Nape na posho za Wabunge

safi sana vijana inaelekea mnaanza kuwa na akili kidogo. sasa nataka muendelee kujadili kama kweli wanauchungu na hizo pesa kwa nini wawe na uchungu na hizi na wasiwe na uchungu na milioni 7 isiyotozwa kodi wanayomlipa Slaa. Acheni kuwa makasuku hapa hakuna nia yeyote njema zaidi ya kutaka umaarufu. lakini kwa miaka hii yote mitano iliyopita alipokea. Amekumbuka nini mwaka huu? I know Zitto vizuri toka nikiwa naye UDSM. He is the same hajabadilika ila kwa ninyi msiomfahamu endeleeni kula chaka.


Kumbe nia yako ilikuwa ni kutuambia wewe ulisoma na zitto hiyo kali, mimi nilivyoona jina ACHEBE nikajua pointi nitakazozikuta ndani ni za kufa mtu, sasa naanza kupata wasiwasi kama wewe umesoma UD labda ulikuwa FPA pale tena option yako ilikuwa kucheza ngoma pale karibu na ofisi za Daruso sijui kama bado zipo pale au zimehama
 
safi sana vijana inaelekea mnaanza kuwa na akili kidogo. sasa nataka muendelee kujadili kama kweli wanauchungu na hizo pesa kwa nini wawe na uchungu na hizi na wasiwe na uchungu na milioni 7 isiyotozwa kodi wanayomlipa Slaa. Acheni kuwa makasuku hapa hakuna nia yeyote njema zaidi ya kutaka umaarufu. lakini kwa miaka hii yote mitano iliyopita alipokea. Amekumbuka nini mwaka huu? I know Zitto vizuri toka nikiwa naye UDSM. He is the same hajabadilika ila kwa ninyi msiomfahamu endeleeni kula chaka.

Basi kama unatoa hoja kwa misingi ya chuoni utakuwa na wivu sana na huyu Jamaa
atakuwa alikuwa anakukimbiza since then mpaka leo yuko front yako
 
nimesoma Mpango wa maendeleo wa miaka mitano: "THE TANZANIA FIVE YEAR DEVELOPMENT PLAN 2011/12-2015/16".
nimevutiwa na kipengele hiki kizuri ukurasa wa 15:

On the expenditure side, containing Government expenditure will contribute towards ensuring that macroeconomic stability is maintained. This will require enhancing the expenditure control and accountability as well as ensuring value for money. One important area of expenditure is wages and salaries. Consolidation of most of the fringe benefits such as housing, transport and allowances into salaries and wages will be one of the ways of creating an appropriate incentive structure. Sitting and travelling allowances currently create a perverse incentive’s structure, and will need to be rationalized or removed.

Najiuliza ina maana Mustafa Mkullo na ofisi ya bunge hawajui kwa undani mpango huu na mikakati iliyomo ndani yake. kama Mkullo anajua kwa nini anasema posho zitaendelea kutolewa. anataka kutuambia kilichomo kwenye mpango huo ni kiini macho. au mpango umeandaliwa ili kukidhi matakwa ya wahisani kumbe hatuna utashi wa kisiasa.



Nawapongeza chama cha chadema (wakiongozwa na Zitto Kabwe) kuanza kutekeleza kwa vitendo mpango huu ambao ni brand new. Hongera sana CHADEMA.
 
unafikiri basi wanasoma na yanawakaa kichwani ? yanaingilia sikio ya kushoto na yanatokea kulia, ndio maana wachambuzi wamemshangaa Mkulo kuanza kusoma bajeti kabla ya kuusoma mpango huo kwanza kwasababu kuna husianao mkubwa mno na bajeti, sasa yeye kichwa chake ni maji matupu !
 
Think tank ya taifa (tume ya mipango) inafanya kazi vizuri. Tatizo ni hao vilaza ambao kila leo wanapewa semina elekezi.
 
Wabunge wa NCCR - Mageuzi waotoka Kigoma wanamfuat tu Zitto bila kujielewa.
 
sio hao wa ccm tu, hata wa cdm nao wapo nawajua wamejisikia hovyo sna ila wanaona aibu tu mzeee, wanalo mwaka huu.
mahesabu yao yote ya kuezka kwa vigae kwa viposho yamezimwa mwaaaaaaaa, zitto kawapa mtihani mzee

Zitto ni mtu mzito kama jina lake linavyojieleza pale,anauchungu sana mbunge wangu. Ni jembe la ukweli tunajivunia kwa jembe lile, kipindi hichi litawalima sana bungeni, na hizo ni cheche za mwanzo tu. asiyemjua akamuulize mudhihir kuwa who is Zitto, jamaa atakuhadithia vyema
 
Mkuu upo wapi wewe? hoja ya KDI imeshafungwa Zitto ameshakataa kabisa kuchukua hiyo "posho ya kukaa" kuanzia tarehe 8/6/2011.. Kusanyeni hizo posho kwa ajili ya kofia, fulana na mabango 2015.

Kitu unakataa halafu unaelekeza kipelekwe wapi! Inaingia akilini hiyo?
 
Kumbe nia yako ilikuwa ni kutuambia wewe ulisoma na zitto hiyo kali, mimi nilivyoona jina ACHEBE nikajua pointi nitakazozikuta ndani ni za kufa mtu, sasa naanza kupata wasiwasi kama wewe umesoma UD labda ulikuwa FPA pale tena option yako ilikuwa kucheza ngoma pale karibu na ofisi za Daruso sijui kama bado zipo pale au zimehama

Ndugu yangu ina maana sie wa madrasa hatuna haki ya kujadili? Iwapo hoja ya mtu inakuwa dhaifu eti kisa elimu inashangaza. Badala ya kumjibu kwa hoja unakurupuka na kiwango cha elimu kitu ambacho hakijawasaidia watanzania hadi leo kwani wenye kujitapa kuwa mna elimu mnaacha fani zenu na kwenda kuamrisha Maandamano kitu ambacho huko nyuma kikifanywa na magamba ya kijani.
 
ya zitto ni kutafuta umaarufu usio na maana yoyote ile.kilichonishangaza ni kwa yeye kuamua kuachana na posho za bunge at the same time anaamrisha posho hiyo aliyoikataa ippelekwe jimboni kwake ktk taasisi ambayo huenda ameianzisha yeye na huenda katibu wa taasisi hiyo ni ndugu yake.hivyo kwa wasioweza kutafakari wataona amefanya jambo la maana sana kumbe changa la macho.pesa hizo zaweza kuwa zinamrudia kupitia mlango wa nyuma.kuwa makini mtazania.
 
Kuibuka kwa hoja ya baadhi ya wabunge hasa wa upinzani kupinga posho za vikao, nawashauri wasielekeze malipo hayo kwenye common pool, bali waunde umoja na kukusanya mapato hayo na baadaye kwa awamu watumie kwa ajili ya maendeleo vijiji kama kujenga shule, zahanati nk miradi hiyo ikisimamiwa na wabunge wenyewe ili kuleta taswira kamili ya pesa zinazoliwa na wajanja jinsi gani zengeweza ondoa baadhi ya matatizo sugu vijijini.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom