Mabasi kutoka vijiji vya Ruyaya, Pande na Lihimalyao yalionekana yakikusanya wana CCM ili kuwapeleka Kilwa Kivinje, umbali wa zaidi ya kilometa 50. Madabida alichelewa kuanza kampeni zake kutokana na mvutano wa wana CCM waliokuwa wakipinga kuteuliwa kwake kuwa mgombea ubunge licha ya kushindwa kwenye kura za maoni na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Hasnain Dewji aliyeenguliwa na Halmashauri Kuu ya CCM hivi karibuni. Zaidi ya wana CCM 2,000 walirejesha kadi zao baada ya kutokea mvutano huo na kukabidhiwa kadi za CUF Kwa hali hiyo alikuwa akiutumia muda huo kuwashawishi wana CCM hao katika vikao vya ndani ili wamuunge mkono kwenye kampeni hizo. Pamoja na kuwashawishi wana CCM, bado mikutano ya CUF inaelekea kupata wafuasi wengi kuliko wa CCM. Baadhi ya wana CCM waliokuwa wakisubiri kusafirishwa walisema kuwa wanalazimika kufanya hivyo ili kukilinda chama chao, lakini hata hivyo bado maamuzi yao yatategemea. "Kura ni siri ya mtu, hapa tunakwenda kwenye mkutano, lakini tutaangalia wa kumpa kura," alisema Mussa Omar mkazi wa Kijiji cha Ruyaya wilayani Kilwa. Naye mgombea urais wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba aliwataka wakazi wa Kijiji cha Lihimalyao kumchagua awe rais na ***** kuwa mbunge wao kuliko kumchagua Madabida ambaye haishi Kilwa. "Unakwenda kumchagua TX Madabida anayeishi Dar es Salaam? Akitoka Bungeni hatakuja Kilwa, bali atakwenda Dar es Salaam. Mchagueni ***** wa hapahapa," alisema Lipumba. ***** ambaye jina lake halisi ni Suleiman Said Bungala ni mume wa aliyekuwa mbunge wa viti maalumu CUF, Mwanawetu Zarafi. |