Nape nakupongeza

Jana nilikuwa namtazama EDWARD LOWASA akichangia hoja bungeni kwa mara ya kwanza toka ajiuzulu, lengo ilikuwa kupima nguvu na uwezo alionao ndani ya ccm baada ya propaganda ya kilivua gamba iliyoanzishwa dhidi yake ukweli ni kwamba Nape anajihangaisha na ukweli wa mambo ni kwamba waliompa hii kazi hawana nia njema na future yake kwani watammaliza mtoto wa watu kisiasa namuonea huruma kwani bado kijana mdogo anapaswa ajiulize kwanini wakubwa wake akiwamo mwenyekiti wake hathubuti kunyanyua mdomo dhidi ya LOWASA? Nape nakushauri swala la kuvua gamba wamekutupia zigo huwawezi hata kidogo wamekudhidi umri na hata ushawishi wewe endelea na kazi zingine za chama ambazo hata hivyo zinaboa kwani wananchi wamekata tamaa na nyie

Nape ni kipofu na ni zao la ufisadi. Nyerere (RIP) alishatueleza kwamba hakuna kiongozi anayetokana na ufisadi atakayemudu kuupiga vita ufisadi.
Nape haiwezi vita dhidi ya ufisadi kwa vile tayari watu wameshaijua bei yake. Mnakumbuka alipopigapiga kelele dhidi ya ufisadi ndani ya CCM hadi kuanzisha CCJ Kikwete alilijua hilo, kwamba ni njaa tu iliyokuwa inamsumbua. Ndiyo maana alimhonga kitu kiduchu tu akamsambaratisha, nacho kilikuwa cheo cha Ukuu wa Wilaya. Kijana alijiona kama amepelekwa nusu ya mbingu na pole pole alianza kuitikia kiitikio cha '"Si CCM wote Mafisadi.... bali wachache...'" Hakuishia pale bali alianza kufurukuta tena kwenye ukurasa wake wa Facebook na mwerevu Kikwete akaona amwongezee zigo la uongozi ndani ya chama chakavu, kilichochakachuliwa na mafisadi na kubakizwa pumba tupu cha CCM ambako aliingia kichwa kichwa na sera yake ya kuwapa aliowaita mafisadi siku 40 kujivua magamba! Sasa ni zaidi ya siku sitini na ameufyata mkia bila ya kuchukua hatua yoyote.
Nape ni mropokaji kama Makamba na Tambwe Hiza, na laana ya kuusaliti msimamo wa kisiasa wa Hayati Baba yake aliyekufa akiwa mwadilifu, mwenye kuheshimiwa na kutukuka na akiwa mjamaa wa kweli itamwandama maishani mwake mwote.
Kina Lowasa, Chenge, Rostam Aziz, Kikwete, Mkono na orodha ndefu ya mafisadi ndani ya CCM ni werevu kuliko Nape na wanajua fika wanachofanya. Kwa vile ni suala la wakati Nape na wapambe wake wataumbuka na kama kawaida mafisadi watashinda.
Vita dhidi ya ufisadi kamwe haitaweza kusimamiwa kikamilifu na CCM - chama kichakavu, kinachougua kansa na kilichokwisha poteza mwelekeo bali chama kipya, chenye ari na dhamira ya kweli kama CHADEMA. Watanzania wameshalijua hilo na ni suala la muda tu kabla hawajachukua hatua. Binafsi naamini 2015 utakuwa ndiyo mwisho wa usanii unaoendelea sasa wa hili dude linaloitwa CCM.
 
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, ametangaza kiama cha walanguzi wa ufuta kwa kuitaka Serikali ya Wilaya ya Kilwa na Mkoa wa Lindi kuhakikisha inakomesha ulanguzi huo mara moja.

Aidha, amemtuhumu waziwazi mmoja wa wabunge, Mbunge wa Kilwa Kusini, Selemani Bungala `*****' (B.we.g.e ili ni tusi) kuwa ni mmoja wa walanguzi, huku akimtaka arejee bungeni kuwawakilisha wananchi wake, badala ya kuwakandamiza kiuchumi.

Nape aliyasema hayo kwa nyakati tofauti katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika mji mdogo wa Kilwa Kivinje na Kilwa Masoko katika ziara ya siku mbili ya baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti ya CCM mkoani Lindi katika kufikisha ujumbe wa maamuzi ya NEC yaliyofanyika mjini Dodoma Aprili mwaka huu.

Kwa mujibu wa Nape wapo viongozi wa kisiasa wanaongoza dhuluma hiyo kwa kisingizio cha kuwasaidia wakulima wakati ukweli wanawadhulumu na kumshushia tuhuma hizo Mbunge wa jimbo hilo, '*****'(Bweg.e) kuwa ni kinara wa dhuluma hiyo.

"Naambiwa Mbunge wenu bwana '*****' (Bweg.e)kaacha Bunge la Bajeti na kuja kusimamia dhuluma yake dhidi ya wakulima masikini wa ufuta.

*****(Bweg.e) rudi bungeni kama hujui kazi yako ni kuwatetea wananchi, basi bora ujiuzulu
wananchi wapate mwakilishi na si mlanguzi" alisema Nape
.

Alisema wakati bei ya dira mwaka huu ni Sh 1,000 ambayo Serikali iliagiza mkulima alipwe yote ndio asubiri malipo ya pili ambayo nayo yatakuwa mazuri kwani bei ya ufuta safari hii ni nzuri, walanguzi wananunua ufuta kwa kati ya Sh 1,150 na Sh 1,200 ambayo ni wizi kwa
wakulima.

Akifafanua wizi huo Nape alisema, ushahidi wa wazi uliopo walanguzi wamechezea mizani yao na kwa kila kilo moja wanaiba kati ya robo na nusu kilo na hivyo bei ya Sh 1,200 wanayonunua walanguzi ni danganya toto kwani tayari wameshafidia kwenye mizani za wizi.

"Mizani za vyama vyetu vya ushirika imepimwa na wakala wa vipimo hivyo ni sahihi na tayariS yenu imeshasimamia upatikanaji wa bilioni kumi na moja kutoka benki za NMB na CRDB kwa ya ununuzi wa ufuta msimu huu, hivyo hakuna sababu ya wakulima wa ufuta kuendelea kudhulumiwa na hawa matapeli," Alisisitiza Nape.

Alisema kuendelea kukwepa mfumo wa stakabadhi ghalani ni kwenda kinyume na maamuzi ya RCC, ambacho ni kikao halali na hata Baraza la Madiwani ambao ni wawakilishi halali wa wananchi.

"Naambiwa wako na baadhi ya madiwani wa CCM wanaojihusisha na dhuluma hii, naagiza ushahidi ukipatikana vikao vya chama mchukue hatua kali dhidi yao, tuko tayari kufanya uchaguzi mdogo kuliko kuvumilia dhuluma hii," alisema Nape.

Mapema, Nape akizungumza na viongozi hao alieleza kwa kina lengo la hatma ya CCM kufanya mabadiliko ‘kujivua gamba' mjini Dodoma na kwamba moja ya malengo ni kukirejesha chama kwenye misingi yake ili kiweze kukidhi kwa dhati matarajio ya wananchi hasa wanyonge.
 
Yaani huyu bwana nimeambiwa ,nimesikia
na maneno kibao ya kuwalaghai wananchi

kama kuna kitu wachukue hatua
 
mwaga nyuki Nape..najua watu wataanza kuponda badala ya kukupa credit hapa

tatizo ni yeye kwenda hapo kusema kisha anapotea, kama ni wizi ni kweli kwa sasa watumishi wa umma na wawakilishi wa jamii katika mambo mbalimbali ni wapolaji

yeye anaposema arudi bungeni hali anamjua ni mlanguzi hiyo inatija kwa taifa kweli?
au ndio ana jijenga kisiasa kwa alimtaja mbunge mlanguzi?

ina maana NAPE anataka kuiambia jamaa leo kwamba ccm inakubaliana na wabunge walanguzi kuwa bungeni?
 
tatizo ni yeye kwenda hapo kusema kisha anapotea, kama ni wizi ni kweli kwa sasa watumishi wa umma na wawakilishi wa jamii katika mambo mbalimbali ni wapolaji

yeye anaposema arudi bungeni hali anamjua ni mlanguzi hiyo inatija kwa taifa kweli?
au ndio ana jijenga kisiasa kwa alimtaja mbunge mlanguzi?

ina maana NAPE anataka kuiambia jamaa leo kwamba ccm inakubaliana na wabunge walanguzi kuwa bungeni?
sasa Nape amfanye nini? keshamwambia jamaa atajirekebisha na kuacha ulanguzi....kwa nini tunapenda sana kumshambulia Nape hata kwenye mazuri? kwazna badilisha tittle ya thread...iandike kiustaarabu acha jazba
 
sasa Nape amfanye nini? keshamwambia jamaa atajirekebisha na kuacha ulanguzi....kwa nini tunapenda sana kumshambulia Nape hata kwenye mazuri? kwazna badilisha tittle ya thread...iandike kiustaarabu acha jazba

Amfanyi nini? kwani kama alikuwa na nia ya kumfanya MBUNGE ajirekebishe bila kumchuia hatua alishindwa kuongea naye kwa faragha mpaka kwenye majukwaa ndio huyo mbunge anaelewa?

huu mchezo wa kuyumbisha wananchi kwa siasa za chuki lazima upigwe vita kama yeye alikuwa na nia ya kumwambia huyo mbunge ili ajirekebishe anajua namba zake za simu alipaswa kumwambia faraghani na sio kwenye majukwaa lakini ni mambo ya kusikia hakupaswa kuyasema kama hana hakika nayo, kama sio ulopokaji
hisitoshe bungeni sio sehemu ya walanguzi

thread heading hiko sahihi unaweza kuanzisha ya kumsifi kama unataka
 
Amfanyi nini? kwa ni kama alikuwa na nia ya kumfanya jamaa ajirekebishe alishindwa kuongea naye kwa faragha mpaka kwenye majukwaa ndio huyo mbunge anaelewa?

huu mchezo wa kuyumbisha wananchi kwa siasa za chuki lazima upigwe vita kama yeye alikuwa na nia ya kumwambia huyo mbunge ili ajirekebishe anajua namba zake za simu alipaswa kumwambia
hisitoshe bungeni sio sehemu ya walanguzi

thread heading hiko sahihi unaweza kuanzisha ya kumsifi kama unataka
fail.jpg
 
Hivi jurisdiction ya Nepi inaishia wapi? Maana naona kila siku anatoa matamko kama yeye ni Naibu Waziri Mkuu
 
nape aanzishiwe thread yake ambayo kila kitu kuhusu yeye kiwekwe ashatuchosha amekuwa kiraka kila mahali anataka kuwepo khaaa! Hiyo thread iitwe HEKAYA ZA NAPE
 
Nape acha maneno mengi yasio na tija kwa jamii shawishi uongozi wako uchukue hatua dhidi ya walanguzi na si kusema na kuacha. Huo ni unafiki. We ndo mlanguzi mkubwa. Kwa sababu kila mkutano wako unawahadaa wananchi kwa maneno yenye sukari. Umeshindwa kuhubiri juu ya mapacha wa chama chako ambao ndiyo 'mabwege' zaidi unakuja kupambana na 'vibwege'.
 
Serikali inaweza kununua tani 350 000 tuu za mahindi tanzania nzima.wakati rukwa pekee wanazalisha zaidi ya tani 1m.jee ziada ipelekwe wapi?ufuta,korosho,mbaazi,alizeti,pamba wanunuzi ni moetl na fidahussein wahindi
 
Amfanyi nini? kwa ni kama alikuwa na nia ya kumfanya jamaa ajirekebishe alishindwa kuongea naye kwa faragha mpaka kwenye majukwaa ndio huyo mbunge anaelewa?

huu mchezo wa kuyumbisha wananchi kwa siasa za chuki lazima upigwe vita kama yeye alikuwa na nia ya kumwambia huyo mbunge ili ajirekebishe anajua namba zake za simu alipaswa kumwambia
hisitoshe bungeni sio sehemu ya walanguzi

thread heading hiko sahihi unaweza kuanzisha ya kumsifi kama unataka
mtoto akinyea mkono wako utaukata na kuutupa?
 
sasa Nape amfanye nini? keshamwambia jamaa atajirekebisha na kuacha ulanguzi....kwa nini tunapenda sana kumshambulia Nape hata kwenye mazuri? kwazna badilisha tittle ya thread...iandike kiustaarabu acha jazba
Hakuna zuri alilolifanya Nape hapo, jambo zuri angeamuru halmashauri imnyang'anye leseni ya kununua mazao huyo mbunge mara moja kwa kuwa ni tapeli na sio kumsema. Kwanza theme nzima ya Nape ni usanii na maneno ya kupandikizwa na viongozi wa ushirika ambayo ni kama majungu. kasema bei dira ni 1000 na wao wananunua kwa 1,150 na 1,200 sasa wizi uko wapi?? Na kwamba wanaiba kwa kutumia mizani, je hakuna mamlaka za udhibiti mizani mkoani humo?? Tuache kutafuta cheap popularity kwa kutumia shida za wananchi. either tukae kimya au tuje na solution na sio porojo wakati anatoka chama tawala chenye authority zote na dola juu. Angeyasema hayo akiwa CCJ tungejua ni kwa kuwa hana dola
 
Hivi huyo mbunge ni wa Chama Gani jamani? .... hvi kweli nape ni kakosa ustaarabu kiasi gani kutumia lugha ya matusi hivi?? kama mbunge alichaguliwa na wananchi na si yeye
 
mtoto akinyea mkono wako utaukata na kuutupa?

kwa hiyo unatetea ufisadi au?
weka sawa kwanza hiyo ndio nitakujibu maana sioni uhusiano wa mtoto na watu wazima na wizi au kuwapola wananchi
mtoto Hana sense za ufahamu kama mtu mzima ndio maana akinya uwezi kumkata mkono wako

sasa NAPE kambeba lini huyo mbunge mpaka anye mkono kwake?
au huyo mbunge ni nini hasichojua kwamba hapo ana wapola wananchi wake?
kwanza hii kesa ni ya kipolisi zaidi kama NAPE amgekuwa msaada kama angewajulisha polisi waweke tego kwa huyo mbunge kuliko kwenda kwenye majukwaa kutafuta manufaa binfsi ya kisiasa cheap popularity
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom